Punguza Mzigo: Kampeni ya Ekuru Aukot yaidhinishwa na IEBC kushinikiza kura ya maoni ya kutaka mageuzi ya katiba Kenya

Tume huru ya uchaguzi nchini Kenya imeidhinisha ombi linaloshinikiza kura ya maoni baada ya kukusanywa saini za wapiga kura milioni 1.2 wanaounga mkono kampeni ya 'Punguza Mzigo'.
Kampeni hiyo iliyoongozwa na chama cha kisiasa Thirdway Alliance Kenya cha aliyekuwa mgombea urais Kenya, Ekuru Aukot, imeidhinishwa kwa lengo la kupunguza kiwango cha mishahara serikalini na matumizi yasio kuwa na faida.
Tume ya uchaguzi nchini IEBC hapo jana ilieleza kwamba Punguza Mzigo imepitisha saini milioni moja zinazohitajika ilikuweza kujaribu kuibadili sheria kupitia jitihada iliyo na umaarufu wa wengi.
Mpango huo unapendekeza muhula mmoja wa miaka 7 kwa rais, kadhalika unapendekeza kupunguza idadi ya wabunge na Maseneta kutoka idadi iliopo sasa ya 416 hadi 147.
Mwenyekiti wa IEBC Wafula Chebukati amesema tume hiyo imeridhishwa na saini zilizowasilishwa, na jukumu hilo sasa la kutaka kuidhinishwa safari ya kura ya maoni litawasilishwa kwa serikali za kaunti 47 nchini.
"Kwa mujibu wa kifungu 257 (4) cha katiba ya Kenya, 2010, tume ilifanya ukaguzi kuthibitisha iwapo kampeni ya Punguza Mzigo inaungwa mkono na wapiga kura angalau milioni moja nchini. Tume imethibitisha ni wapiga kura 1, 222, 541 wanaoiunga mkono. Hii ni kuuarifu umma basi na washikadau wote kwamba mpango huo umefikia masharti yanayohitajika kwa mujibu wa katiba ," alisema Chebukati.
Mkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue
Mwisho wa X ujumbe, 1
Nini kinafuata sasa?
Kwa mujibu wa katiba, baada ya saini kukusanywa na kuthibitishwa safari ya iwapo kutakuwa na kura ya maoni nchini inaelekzwa katika serikali za kaunti ambapo zaidi ya nusu ya idadi ya wajumbe watahitajika kuuidhinisha mswada.
Kwa mujibu wa tume hiyo ya uchaguzi, kawaida pendekezo la marekebisho ya katiba huweza kuwasilishwa kupitia jitihada inayoungwa mkono na wengi, kwa kuwasilishwa ombi lililotiwa saini na wapiga kura angalau milioni moja nchini.
Baada ya kuthibitishwa kwa saini hizo, rasimu ya mswada na saini zilizokusanywa huwasilishwa kwa tume hiyo kwa ukaguzi.
Mkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue
Mwisho wa X ujumbe, 2
Kitakachofuata ni tume ya IEBC inawasilisha mswada huo kwa serikali zote za kaunti nchini ziitathmini na katika miezi mitatu serikali hizo zinatarajiwa kubaini kwa spika wa bunge la taifa na Seneti iwapo wanauunga mkono mswada huo au la.
Bunge nalo likiamua kupiga kura kuunga mkono mswada huo utawasilishwa kwa rais ausaini na kuidhinishwa.
Na iwapo bunge litaupinga mswada huo, basi mswada utawasilishwa kwa wapiga kura kupitia kura ya maoni, kuamua iwapo wanaukubali au la.
Kumekuwa na hisia tofauti miongoni mwa Wakenya kuhusu suala hili huku baadhi wakiiona kama fursa ya kuwawajibisha wanasiasa
Mkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue
Mwisho wa X ujumbe, 3
Baadhi wakilalamika kwamba hawawezi tena kuendelea kufanya kazi kuwalipia wanasiasa mishahara na marupurupu yao.
Mkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue
Mwisho wa X ujumbe, 4
Hata hivyo kuna wale walio na shaka na ufanisi wa kampeni hii.
Mkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue
Mwisho wa X ujumbe, 5
Tony katika ujumbe wake anatathmini uwezekano wa mswada huo kupitishwa katika serikali za Kaunti, akihoji kwamba kuna sababu msingi kwanini 'vizingiti hivyo' viliwekwa.
Ekuru Aukot: 'Daktari wa Katiba'
Baadhi humfahamu kama Daktari wa Katiba kutokana na mchango wake katika kupatikana kwa Katiba Mpya nchini Kenya ambayo ilianza kutekelezwa mwaka 2010.
Dkt Ekuru Aukot, ambaye ni mtaalamu wa masuala ya katiba, alikuwa mkurugenzi na afisa mkuu mtendaji wa Kamati ya Wataalamu iliyohusika katika kuandika rasimu ya katiba hiyo.
Dkt Aukot alizaliwa katika eneo la Kapedo, katika kaunti ya Turkana kaskazini magharibi mwa Kenya.
Babake, Mzee Aukot Tarkus, alikuwa na wake wanne na watoto 27.
Alisomea shahada ya uanasheria Chuo Kikuu cha Nairobi na kufuzu 1997 na mwaka 1999 akahitimu kama mwanasheria katika Chuo cha Wanasheria Kenya.
Baadaye alijiunga na Chuo Kikuu cha Warwick nchini Uingereza na kufuzu na shahada ya uzamili (Sheria na Maendeleo) na uzamifu (Sheria ya Kimataifa kuhusu Wakimbizi) katika uanasheria.
Alifundisha masuala ya Sheria ya Katiba na Utawala katika chuo kikuu cha Warwick kati ya 2005-2005 na baadaye akafundisha katika Chuo cha Uanasheria Kenya kati ya mwaka 2006 na mwaka 2009.
Alianzisha chama cha Thirdway Alliance katika juhudi za kutoa uongozi mbadala na uongozi wa mageuzi kwa Wakenya.
Anaamini Wakenya hawawezi kuwategemea tena viongozi ambao wamekuwa madarakani kufikia sasa kumaliza ufisadi na ukabila.
Mafanikio yake katika kupatikana kwa katiba mpya Kenya yalimfanya kupata kazi karibu sawa na hiyo mataifa mbalimbali barani Afrika.
Alihudumu kama mshauri mkuu wa masuala ya kiufundi wa Shirika la Umoja wa Mataifa kuhusu Maendeleo (UNDP) katika Kamati ya Marekebisho ya Katiba nchini Liberia.
Mwaka 2016, nchini Lesotho alisaidia kuchora ramani ya shughuli ya marekebisho ya katiba nchini humo.
Ametoa mihadhara na kutoa ushauri kuhusu marekebisho ya katiba katika nchi nyingine kama vile Misri, Tunisia, Sudan Kusini, Zimbabwe, Zambia, Ukraine, Ujerumani, mjini the Hague na vyuo vikuu kadha Marekani.