Benki ya Dunia yatofautiana na serikali ya Tanzania kuhusu ukuaji wa uchumi

Mji wa Dar es Salaam

Uchumi wa taifa la Tanzania ulipanuka kwa asilimia 5.2 mwaka 2018 kulingana na benki ya dunia iliosema katika katika ripoti yake kuu mwaka huu ambapo imetofautiana na takwimu zilizotolewa na serikali hiyo za kuimarika kwa uchumi huo.

Kulingana na chombo cha habari cha Reuters, waziri wa fedha nchini Tanzania alikuwa ameliambia bunge mwezi uliopita kwamba ukuwaji huo ulikuwa wa asilimia 7 mwaka uliopita.

Katika ripoti hiyo, kulingana na Reuters, benki kuu ya dunia ambayo hufanya hesabu zake kwa kutumia data ilizonazo pia ilikadriria kwamba uchumi huo utakua kwa asilimia 5.4 ikiwa ni chini ya asilimia 7.1 inayokadiriwa na serikali.

Ukuaji wa mwaka uliopita uliathiriwa na kushuka kwa viwango vya uwezekazji, mauzo katika mataifa ya kigeni na ukopeshaji katika sekta ya kibinfasi, ripoti hiyo imesema.

Kulinga na Reuters, data inayohusiana na matumizi, uwekezaji na biashara inonyesha kwamba ukuaji huo ulipungua mwaka 2018, imesema ripoti hiyo.

Rais John Pombe Magufuli alianzisha mpango wa kuimarisha sekta ya viwanda baada ya kuchukua hatamu mwaka 2015, akiwekeza mabilioni ya dola katika miundo msingi, ikiwemo barabara ya reli, kufufua uchukuzi wa kitaifa wa angani pamoja na kiwanda cha umeme.

Lakini hatua ya serikali kuingilia sekta ya uchimbaji wa madini pamoja na ile ya kilimo imesababisha kupungua kwa uwekezaji katika sekta hizo katika taifa hilo linalotajwa kuwa la tatu kwa ukubwa kiuchumi Afrika mashariki, ilisema ripoti hiyo iliochapishwa na Ruters.

Kulingana na chombo hicho cha habari uwekezaji wa kigeni wa moja kwa moja umepungua maradufu tangu 2013, huku ukuaji wa mikopo katika sekta ya kibinafsi ukipungua na kufikia chini ya silimia 4 mwaka 2018, ikiwa ni kiwango cha chini cha wastani kati ya 2013-16.

Ripoti hiyo ya benki ya dunia inajiri kufuatia ripoti ambayo haikuchapishwa ya hazina ya shirika la fedha duniani IMF mnamo mwezi Aprili ambayo pia ilihoji jinsi rais Magufuli anavyoendesha uchumi wa taifa hilo.

Sarafu ya Tanzania

Kulingana na reuters ripoti iliovuja ambayo ilionekana na chombo hicho cha habari, iliishutumu serikali kwa kukandamiza uchumi huo kupitia sera ''zisizotabirika mbali na zile zinazoingilia kati'', ikisema kuwa ukuwaji wa katikati wa uchumi huo utakua kati ya asilimia 4-5 kwa mara nyengine ikiwa ni chini ya makadirio ya serikali.

Katika ripoti yake, benki ya dunia WB imesema kuwa ukuaji wa kiwango cha uwekezaji ulishuka kwa sababu ya serikali kushindwa kuafikia malengo yake ya matumizi katika miradi ya maendeleo.

Ripoti hiyo inasema kwamba uchumi huo unaweza kunawiri kwa asilimia 6 kufikia 2021 iwapo kutakuwa na uimarikaji wa wa sekta ya biashara, uwekezaji wa kigeni wa moja kwa moja mbali na uwekezaji mwengine wa kibinafsi, ilisema benki hiyo.

Viashiria vingine vya kiuchumi pia vimeonyesha kupungua kwa kasi ya ukuaji wa uchumi.

Upungufu huo uliongezeka hadi asilimia 5.2 ya pato la taifa katika mwaka uliokwisha Januari 2019, kutoka asilimia 3.2 mapema mwaka mmoja uliopita.

Reuters inasema kwamba thamani ya mauzo ya nje imepungua karibu 4% mwaka jana, kwa sababu serikali imepiga marufuku mauzo ya nje ya korosho bidhaa inayoingiza pato la kigeni kutokana na bei yake ya chini.

Kwa upande mwengine , ujenzi wa reli ya kasi ya SGR na upanuzi wa bandari ya Dar es Salaam umesaidia kuimarisha thamani ya mauzo ya kigeni yanayoingia nchini kwa asilimia 7.8%, ilisema benki ya dunia.

Kulinga na reuters serikali inahitaji kupunguza athari za kiuchumi kupitia kuimarisha mazingira ya kibiashara na usimamizi wa fedha , ilipendekeza benki hiyo.