Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Ahmad: Rais wa Shirikisho la soka barani Afrika Caf akamatwa Ufaransa
Fifa imethibitisha kuwa rais wa shirikisho la soka barani Afrika Ahmad anahojiwa na mamlaka nchini Ufaransa.
Taarifa kutoka kwa shirikisho la soka duniani Fifa linasema kuwa anazuiliwa kutokana na madai kuhusiana na jukumu lake kama rais wa Caf.
Iliongezea kwamba Fifa haijui kuhusu maelezo kuhusiana na uchunguzi huo hivyobsi haiko katika nafasi ya kutoa tamko kuhusu swala hilo.
Fifa imeitaka mamlaka ya taifa hilo kuipatia habari ambayo huenda sawa na uchunguzi wa maadili unaondelea katika kamati yake.
Ahmad ambaye ni waziri wa zamani wa Madagascar aliripotiwa kwa kamati ya maadili ya fifa kwa madai ya ufisadi na unyanyasaji na katibu mkuu wa Caf Amr Fahmy. Baadaye Fahmy alifutwa kazi.
Ahmad mwenye umri wa miaka 59, alichukuliwa katika hoteli yake, mjini Paris mapema mwendo wa alfajiri na kuhojiwa na maafisa wa polisi wa Ufaransa wanaokabiliana na uhalifu wa kifedha na Ufisadi, kulingana na vyombo vya habari vya Ufaransa.
Ahmad ambaye pia ni naibu rais wa Fifa alikuwa nchini Ufaransa katika mkutano wa Fifa siku ya Jumatano ambapo rais wake mpya Gianni Infantino alisema kuwa shirikisho hilo limeondoa picha mbaya iliokuwa nayo.
Shirika la habari la Reuters limejaribu kila njia ya kuwasiliana na Ahmad na Caf ili kutoa tamko.
Fahmy alimshutumu Ahmad kwa ufisadi na matumizi mabaya ya mamia ya maelfu ya madola kulingana na maafisa na stakhabadhi zilizoonekana.
Stakhabadhi zilizotumwa mnamo tarehe 31 mwezi Machi na Fahmy kwa kamati ya maadili ya Fifa zilizoonekana na Reuters zilimtuhumu Ahmad akimuagiza katibu wake mkuu kulipa hongo katika akaunti za rais wa Caf.
Wakati huo Ahmad kulingana na Reuters hakujibu ombi la kumtaka kuzungumzia madai hayo yake.
Tangu wakati huo Fifa ilianzisha uchunguzi kupitia kamati yake ya maadili.