Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Champions League: Liverpool ndio mabingwa wapya wa Ulaya baada ya kuilaza Tottenham Hotspurs
Liverpool ndio mabingwa wa kombe la ligi ya mabingwa Ulaya kwa mara ya sita baada ya kuilaza Tottenham katika mechi ilioshirikisha timu mbili za Uingereza mjini Madrid.
Mohamed Salah alifunga goli la penalti baada ya dakika mbili kufuatia masihara ya Moussa Sissoko aliyehusishwa mpira wa mkononi na Sadio Mane katika eneo hatari
Baada ya penalti hiyo, kipindi kilichosalia cha mchezo hakikuwavutia wengi kutoka timu zote mbili hadi pale Divock Origi aliyefunga magoli mawili katika nusu-fainali dhidi ya Barcelona alipoifungia Liverpool goli lao la pili.
Hatahivyo kiwango cha mchezo hakitamjalisha mkufunzi wa Liverpool Jurgen Klopp ambaye alipoteza fainali ya kombe hilo mwaka uliopita kwa Real Madrid.
Hatua ya Tottenham kumuanzisha mshambuliaji Harry Kane ambaye alikuwa akiuguza jeraha kwa kipindi cha miezi miwili haikuzaa matunda.
Spurs ambao hawakupata fursa ya kutekeleza hata shambulio moja hadi dakika ya 73 walipata fursa nzuri ikiwa imesalia dakika 10 wakati Son Heung -min na Lucas Moura aliyeingia katika kipindi cha pili waliposhambulia lakini kipa Allison aliokoa mashambulio yao.
Ni kombe la kwanza la Liverpool chini ya ukufunzi wa Klopp, ambaye alikuwa amepoteza fainali sita ikiwemo fainali mbili za kombe la mabingwa Ulaya.
Na Tottenham waliposhindwa kusawazisha waliadhibiwa na Divock Origi aliyingia kama mchezaji wa ziada na kuhakikisha kuwa mkufunzi Jurgen Klopp anashinda kombe lake la kwanza kama Mkufunzi wa Liverpool baada ya kupiga mkwaju wa kimo cha nyoka uliomuwacha bila jibu kipa wa Spurs Hugo Lloris huku ikiwa zimesalia dakika tatu.
Mkufunzi wa Spurs Mauricio Pochettino alifanya uamuzi wa bahati nasibu bada ya kumchagua nahodha wa klabu hiyo na Uingereza Harry Kane kushiriki katika mechi hiyo licha ya yeye kutoshiriki katika mechi tangu mwezi Aprili kutokana na jeraha la kifundo cha mguu, akichukua mahala pake Lucas Moura aliyefunga magoli matatu dhidi ya Ajax.
Liverpool walishinda kombe hilo ambalo liliwaponyoka msimu uliopita nchini Ukraine na sasa wako nyuma ya Real Madrid na AC Milan kama klabu zilizoshinda kombe hilo kwa mara nyingi.
Kipenga cha mwisho kilizua sherehe kubwa miongoni mwa wachezaji , wasimamizi wa timu pamoja na mashabiki waliojaa katka uwanja wa Wanda Metropolitan.
Kitu kimoja ambacho hakitasahaulika wakati Liverpool iliposhindwa na Real Madrid katika fainali ya kombe hilo msimu uliopita ni picha ya Mo salah akionekana kububujikwa na machozi baada ya kupata jeraha la bega wakati walipokuwa wakipigania mpira na Sergio Ramos.
Ulikuwa wakati ambao ulibadilisha hamu ya mchezo huo ndani ya uwanja huo huku Liverpool ikishindwa kubadili matokeo.
Klopp afuta msururu wa bahati mbaya
Mkufunzi wa Liverpool Jurgen Klopp alijua kwamba mkosi mkubwa wa fainali ya kombe la mabingwa ni kupoteza mara sita fainali ya kombe hilo.
Alikuwa amepoteza mara ya tatu na Liverpool ikiwemo katika kombe hilo msimu uliopita na huku ikiwa hakuna mtu ambaye anaweza kushuku kazi nzuri ya raia huyo wa Ujerumani ni mtangulizi wake katika uawaja wa Anfield Bill Shankly aliyesema kuwa wa kwanza ni wa kwanza na wa pili hajulikani.
Sasa Klopp amejivua gwanda hilo la bahati mbaya na badala yake kujulikana kama mkufunzi ambaye aliipandisha Liverpool katika kilele cha michuano ya Ulaya.
Pochettino alicheza bahati nasibu kwa kumuanzisha Harry Kane
Mwishowe jaribio hilo lilikuwa gumu kulikataa na ilikuwa rahisi kulewa ni kwa nini.
Pochettino alijua kwamba mshambuliaji wake Kane alikuwa mchezaji ambaye alikuwa amewaumiza Liverpool awali na huenda angawaumiza tena hivyobasi akaamua kumwcha Moura nje, mfungaji wa magoli matatu katika nusu fainali ya awamu ya pili dhidi ya Ajax ambayo yaliifanya Tottenham kutinga fainali.
Kane alikuwa hajacheza tangu tangu alipapata jeraha la kifundo cha mguu katika mechi ya robo fainali dhidi ya Manchester City mnamo tarehe 9 Aprili na alionekana wakati aliposhindwa kushawishi mechi hiyo hatua iliomlazimu Moura kuingia lakini hakufanya miujiza yoyote ya pili.
Spurs na Pochettino waliwachwa wakiwa shingo upande huku wakikosa fursa kwa kuwa Liverpool hawakucheza kwa kiwago chao kizuri cha mchezo na mara kwa mara walijikuta wakishambuliwa.
Hatahivyo Pochettino anahitaji sifa kubwa kwa kuifikisha Tottenham katika fainali ya kombe hilo bila ya kukiimarisha kikosi chake msimu huu.
Haitachukua muda mrefu kabla ya kufuata nyayo za Klopp katika kushinda taji lake la kwanza kama mkufunzi nchini Uingereza.