Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Champions League: Barcelona ikiongozwa na Messi yaicharaza Liverpool bao tatu bila huruma
Liverpool watalazimika kujitahidi zaidi msimu huu katika uwanja wao wa Anfield baada ya Barcelona kuwacharaza magoli matatu uwanjani Nou camp katika mkondo wa kwanza wa mechi ya nusu fainali ya kombe la vilabu bingwa Ulaya.
Baada ya kujipata nyuma kupitia bao la Luis Suarez katika kipindi cha kwanza, wachezaji wa Jurgen Klopp walionekana kutawala mpira na kuwa na uwezo wa kusawazisha huku Mohamed Salah na James Milner wakimjaribu kipa Mar-Andre ter Stegen wa Barcelona.
Hatahivyo Barcelona walionyesha kwamba wana uwezo mkubwa kwa kuizuia Liverpool katika lango lake.
Na haikuchukua muda kabla ya Messi kuongeza uongozi wa Barcelona baada ya shambulio la Suarez kugonga mwamba wa goli kabla ya Messi kufunga bao la pili.
Na 'mchawi' huyo wa Argentina alimaliza udhia kwa kuipatia timu yake goli la tatu kufuatia mkwaju wa adhabu.
Hatahivyo Liverpool walikaribia kujipatia bao la kufutia machozi na la ugenini kunako dakika za lala salama wakati shambulio la Roberto Firmino kuokolewa kabla ya Salah kugonga mwamba wa goli.
Liverpool hawana bahati Nou Camp
Ni nini zaidi ambacho Klopp atawataka wachezaji wake kumpatia katika mkondo wa pili wa nusu fainali hiyo siku ya
Jumanne ijayo katika mchuano ambao waliwazuia na kuonyesha uwezo wa kuwafunga wenyeji wao? Pengine bahati ingewaendea .
Sadio Mane ambaye amefunga magoli 15 katika mechi 18 , alikosa bao la wazi kutoka maguu kumi baada ya kupatiwa pasi muruwa na Jordan Henderson kunako kipindi cha kwanza.
Na wakati walipokuwa wakitawala mpira , Ter Stegen aliokoa shambulio lililopigwa na James Milner na baadaye kipa huyo akaruka upande wa kulia kuokoa shambulio jingine la kimo cha nyoka la Mo Salah.
Liverpool walikataa kuona aibu hata baada ya Messi kufikisha bao lake la 600 katika klabu hiyo ya Catalan.
Hatahivyo waliona kana kwamba hawakuwa na bahati mwaka huu huku Firmino na Mo Salah wakikosa nafasi za wazi.
Hatahivyo Liverpool inajulikana kwa kufanya miujiza baada ya kuwa chini 3-0 .
Watalazimika kuonyesha muujiza mwengine wiki ijayo.
Mshambuliaji wa Barcelona Ousmane Dembele angekuwa ameimaliza Liverpool katika dakika za mwisho lakini alipiga mpira katika mikono ya kipa Alisson akiwa amesalia na kipa huyo kufuatia kupa nikupe na Lionel Messi.
Muujiza wa Messi wapunguza presha
Mabingwa hao wa La Liga walikuwa katika kiwango cha pekee huku wakicheza mchezo wa kushambulia kupitia Lionel Messi , Suarez na Phillipe Coutinho.
Pengine ushindi huo ulikuwa muhimu zaidi kwa mkufunzi Ernesto Valverde, ambaye safu yake ya ulinzi ilivunjwa mara kwa mara na Man United katika robo fainali huku ikionekana imara zaidi dhidi ya washambuliaji hatari.
Baada ya presha ya muda mchache walichukua uongozi katika dakika ya 26 wakati Suarez alipokimbia nyuma ya Joel Matip na kufunga krosi ya Jordi Alba.
Mabingwa hao wa Catalan walipoteza mchezo kwa wa Liverpool huku kikosi hicho cha kocha Jurgen Klopp kikizuiliwa kutofunga wakati kipa wa Barcelona alipozuia mashambulizi mawili hatari kutoka kwa Milner na Salah.
Lakini Messi aliondoa wasiwasi wa mashabiki wa Bareclona alipofunga bao lake la kwnza na la pili la Barcelona na kufunga bao lake la pili baada ya dakika saba.