Tetesi za soka Ulaya Jumanne 30.04.2019: Oblak, De Gea, Ferdinand, Fraser, Odegaard, Cavani

Paris St-Germain inafikiria kumnunua kipa wa Manchester United davdi De Gea kwa dau la £90m huku kipa huyo wa Uhispania mwenye umri wa miaka 28 akitarajiwa kulipwa £450,000 kwa wiki na mabingwa hao wa Ufaransa. (Star)

Manchester United inajiandaa kumnunua kipa wa Atletico Madrid mwenye umri wa miaka 26 Jan OBlack. (ESPN)

Mchezaji wa zamani wa Man United na Uingereza Rio Ferdinand amekutana na naibu afisa mkuu mtendaji Ed Woodward ili kuzungumzia kuhusu kuwa mkurugenzi wa michezo katika klabu hiyo (Mail)

Winga wa Bournemouth na Uskochi Ryan Fraser, 25, anajiandaa kuondoka katika klabu hiyo mwisho wa msimu huu kwa kuwa anataka kujiunga na klabu ya juu (Mirror)

Real Madrid wako tayari kumuacha kiungo wa kati wa Norway mwenye umri wa miaka 20 Martin Odegaard ajiunge na Ajax kwa mkopo wa miaka miwili. (Mail)

Chelsea na Manchester United wanachunguza hali ya mshambuliaji wa PSG na Uruguay mwenye umri wa miaka 32 Edinson Cavani, ambaye anataka kujiunga na ligi ya Uingereza.(Calciomercato)

Liverpool inajiandaa kumpatia Alex Oxlade-Chamberlain kandarasi mpya hadi 2023 - siku chache tu baada kiungo huyo wa kati mwenye umri wa miaka 25 kurudi baada ya jeraha la muda mrefu. (Mirror)

Inter Milan inaendelea na mazungumzo ya kutaka kumsaini beki wa Brazil Danilo, 27, kwa dau la £18m kutoka Manchester City. (Mail)

Wolves watajaribu tena kumsaini beki wa Sweden mwenye umri wa miaka 24 Victor Lindelof kutoka Manchester United, baada ya kufeli kumsaini mwisho wa msimu uliopita. (Teamtalk)

Beki wa Ajax na Uingereza Matthijs de Ligt, 19, anatabiri kwamba huenda asigharimu zaidi ya dau alilonunuliwa mchezaji mwenza Frenkie de Jong, aliyenunuliwa na Barcelona kwa dau la £65m, huku uvumi unaozunguka hatma yake ukiendelea.. (Mirror)

Beki wa kulia wa klabu ya Nice na Algeria Youcef Atal, 22, ni miongoni mwa wachezaji wanaolengwa na Chelsea mwisho wa msimu huu iwapo Fifa itaondoa marufuku ya uhamisho wa klabu hiyo. (Telegraph)

Real Madrid imefanya mazungumzo na klabu ya Lyon kuhusu uhamisho wa kiungo wa kati Tanguy Ndombele. (AS)

Beki wa West Ham, 20, na Uingereza Reece Oxford anakaribia kuandikisha mktaba wa kudumu na klabu ya Bundesliga Augsburg kwa thamani ya £8m. (Sky Sports)

Wachezaji wa Arsenal wameshangazwa na mbinu anazotumia kocha wao mpya Unai Emery wakati wa msururu wa matokeo mabaya wa klabu hiyo. (Telegraph)

Mshambuliaji wa Barcelona na Ghana Kevin-Prince Boateng, 32, anasema kuwa angeichezea Man United kwa miaka 10 iwapo angepata motisha (Goal)

Beki wa Brazil Dani Alves, 35, anafikiria hatma yake katika klabu ya Paris St-Germain kufuatia kufungwa na klabu ya Rennes katika fainali ya kombe la Ufaransa. (RMC)

Kipa wa Barcelona na Uholanzi Jasper Cillessen, 30, amethibitisha kwamba ataondoka katika katika klabu hiyo ya Uhispania ili kushiriki mechi nyingi (Marca)

Kipa wa Manchester United Dean Henderson - ambaye yuko kwa mkopo katika klabu ya Sheffield United - anatarajiwa kuanza mazungumzo kuhusu hatma yake ya Old Trafford lakini atataka kusalia katika uwanja wa Bramall Lane msimu ujao. (Express)

TETESI ZA SOKA JUMATATU

Wachezaji wa Manchester United wanataniana 'hadharani" kuhusu tetesi za uhamisho wa Paul Pogba kwenda Real Madrid.

Pogba, 26, ameonekana akiwatania wenzake kuwa anataka kujiunga na Real Madrid. (AS - in Spanish)

Mchezaji nyota wa Chelsea Eden Hazard amepigwa picha akiwa amevalia jezi mpya ya mazoezi ya klabu hiyo.

Hatua hiyo imewapa matumaini mashabiki wa Blues kwamba Hazard ambaye pia ni kiungo kimataifa wa Ubelgiji atasalia Stamford Bridge msimu ujao. (Express)

Ubelgiji inamfuatilia Thorgan Hazard, ambaye ni ndugu ya Eden, na inasema kuwa kiungo huyo wa miaka 26 amekubali kujiunga na Borussia Dortmund na kwamba anasubiri klabu yake ya sasa Borussia Monchengladbach kuidhinisha uhamisho wake. (VTM Nieuws - in Dutch)

Kipa Joe Hart, 32, yuko huru kuondoka Burnley kwa uhamisho bila malipo msimu huu wa joto, huku vilabu kadhaa vya Ligue 1 vikionesha azma ya kutaka kumsajili. (Mail)

Meneja wa Leicester City Brendan Rodgers amesema kuwa klabu hiyo itafanya kila iwezalo kuhakikisha inampampatia mkataba wa kudumu kiungo wa kati wa Monako Youri Tieleman, 21, msimu ujao. (Mirror)

Kiungo wa kati wa Foxe James Maddison ametoa wito kwa klabu yake kumsaini kiungo huyo wa kimataifa wa Ubegiji. (Leicester Mercury)

Kocha wa Chelsea Maurizio Sarri anapigiwa upatu kuchukua nafasi ya Gennaro Gattuso katika klabu ya AC Milan. (Evening Standard)

Manchester United imeungana na Liverpool katika kinyang'anyiro cha kusaini mshambuliaji wa Lille na Ivory Coast Nicolas Pepe, 23 ambaye thamani yake inakadiriwa kuwa paini milioni 60. (Express)

Kiungo wa kati wa Croatia Ivan Rakitic, 31, amesema kuwa atasalia Barcelona hadi mkataba wake wa sasa utakapokamilika mwaka 2021. (Marca)

Nicolas Otamendi ataondoka Manchester City msimu huu, na tayari West Ham na Wolves wanataka kumsaini mlinzi huyo wamiaka 31. (Star)

Mpango wa Chelsea msimu ujao ni huenda ukaathiriwa na marufuku ya usajili wa wachezaji Fifa dhidi yao. (Evening Standard)

Bournemouth wanapania kumsajili beki wa nyuma na kati wa West Brom Dara O'Shea, 20, amabaye amekuwa akichezea klabu ya daraja la pili Exeter City. (Mail)

Kipa wa Barcelona na Uholanzi Jasper Cillessen, 30, amesema kuwa anataka kuondoka Nou Camp msimu huu baada ya kushindwa kumuondo Marc-Andre ter Stegen. (Ziggo Sport, via Marca)

Tetesi Bora Jumapili

Juventus wanataka kumregesha Pogba,Turin lakini watalazimika kuwauza wachezaji watatu muhimu ili wawaeze kumnunua mchezaji huyo wa Manchester United raia wa Ufaransa kwa kima cha pauni milioni 130.(Guadian)

Mabingwa hao wa Italia pia huenda wakajaribu kuipiku Paris St-Germain katika kinyang'anyiro cha usajili wa kipa wa United,28, David de Gea. (Le10 Sport in French)

PSG imeipatia Juventus ofa ya euro milioni 70 kumunua kiungo wa kati Miralem Pjanic, 29 , lakini miamba hao wa Ligi ya serie A wanataka euro milioni 100. (Corriere dello Sport-in Italian)