Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Mkusanyiko wa habari za soka Ulaya Alhamisi: Guardiola, Pogba, Solskjaer, Unai Emery
Wachezaji wa Manchester City watalazimika kuwa watulivu baada ya mechi yao ya debi iwapo wanataka kulihifadhi taji la ligi ya Uingereza.
Magoli kutoka kwa bernand Silva na leroy sane yaliipatia City ushindi wa 2-0 dhidi manchester United na kupanda juu ya Liverpool juu ya jedwali la ligi.
City italihifadhi taji hilo iwapo watashinda mechi tatu zilizosalia.
''Bado hatujakuwa mabingwa huku ikiwa imesalia mechi tatu'', alisema Guardiola, ambaye amewataka wachezaji kuwa watulivu baada ya mechi hiyo ya debi iwapo wanataka kulihifadhi taji
Pogba aorodheshwa katika kikosi bora cha mwaka Uingereza
Wachezaji sita wa Manchester City ni miongoni mwa wachezaji wanne wa Liverpool ambao wameorodheshwa katika kikosi bora cha mwaka cha ligi ya Uingereza -lakini ni kushirikishwa kwa wachezaji waliosalia ambako kumezua hisia.
Licha ya msimu wenye matokeo mabaya kiungo wa kati wa timu ya Manchester United Paul Pogba amejipata katika kikosi hicho cha wachezaji 11 bora, akiwa ni mchezaji wa pekee ambaye hatoki katika klabu mbili za kwanza katika ligi hiyo ya EPL.
Kikosi hicho kilipigiwa kura na achezaji wa ligi ya Uingereza.
Lakini je, Paul Pogba alistahili kushirikishwa katika kikosi hicho? Na iwapo hapana ni nani aliyefaa kushirikishwa?
Solskjaer awataka wachezaji wake kubadili mwenendo
Wachezaji wa Manchester United wanafaa kubadili tabia zaidi ya kila mtu iwapo wanataka kupunguza pengo dhidi ya Manchester City, kulingana na mkufunzi Ole Gunnar Solskjaer.
United, ambao walipoteza 2-0 dhidi ya City katika uwanja wa nyumbani wa Old Trafford siku ya Jumatano wako katika nafsi ya sita wakiwa pointi 25 nyuma ya viongozi hao wa ligi.
Matokeo mabaya katika mechi ya debi ni yao ya saba katika mechi tisa katika mashindano yote.
''Kipindi cha kwanza tulicheza mchezo wa kuridhisha'', alisema Solskjaer.
Hatahivyo tulifungwa magoli rahisi ambayo tungeyazuia.
Unai Emery: Arsenal itatinga nne bora
Arsenal iliopo katika nafasi ya tano katika jedwali la ligi ya Uingereza inaweza kujikwamua na kupanda hadi nafasi nne bora licha ya kupoteza mechi mbili mfululizo, kulingana na mkufunzi wa klabu hiyo Unai Emery.
Magoli kutoka Ruben Neves , Matt Doherty na Diogo Jota aliisaidia Wolves kushinda 3-1 dhidi ya Arsenal, ambayo ilifunga bao la kufutia machozi kupitia kichwa cha Sokratis.
Ilikuwa ni mechi ya pili kupoteza katika kipindi cha siku nne baada ya kupoteza 3-2 dhidi ya Crystal palace nyumbani.
Huku ikiwa imesalia mechi tatu Arsenal iko alama nne nyuma ya majirani zao Tottenham waliopo katka nafasi ya tatu na wana pointi moja chini ya Chelsea walio katika nafasi ya nne.