Mkusanyiko wa habari za michezo Jumatano: Mkufunzi wa Man United Ole Gunnar Solkjaer akiri kwamba sio rahisi kutinga nne bora EPL

Chanzo cha picha, Getty Images
Manchester United inahitaji kushinda mechi tano mfululizo kati ya sita zilizosalia ili kuweza kumaliza katika nafasi nne za kwanza katika ligi ya Uingereza, kulingana na mkufunzi wa klabu hiyo Ole Gunnar Solskjaer.
United ilipoteza kwa magoli 2-1 dhidi ya Wolveshampton na hivyobasi kusalia katika nafasi ya tano wakiwa pointi mbili nyuma ya Arsenal , sawa na Tottenham ambao wako katika nafasi ya nne na pointi moja juu ya Chelsea walio katika nafasi ya sita.
Hatahivyo , United kufikia sasa wamecheza mechi moja zaidi ya timu hizo tatu za mjini London.
Tulihitaji pointi 15 kutoka mechi saba na sasa tunahitaji pointi 15 kutoka kwa sita-''hatuna uwezo wa kupoteza mechi zaidi'', alisema Slskjaer.
''Ni vigumu zaidi ya ilivyokuwa awali''.
Kinda wa Juventus Keane arushiwa matamshi ya ubaguzi

Mshambuliaji wa klabu ya Juventus na raia wa Itali Moise Kean alirushiwa maneno ya kibaguzi kutoka kwa maeneo ya mashabiki wakati wa mechi ya ligi ya Seria A dhidi ya Cagliari siku ya Jumanne.
Kinda huyo mwenye umri wa miaka 19 alishika mikono yake juu baada ya kuifungia Juve bao la pili katika ushindi wa 2-0 akijibu sauti alizokuwa akisikia kutoka kwa maeneo ya mashabiki.
Baadaye aliandika katika mtandao wa ke wa Instagram: Njia mwafaka ya kujibu ubaguzi a rangi.
Mkufunzi wa klabu hiyo Massimiliano Allegri na beki Leonardo Bonucci walisema kuwa Kean anafaa kulaumiwa kutokana na vile alivyosherehekea goli lake.
''Asingesherehekea namna alivyofanya'' , alisema Allegri. ''Ni kijana mdogo na anafaa kupata funzo, lakini pia kuna baadhi ya vitu ambavypo mashabiki pia hawafai kufanya''.
Guardiola: Musiwe na tamaa ya kushinda mataji manne

Mkufunzi wa Manchester City Pep Guardiola ameambia wachezaji wake kusahau kushinda mataji manne.
Mabingwa hao wa ligi ya Uingereza tayari wameshinda taji la Carabao na wanaweza kuilaza Cardiff siku ya Jumatano.
Baaaye watakabiliana na Brighton katika nusu fainali ya kombe la FA siku ya Jumamosi na baadaye Totenham katika awamu ya kwanza ya robo fainlai ya kombe la vilabu bingwa Ulaya mnamo tarehe tisa Aprili.
Katika wiki moja ama siku taytu tunaweza kupoteza mataji yote matatu, Guradiola alisema.
Mkufunzi huyo wa zamani wa Barcelona ameshinda makombe mawili ya ligi na kombe la ligi ya Uingereza msimu uliopita tangu alipojiunga na City mwanzo wa msimu wa 2016.
Bado anasalia kukata tamaa ya kushinda mataji manne msimu huu: Nimewaambia wakati mwingi kwamba niulizeni mwisho wa msimu.
Barcelona yatoka nyuma na kupata ya sare ya 4-4 dhidi ya Villareal

Chanzo cha picha, Getty Images
Viongozi wa ligi ya La Liga Barcelona walifunga magoli mawili ya haraka katika dakika za mwisho ili kupata droo ya 4-4 dhidi ya Villareal katika mechi kali.
Mabingwa hao waliongoza 2-0 kupitia Philippe Coutinho na Malcom.
Lakini Villarela baadaye waliongoza 4-2 huku Samuel Chukwueze , Karl Toko Ekambi , Vicente Iborra na Carlos Bacca wakicheka na wavu.
Mchezaji wa wa Villareal Alvaro Gonzalez alipewa kadi nyekundu huku Barca wakitumia fursa hiyo na mchezaji wa ziada Lionel Messi akifunga kunako dakika ya 90 naye Luis Surez akisawazisha dakika za majeruhi.
Barca wako pointi nane juu ya Atletico Madrid waliopo katika nafasi ya pili kabla ya kipute cha Jumamosi kinchoshirikisha wawili hao katika uwanja wa Nou camp.












