Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Tetezi za soka Ulaya: Hazard, Dzeko, Lukaku, De Gea, Modric, Ake, Heaton, Guardiola
Kiungo wa kati wa Chelsea na timu ya taifa ya Ubelgiji Eden Hazard, 27, anasema katu hatalazimisha uhamisho wake kwenda Real Madrid. (Telefoot, via Sun)
Mlinzi wa Bournemouth ambaye pia anaechezea timu ya taifa ya Uholanzi Nathan Ake, 23, amepuuzilia mbali tetesi kuwa yuko tayari kujiunga na klabu ya Manchester United. (Football Oranje, via Metro)
Manchester United yenyewe kwa sasa inajiandaa kumpatia kandarasi mpya kipa wake David de Gea,27, ambayo itamfanya kuwa mchezaji anayelipwa fedha nyingi katika klabu hiyo. (Calciomercato)
Kipa wa England Tom Heaton, 32, anasema huenda akalazimika kuondoka Burnley kwenye dirisha dogo la usajili mwezi Januari. (Mirror)
Mshambulliaji wa Roma na Bosnia-Herzegovina Edin Dzeko amesema yuko huru kurejea ligi kuu ya England lakini amekiri kuwa huenda "amechelewa sana".
Mchezaji huyo mwenye miaka 32 aliingia dimbani mara 189 katika ligi hiyo katika kipindi cha miaka mitano aliyochezea klabu ya Manchester City. (Sky Sports)
Romelu Lukaku, 25, ambaye ni mshambulizi wa Manchester United na Belgium amegusia ndoto yake ya siku zijazo ya kucheza katika ligi Italia ya Serie A. (Gazzetta dello Sport, via Goal)
Meneja wa Manchester City, Pep Guardiola pia huenda siku moja akahamia Italia, baada ya kusema hana shaka ya kuwa mkufunzi wa moja ya vilabu vinavyoshiriki ya ligi hiyo maarufu kama Seria A. (Manchester Evening News)
Guardiola pia amesema hajui kama Manchester City wako tayari kushinda ligi ya mabingwa. (Times - subscription required)
Inter Milan inajiandaa kufufua azma yake ya kumchukua kiungo wa kati wa Real Madrid na timu ya taifa ya Croatia Luka Modric, 33. (Corriere dello Sport)
Fulham nayo inajitayarisha kwa uhamisho wa mlinzi wa AC Milan na timu ya taifa ya Argentina Mateo Musacchio, 28. (Mirror)
Kiungo wa kati wa Ufaransa Tiemoue Bakayoko, 24, huenda akarejea Chelsea baada ya AC Milan kutishia kufutilia mbali makubaliano ya yeye kucheza kwa mkopo kutokana na ''kusindwa katika michezo yake". (Corriere dello Sport via Mirror)
Kiungo wa kati wa Ubelgiji Mousa Dembele, 31, yuko tayari kuachia kandarasi yake ya Tottenham ili aweze kuhamia Ligi ya Uchina bila malipo. (Sun)