Tetesi za soka Ulaya: Kane, De Gea, Mourinho, Sancho, Tosun, Herrera

Kane

Chanzo cha picha, Reuters

Real Madrid inapania kumsajili mshambulizi wa Tottenham na England Harry Kane, lakini huenda ikashindwa kumnunua mchezaji huyo wa miaka 25 ambaye gharama ya kumsajili ni Euro milioni 200 (El Confidencial - in Spanish)

Manchester United inakabiliwa na kibarua kigumu kumshawishi kipa wa Uhispania David de Gea, 27, kusalia Old Trafford baada ya kandarasi yake ya sasa kumalizika.(Telegraph)

David de Gea

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Kipa wa Manchester United David de Gea

Vilabu kadhaa zinazo shiriki ligi ya Premier vinammezea mate winga wa Borussia Dortmund Jadon Sancho, lakini huenda dau la mchezaji huyo wa miaka 18 likapanda zaidi ya Euro 100 baada ya kuitwa na England wiki hii. (Sun)

Jadon Sancho winga wa Borussia Dortmund

Chanzo cha picha, EPA

Maelezo ya picha, Jadon Sancho winga wa Borussia Dortmund

Meneja wa Manchester United Jose Mourinho anataka kumsajili mlinzi wa Inter Milan na Slovakia Milan Skriniar pamoja na beki wa kati wa AC Milan Alessio Romagnoli, mwezi Januari. (ESPN)

Maafisa wa Manchester United walikua nchini Ureno kuwafuatilia wachezaji kadhaa wa Benfica siku ya Jumapili. (Manchester Evening News)

Alessio Romagnoli

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Alessio Romagnoli beki wa kati wa AC Milan

Mshambulizi wa Everton Cenk Tosun anajiandaa kurejea Besiktas, ambao huenda wakamchukua mchezaji huyo wa kimataifa wa Uturuki wa miaka 27 kwa mkopo mwezi Januari. (MyNet, via Talksport)

Mshambulizi wa Genoa Krzysztof Piatek anafahamu fika kuwa Barcelona inataka kumsajili lakini kuna fununu kwamba Manchester City, Tottenham Hotspur na Liverpool pia zinafuatilia jinsi sogora huyo wa mika 23 raia wa Poland anavyosakata kabumbu. (Diario Sport, via Talksport)

Krzysztof Piatek mshambulizi wa Genoa

Chanzo cha picha, EPA

Maelezo ya picha, Krzysztof Piatek mshambulizi wa Genoa

Kiungo wa kati wa Manchester United Ander Herrera, 29, huenda akarejea Uhispania kujiunga na klabu yake ya zamani Athletic Bilbao mwisho wa msimu huu kandarasi yake itakapomalizika.(El Correo, via Sun)

West Ham nayo inajiandaa kutangaza ofa ya mlinzi wake Declan Rice,19,- ambaye anakibali cha kuchezea mataifa ya Jamhuri ya Ireland na England - kwa kandarasi iliyo imarishwa ya karibu Euro 21,000 kwa wiki. (Football London)

Declan Rice wa West Ham (kushoto) na Paul Pogba wa Man Utd

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Declan Rice wa West Ham (kushoto) na Paul Pogba wa Man Utd

Kiungi wa Kati wa Manchester City, Kevin de Bruyne, 27,anajiandaa kurejea uwanjani baada ya kupona jeraha alilopata wakati wa mchuano wa City dhidi ya Burnley Oktoba 20 baada ya klabu hiyo kuhofia kumchezesha kingo huyo wa kimataifa wa Ubelgiji mjini Liverpool siku ya Jumapili.(ESPN)

Kevin de Bruyne, 27, anajiandaa kurejea uwanjani

Chanzo cha picha, Reuters

Maelezo ya picha, Kevin de Bruyne, 27, anajiandaa kurejea uwanjani

Aston Villa imehusishwa na uhamisho wa mwezi Januari wa mshambuliaji wa Chelsea Callum Hudson-Odoi wa miaka 17. (Birmingham Mail)

Manchester City, Tottenham na Southampton wamekuwa wakimfuatilia mshambuliaji wa Sunderland Josh Maja mwenye umri wa miaka 19. (Mirror)

Daktari wa Liverpool Matt Konopinski anatarajiwa kuiacha klabu hiyo na kuenda England kuchukua wadhifa mpya baadaya ya kuwa Anfield kwa muda mrefu. (Liverpool Echo)