Tetesi za soka Ulaya Jumatatu 08.10.2018: Zinedine Zidane, Paul Pogba, Jose Mourinho, Henry, John Terry, Brendan Rodgers

Chanzo cha picha, Getty Images
Agenti wa Zinedine Zidane, 46, kocha wa zamani wa Real Madrid ambaye amehusishwa na Manchester United, amesemahuenda asiiongoze klabu hiyo inayocheza katika ligi kuu ya England. (Marca)
Paul Pogba aliisaidia Man Utd kupata ushindi wa kusisimua wa mabao 3-2 wa dhidi ya Newcastle baada ya Jose Mourinho kumshauri kuhusu mbinu za mchezo huo wakati wa muda wa mapumziko. (Sun)
Mshambuliaji wa zamani wa Arsenal anapigiwa upato kuwa meneja wa Aston Villa huku John Terry, 37, akitarajiwa kuwa msaidizi wake. (Express na Star)

Chanzo cha picha, Getty Images
Arsenal huenda ikamsajili mshambuliaji wa Paraguay Miguel Almiron mwezi Januari mwakani. Mchezaji huyo wa miaka 24 amefunga mabao 12 mwaka huu kwa akiwa na MLS Atlanta United.
Ataihama klabu hiyo kwa kima cha Euro milioni 15 mwisho wa msimu huu utakaokamilika mwezi Desemba.(Daily Mirror)
West Brom itarejea na ofa nyingine kwa Bradley Dack wa Blackburn mwezi Januari msimu wa uhamisho wa wachezaji baada ya juhudi zao za kumchukua kugonga mwamba kiungo huyo wa kati wa miaka 24 msimu wa joto. (Birmingham Mail)

Chanzo cha picha, Getty Images
Mshambuliaji Manolo Gabbiadini amekiri kuwa angelitafakari ofa alizopata msimu wa jota laiti angelijua ataendelea kusalia Southampton. Mchezaji huyo alianza kucheza katika ligi ya Premia msimu huu siku ya Jumapili lakini akatolewa uwanjani kabla ya mechi kumalizika. Watakatifu hao wa St Mary's waslishindwa 3-0 na Chelsea.
Meneja wa Chelsea Maurizio Sarri amedokeza kuwa Ruben Loftus-Cheek aliachwa nje ya kikosi katika mechi dhidi ya Southampton kwa sababu kiungo huyo alicheza dakika 70 siku ya Alhamisi.

England na Tottenham wana hofu kuhusiana na hali ya Danny Rose baada ya Mauricio Pochettino kuthibitisha kuwa mchezaji huyo wa miaka 28 anakabiliwa na tatizo la mara kwa mara la kinena (London Evening Standard)
Meneja wa Crystal Palace Roy Hodgson anasema hakuna miujiza itakayobadilisha mkondo wa mchezo wao baada ya kushindwa mara tatu katika mechi nne katika uga wa Selhurst Park (Football London)

Lucas Digne wa Everton, 25, amepuuzilia mbali uwezekano wa kuzuka uhasama kati yake na Leighton Baines,33, kuhusiana na nafasi ya beki wa kushoto baada ya kuishindia nafasi katika kikosi cha kwanza (Liverpool Echo)
Bora kutoka Jumapili
Wakuu wa Manchester United wamemshauri Zinedine Zidane kutotafuta umeneja kwingine wakati wakiamua hatma yake Jose Mourinho. (Mirror)
Mashabiki wa United walipigwa picha na sanamu ya meneja wa zamani wa Real Madrid Zinedine Zinade, 46 nje ya Old Trafford kabla ya ushindi wa siku ya Jumamosi dhidi ya Newcastle. (Eurosport)
Machester United watahitajika kumlipa Mourinho pauni milioni 29 ikiwa watamfuta meneja huyo mwenye maiaka 29 lakini kiwango hicho kitashuka hadi pauni milioni 10 ikiwa atamaliza msimu na United washindwe kumaliza katika nafasi za Ligi ya Mabingwa. (Mirror)
Mourinho alifichua kuwa alipokea ujumbe wa imani naye kutoka bodi ya Manchester United kabla ya ushindi wa mabao 3-2 dhidi ya Newcastle. (Times)

Chanzo cha picha, Getty Images
Manchester City watahitaji kuvunja rekodi yao ya kusaini wachezaji kumsaini kiungo wa kati wa Lyon Tanguy Ndombele baada ya klabu hiyo ya ufaransa kumwekea thamani ya pauni milion 70 mchezaji huyo wa miaka 21 mwezi Januari. (Star)
Manchester United wamemuambia Paul Pogba kuwa hatauzwa mwezi Januari licha ya mfaransa huyo wa miaka 25 kuripotiwa kuwa na nia ya kujiunga na Barcelona baada ya wao kuonyeha nia ya kumsaini. (Mail)














