Tetesi za Soka Ulaya Jumapili 30.09.2018: Mbappe, Mourinho, Zidane, Pogba, Mbappe, Hazard, Morata

Kylian Mbappe

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Kylian Mbappe

Manchester City wanataka kuvunja rekodi ya kununua wachezaji kwa kumsaini mshambuliaji wa Paris St-Germain Kylian Mbappe, 19 kwa pauni milioni 200. (Sun on Sunday)

Manchester United wanaamini kuwa meneja Jose Mourinho anaweza kufutwa kazi mwishoni wa wiki ijayo huku wachezaji wakizungumzia uwezekano wake kufutwa walipokuwa wakirudi nyumbani baada ya kushindwa kwa mabao 3-1 na West Ham siku ya Jumamosi. (Mail on Sunday)

Lakini United wanasema ripoti kuwa wamezungumza na meneja wa zamani wa Real Madrid Zinedine Zidane kuchukua mahala pake Mourinho hazina msingi. (ESPN)

Alexis Sanchez

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Alexis Sanchez

Mourinho alimkosoa mshambuliaji wa United Mchile Alexis Sanchez, 29, mbele ya wachezaji wenzake kabla ya kumtoa kutoka kwa kikosi kilichocheza Jumamosi. (Sunday Mirror)

Barcelona wanamtaka kiungo wa kati wa United Paul Pogba, ambaye aliambia wiki hii kuwa hawwezi kuwa nahodha wa Manchester United tena lakini wanaweza kumsaini mchezaji huyo wa miaka 25 msimu ujao badala ya mwezi Januari. (Sunday Express)

Mshambuliaji wa Chelsea Alvaro Morata, 25, atauzwa kweda Juventus mwezi Januari. (Sun on Sunday)

Eden Hazard

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Eden Hazard

Chelsea wanamfuatilia ndugu wa miaka 15 wa mshambuliaji Mbeljii Eden Hazard, 27, na kiungo wa kati Kylian, 23. Ethan Hazard anaichezea klabu ya Ubelgiji ya AFC Tubize. (Sunday Mirror)

Cristiano Ronaldo anaamini bao lake dhidi ya Juventus akiwa na Real Madrid lilikuwa bora zaidi kuliko la Mohammed Salah lililomshindia mshambuliji huyo wa Liverpool tuzo ya Fifa la Puskas Award. Lakini mreno huyo aliongeza kuwa Salah, 26 alistahli tuzo hiyo. (L'Equipe - in French)

Mohammed Salah

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Mohammed Salah

Kipa wa Liverpool Alisson, 25, anasema mchezaji mwenzake Philippe Coutinho - ambaye aliondika Anfield na kujiunga na Barcelona mwezi Januari - alimsaidia kuamua kujiunga na Ligi ya Premier. (Goal)

Mkurugenzi mkuu wa zamani wa Manchester United na Chelsea Peter Kenyon anajaribu kupanga kuinunua Newcastle kutoka kwa Mike Ashley. (Guardian)

David Luiz

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, David Luiz

Meneja wa Liverpool anafikiri muda wa mshambujia Daniel Sturridge kwa mkopo huko West Brom ulikuwa mzuri kwa mchezaji huyo mwenye miaka 29. Muingereza uyo alifunga bao la kusawazisha huko Chelsea siku ya Jumamosi kuendeleza kutoshindwa kwa Liverpool. (Daily Star Sunday)

Mlinzi wa Chelsea raia wa Brazil David Luiz, 31, anasema angeondoka klabu hiyo msimu uliopita ikiwa Maurizio Sarri hangechukua mahala pake Antonio Conte kama meneja. BT Sport)

Pep Guardiola

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Pep Guardiola

Meneja wa Manchester City Pep Guardiola anaamini mitandao ya kijamii inawza kuleta matatizo kati ya meneja na wacheaji wao. (Independent)

Meneja wa Southampton Mark Hughes anasema atakifanyia mabadiliko kikosi chake baada ya kushindwa kwa mabao 2-0 na Wolves. Saints wameshinda mechi moja na kupoteza nne za Ligi ya Premier msimu huu. (Talksport)

Mshambuliaji wa zamani wa Newcastle Shola Ameobi anasema hajastaafu. Mchezaji huyo mwenye miaka 36 amekuwa bila klabu tangu aondoke huko Notts County mwisho wa msimu uliopita. (Sky Sports)

Bora Kutoka Jumamosi

Zinedine Zidane

Chanzo cha picha, Zinedine Zidane

Maelezo ya picha, Zinedine Zidane

Kocha wa zamani wa Real madrid Zinedine Zidane ameanza kujifunza utamaduni wa kiingereza kwa ajiri ya kumrithi Jose Mourinho akiachana Manchester United. (Sun)

Aliyekuwa kocha msaidizi wa Mourinho kwa miaka 17, Rui Faria akiwa chini ya Mourinho ameanza kutafuta timu ya kuinoa kama Kocha mkuu. (Times)

Jose Mourinho

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Jose Mourinho

Wachezaji wawili wazoefu Juan Mata na Nemanja Matic wote 30, wamekuwa wasuluhishi wa migogoro Old Trafford baada ya kuzuka sitofahamu katika vyumba vya kubadilishia nguo vya wachezaji hao. (Sun)

Kiungo mshambuliaji wa Tottenham na England, Dele Alli, 22

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Kiungo mshambuliaji wa Tottenham na England, Dele Alli, 22

Kiungo mshambuliaji wa Tottenham na England, Dele Alli, 22, atakuwa nje mwezi mmoja kwa mara nyingine baada ya kupata majeruhi katika kifundo cha mguu wake.

Kiungo wa klabu ya Aston Villa na mchezaji wa zamani wa England chini ya umri wa miaka 23, Jack Grealish ameingia mkataba wa miaka mitano ulioambatana na kipengele ya kumruhusu kuondoka klabuni hapo kwa dau la pauni millioni 45. (Times - subscription required)

Beki wa pembeni wa City na raia wa Ufaransa Benjamin Mendy anaweza asiwe na mda mrefu kuitumikia Manchester city baada ya Pep Guardiola kuchoshwa na majeruhi ya mara kwa mara ya beki huyo. (ESPN)

Kinda wa Fulham Ryan Sessegnon, 18, amepoteza uzito wa misuli yake mpaka kufikia 7kg tangu kumalizika kwa msimu uliopita. (Express)