Tetesi za soka Ulaya Jumamosi 29.09.2018

Kocha wa zamnai wa Real madrid Zinedine Zidane

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Kocha wa zamani wa Real madrid Zinedine Zidane

Kocha wa zamani wa Real madrid Zinedine Zidane ameanza kujifunza utamaduni wa kiingereza kwa ajiri ya kumrithi Jose Mourinho akiachana Manchester United. (Sun)

Aliyekuwa kocha msaidizi wa Mourinho kwa miaka 17, Rui Faria akiwa chini ya Mourinho ameanza kutafuta timu ya kuinoa kama Kocha mkuu. (Times - subscription required)

Wachezaji wawili wazoefu Juan Mata na Nemanja Matic wote 30, wamekuwa wasuluhishi wa migogoro Old Trafford baada ya kuzuka sitofahamu katika vyumba vya kubadilishia nguo vya wachezaji hao. (Sun)

Kiungo mshambuliaji wa Tottenham na England, Dele Alli, 22

Chanzo cha picha, Reuters

Maelezo ya picha, Kiungo mshambuliaji wa Tottenham na England, Dele Alli, 22

Kiungo mshambuliaji wa Tottenham na England, Dele Alli, 22, atakuwa nje mwezi mmoja kwa mara nyingine baada ya kupata majeruhi katika kifundo cha mguu wake.

Kiungo wa klabu ya Aston Villa na mchezaji wa zamani wa England chini ya umri wa miaka 23, Jack Grealish ameingia mkataba wa miaka mitano ulioambatana na kipengele ya kumruhusu kuondoka klabuni hapo kwa dau la pauni millioni 45. (Times - subscription required)

Beki wa pembeni wa City na raia wa Ufaransa Benjamin Mendy anaweza asiwe na mda mrefu kuitumikia Manchester city baada ya Pep Guardiola kuchoshwa na majeruhi ya mara kwa mara ya beki huyo. (ESPN)

Kinda wa Fulham Ryan Sessegnon, 18, amepoteza uzito wa misuli yake mpaka kufikia 7kg tangu kumalizika kwa msimu uliopita. (Express)

Kiungo wa Chelsea Jorginho

Kiungo wa Chelsea Jorginho, 26, ameweka bayana kuwa alichagua kujiunga na The Blues na kuikacha Manchester City kwa sababu ya Mauricio Sarri baada ya kufanya kazi nzuri pamoja katika klabu ya Napoli nchini Italy kwa miaka mitatu. (ESPN Brasil)

Mshambuliaji wa wa Atletico Madrid na timu ya taifa ya Hispania Diego Costa amesema kutoelewana na Antonio Conte ndiko kulimfanya aihame klabu na yeye sio mkosaji katika hilo. (Marca)

Mlinda mlango wa Liverpool Alisson, 25, amesisitiza kuwa ubora wake akiwa golini sio majivuno ili aonekana vizuri kwenye kamera. (Guardian)

Kocha wa timu ya taifa ya England Gareth Southgate amepanga kumuangalia kiungo mshambuliaji wa Leicester city James Maddison, 21, katika mchezo dhidi ya Newcastle wikiendi hii akiwa na mpango wa kumjuisha timu ya taifa kinda huyo. (Telegraph)

Maddison, alijiunga na Mbweha hao kwa dau la pauni milioni 20 akitokea Norwich msimu uliopita, amesema anajituma mwenyewe bila kuangalia majukumu ya timu ya taifa. (Mirror)

Kiungo mshambulaiji wa Liverpool na raia wa Uswisi Xherdan Shaqiri
Maelezo ya picha, Kiungo mshambulaiji wa Liverpool na raia wa Uswisi Xherdan Shaqiri

Kiungo mshambulaiji wa Liverpool na raia wa Uswisi Xherdan Shaqiri, 26, amekanusha taarifa kutoka kwa mchezaji wa zamani wa Stoke Charlie Adam alipomtuhumu Mswisi huyo anakumbukwa tu kwa kukosa Penati iliyopelekea timu hiyo kushuka daraja msimu uliomalizika wa 2017/2018. (Evening Standard)

Mlinda mlango wa Fulham Marcus Bettinelli, 26, amesema alikuwa anasafisha jiko alipopokea taarifa ya kushangazwa ya kuitwa timu ya taifa ya England. (Mail)

bayern

Chanzo cha picha, EPA

Bayern Munich imepanga kumsainisha winga wa zamani wa Newcastle kwa sasa Marseille na timu ya taifa ya Ufaransa Florian Thauvin, 25, lakini watatakiwa kulipa pauni millioni 80 kwa. (Ouest-France - in French)

Kiungo wa Atletico Madrid na raia wa Hispania amesema hata siku moja hawezi kusaini Real Madrid ingawa alikaribia kujiunga na Barcelona. (Cadena Ser, via Sport)

Everton imemsimamisha mkuu wa kusaka vapaji wa klabu hiyo baada ya kuwashawishi wachezaji wadogo kujiunga na Ligi kuu England. (Mail)