Mourinho kwa Pogba: hakuna mchezaji mkubwa kuliko Man United

Kocha wa Manchester United Jose Mourinho amethibitisha kuwa kiungo wake Paul Pogba atacheza kwenye mchezo wa kesho dhidi ya West ham ingawa amesisitiza hakuna mchezaji mkubwa zaidi ya klabu.
Hii inakuja baada ya picha fupi ya video kusambaa siku ya Jumatano ikiwaonyesha wawili hao wasioiva katika chungu kimoja wakikwaruzana.
Mourinho amesema ana mahusiano mazuri na Pogba,25, pamoja na kuwa alimwambia hataendelea na unahodha tena katika timu ya Manchester United.
'Kesho atacheza, ni mchezaji kama wachezaji wengine'
"Hakuna mchezaji mkubwa kuliko timu'. Ninafuraha anavyofanya kazi yake, kama nisingefurahia asingecheza, nimefurahishwa zaidi na mazoezi yake wiki hili, amefanya mazoezi kweli, timu inahitaji mchezaji mzuri na Pogba ni mchezaji mzuri." amesema
Akizungumza kama mgogoro wa katikati ya wiki utaleta athari yoyote amesema Manchester United ni kubwa kuliko yeyote hapa, lazima ni tetee hilo.
Hii inakuja baada ya Mourinho kumwambia Pogba hataendelea kuwa nahodha tena.
"Nilimwambia Pogba, Wachezaji na Viongozi wezangu sababu ya kwanini hataendelea kuwa Kapteni msaidizi, hivyo wote wanajua sababu ya kumuondoa Pogba kuwa nahodha wa timu.
Hakuna mchezaji amefanya vizuri kama Pogba

Chanzo cha picha, Getty Images
Alipoulizwa kwanini hakumsalimia Pogba wakati wa mazoezi, Mourinho amesema hakumsalimia Pogba kwa kuwa ni muhimu kufanya mazoezi kuliko kusalimiana. Hivyo hajali hata kama kamera zilikuwepo. 'Zipo kwa ajiri ya kutuchonganisha'
'Aliongeza kuwa hakuna mchezaji mwingine alifanya vizuri Jumanne, Jumatano na Alhamis kama Pogba'
Mourinho alianza kukwaruzana na Pogba Jumatano baada ya kusambaa picha iliyomuonyesha Paul na Andreas Pereira wakicheka baada ya kumalizika kwa mchezo dhidi Derby Country wa Kombe la Ligi ambapo Manchester United ilipoteza mchezo huo.
Akiulizwa Pogba alikanusha taarifa za kusambaa picha za kufurahia kufungwa kwa Manchester united akisema picha aliirusha kabla ya mchezo huo kufanyika hivyo alikuwa hacheki sababu hiyo.
Mourinho alikubaliana na maelezo ya kiungo wake, huku akivishutumu Vyombo vya Habari kuwa vinakuza migogoro isiyokuwa na umuhimu na kuchochea vurugu ndani ya timu.












