Tetesi za Soka Ulaya Jumatano 26.09.2018: Ronaldo, Messi, Sako, Gotze, Hazard, Wenger

Chanzo cha picha, Getty Images
Rais wa Real Madrid Florentino Perez anaamini mshambuliaji wa Ureno Cristiano Ronaldo, 33, siku moja atarudi katika klabu hiyo. Ronaldo alijiunga na Juventus mwezi Julai baada ya miaka tisa huko Bernabeu. (ESPN)
Ronaldo na mshambuliaji wa Barcelona Lionel Messi, 31, wamejikuta kwenye mzozo baada ya kukosa kufika kwenye sherehe za tuzo za Fifa. (Marca via Express)

Chanzo cha picha, Getty Images
West Brom wanatarajiwa kumsaini wing'a wa zamani wa Crystal Palace Bakary Sako, 30, wiki hii. Mchezaji huyo wa kimataifa raia wa Mali amekuwa bila ajenti tangu akatae ofa ya mkataba kutoka Palace. (Sky Sports)
Arsenal wanammezea mate wing'a wa Rennes mwenye miaka 20 raia wa Senegal Ismaila Sarr ambaye amefananishwa na mchezaji wa Barcelona Ousmane Dembele. (Mirror)

Chanzo cha picha, Getty Images
Mmililki wa Chelsea Roman Abramovich anahitaji sio chini ya pauni bilioni 3 kuweza kuiuza klabu hiyo. (Bloomberg)
Msaidizi wa Chelesea Gianfranco Zola anaaminia wing'a Mbelgiji Eden Hazard, 27, hajafikia kiwango chake cha juu zaidi na anaweza kuwania tuzo za juu kwenye kandanda. (Telegraph)
Mkurugenzi wa kiufundi wa shirikisho la FA Dan Ashworth, 47, yuko kwenye mazungumzo kuhusu wajibu kama huo uko Brighton. (The Guardian)

Chanzo cha picha, Getty Images
Mlinzi wa zamani wa Liverpool Jamie Carragher ameunga mkono uamuzi wa mlinzi Declan Rice 19, wa kukataa ofa ya mkataba huko West Ham. (Talksport)
Mmiliki wa Monaco Dmitry Rybolovlev anataka kuiza klabu na kuna ripoti za wanunuzi kutoka Marekani na UAE. (le10sport.com - in French)
Fifa ilitumia karibu pauni milioni 9 kwa ndege za kukodisha chini ya miaka mitatu ikiwemo kwenye safari kwenda kutazama jengo la Taj Mahal. (The Independent)

Chanzo cha picha, Getty Images
Arsene Wenger hana uhakika kuhusu kurejea kwa usimamizi wa kandanda lakini mfaransa huyo mwenye umri wa miaka 68 anasema bado hajastafu baada ya kuonoka Arsenal msimu uliopita. (L'Est Republicain via Evening Standard)
Celtic wanakumbwa kifo cha taratibu kwa sababu hawawezi kushindana kifedha na ligi kuu za Ulaya kwa mujibu wa rais wa Juventus Andrea Agnelli. (The Scotsman)
Bora Zaidi Kutoka Jumanne
Manchester United na Real Madrid wana mipango ya kumsaini kiungo wa kati wa Ajax Mholanzi mwenye miaka 21, Frenkie de Jong, anayewekewa thamani ya pauni milioni 72. (De Telegraaf - in Dutch)

Chanzo cha picha, Getty Images
Kiungo wa kati wa Uhispania Ander Herrera, 29, angetaka kubaki huko Old Trufford licha ya Barcelona kumzea mate. (ESPN)
Arsenal wanamwinda mchezaji wa Rennes raia wa Senegal mwenye miaka 20 Ismaila Sarr, ambaye pia anatazamwa na Inter Milan.(Mirror)

Chanzo cha picha, Getty Images
NewCastle watafanya mkutano na meneja Rafael Benitez kuhusu bajeti ya mwezi Januari kujaribu kumwezesha Mhispania huyo kusalia kwenye klabu baada ya mwisho wa msimu. (Telegraph)
Paris-St Germain wanammezea mate beki wa Juventus mwenye miaka 27 Mbrazil Alex Sandro, ambaye awali amehusishwa na Manchester United. (Le10 Sport - in French)

Chanzo cha picha, Getty Images
West Ham wako kwenye hatari ya kumpoteza mlinzi wa miaka 19 raia wa Ireland Declan Rice baada ya kukataa nyongeza ya mshahara wa pauni 12,000 kwa wiki. (Mail)












