Ligi ya Premier: Matokeo ya timu yakoje yakilinganishwa na ya msimu uliopita?

Chanzo cha picha, PA
Tottenham wameimarika msimu huu, Manchester United wamepiga hatua nyuma.
Ikiwa mechi sita tayari zimechezwa katika Ligi ya Primia, wachanganuzi wamefuatilia mechi za kwanza za kila timu na kugundua mambo mengi ya kusomwa.
Hofu kwa mashabiki wa Tottenham?
Ikiwa imeshindwa mara tatu mfululizo na matamshi yasiyo mazuri kutoka kwa meneja Mauricio Pochettino, hautakosolewa kama utasema kuwa Tottenham wameanza msimu vibaya.
Lakini ukiangalia zaidi utagundua kuwa wako na pointi tatu zaidi ya matokeo waliyoyapata msimu uliopita na pointi moja zaidi kuliko walivyocheza mechi sita msimu wa mwaka 2017-2018.
Manchester United - Iko vizuri lakini inatosha?

Chanzo cha picha, Getty Images
Tuachane na Newcastle ambao hawajashinda, Manchester United wameshuka kwa pointi nyingi kati ya timu za primia Ligi wakati inafikia kulinganisha matokeo ya msimu huu na ule wa mwaka 2017-2018.
Lakini hata hivyo wameithibiti meli wiki mbili zilizopita wakishinda ugenini mara mbili na nyingine barabarani kwa Ligi Kuu. Wako nambari saba katika Ligi na sio mbali saana na timu nne za kwanza.
Na unapoutazama uso wa meneja Jose Mourinho unaweza kuona tabasamu kidogo.
Kutokana na kuwa walimaliza pointi 19 nyuma wa mabingwa Manchester City, kushuka kwao kunaweza kulea wasi wasi.
Man City wako njiani kuzoa pointi sawa na za awali

Chanzo cha picha, Rex Features
Ilipokuwa inaelekea kupata ushindi msimu uliopita, Manchester City iliweka rekodi ya kuwa timu ya kwanza kenye Ligi ya Uingereza kufikisha pointi 100.
Yalikuwa ni kati ya mnafanikio makubwa zaidi ya Pep Guardiola' lakini ambayo Kevin de Bruyne aliseme yatakuwa vigumu kuyarudia.
Lakini tena City wako katika mkondo ya kurudia matokeo ya msimu uliopita.
Wana poiti 16 kutoka mechi sita matokeo ambayo yako sawa na ya msimu uliopita.
Arsenal wanaboreka?

Chanzo cha picha, Reuters
Mashabiki wengi wa Arsenal walisema sana wakitaka Arsene Wenger aondoke klabuni msimu uliopita, lakini kuondoka kwa Wenger kumeleta mabadiliko yoyote?
Lakini pia itakuwa mapema kumweka Emery kwenye uzani lakini takwimu zinaonyesha kuwa Arsenal imeboreka tangu Wenger aondoke.
Wako pointi mbili juu ukilinganisha na msimu uliopita.
Hatua kubwa za Palace na Liverpool

Chanzo cha picha, Getty Images
Chelsea na Watford wameanza vizuri na kuwa na kucheza vizuri dhdi ya timu ambazo ziliwapa wakati mgumu msimu uliopita.
Lakini ni kuboreka kwa pointi za Liverpool na Cystal Palace ulikuwa bora zaidi
Liverpool huenda wakawa na bahati ya kuwakabili City?
The full table
Za juu 10:
Za chini 10:












