Tetesi za Soka Ulaya Jumatano 19.09.2018: Sterling, Maguire, Berbatov, Southgate, Van Dijk, Poyet

Chanzo cha picha, Getty Images
Manchester City bado hawajaanza mazungumzo ya mkataba na wing'a mwenye miaka 23 Raheem Sterling, lakini sasa wanataka kufanya mazungumzo kuhusu kuongeza mkataba huo ambao utakamilika mwaka 2020. (Sun)
Waziri mkuu wa zamani wa Uingereza Tony Blair ametajwa k amamtu anayeweza kuwa mwenyekiti wa siku za usoni wa shirika linalosimamia Ligi ya Premia. Hilo lilifanyika wakati wa mazungumzo ya hivi karibuni ya klabu za England. (Daily Mail)
Brighton wanataka kumteua mkurugenzi wa kiufudi wa FA Dan Ashworth katika nafasi sawa na hiyo kwenye klabu yao.

Chanzo cha picha, Getty Images
Mlinzi wa Leicester raia wa England mwenye miaka 25 Harry Maguire amekana ripoti kuwa wachezaji hawakufurahishwa baada ya wao kusafiri kwa magari badala ya ndege kwa mechi huko Bournemputh. (Leicester Mercury)

Chanzo cha picha, Getty Images
Afisa mmoja wa West Brom aliondoka klabu hiyo baada ya uamuzi wa kukosa kununuliwa Virgine van Dijk kutoka Celtic licha ya kumpendekeza. (Scottish Sun)
Ajenti wa Mesut Ozil amewakashifu Manuel Neuer, Thomas Muller na Toni Kroos kufuatia matamshi waliyotoa baada ya uamuzi wa kiungo huyo wa kati wa Arsenal wa kuacha kuichezea Ujerumani mechi za kimataifa. (Guardian)

Chanzo cha picha, Getty Images
Meneja wa England Gareth Southgate alienda kutazama mechi ya nyumbani kati ya Derby na Blackburn Rovers badala ya mechi la ligi ya mabigwa kati ya Liverpool na Paris St-Germain siku ya Jumanne. (Times)
Meneja wa zamani wa Sunderland Gus Poyet anasema angetaka tena kusimania klabu ya England. (South China Morning Post)
Mwekezaji mmoja huko Uruguay ambaye ana hisa huko Sunderland anasema ana mpango kabambe wa miaka mitatu kusaidia kurejesha klabu hiyo katika Ligi ya Premio. (Northern Echo)

Chanzo cha picha, Getty Images
Jaji mmoja amewakosoa wachezaji wa Swansea Kristoffer Nordfeldt na Martin Olsson baada ya kushindwa kufika mahakamani kwa mashtaka ya kuendesha magari kwa kasi kwa sababu walikuwa wanacheza mechi ugenini huko Stoke. (Wales Online)
Mshambuliaji wa zamani wa Manchester United Dimitar Berbatov anaamini Juventus watacheza na Manchester City au Barcelona katika fainali ya msimu huu wa Ligi ya Mabingwa. (Mirror)
Mashabiki wa Milton Keynes Dons wamepewa fursa ya kununua tikiti kwa mechi kati ya Tottenham na Watford ambayo inachezewa uwanja wao kwa sababu Tottenham wana wakati mgumu wa kuwauzia mashabiki wao. (Daily Mail)
Bora kutoka Jumanne

Chanzo cha picha, Reuters
Mazungumzo ya mkataba mpya kati ya winga wa Manchester City Raheem Sterling na klabu yake yamegonga mwamba Sterling, 23, huku mkataba wa raia huyo wa England ukielekea ukingoni. (Guardian)
Crystal Palace imeulalamikia Uongozi wa Ligi Kuu Uingereza kwa kushindwa kumlinda staa wao Wilfred Zaha, 25, ambaye pia ni raia wa Ivory Coast anaokuwa uwanjani akicheza. (Telegraph)

Chanzo cha picha, Getty Images
Mkurungezi wa michezo wa Roma Monchi amesema walilazimika kumuuza mshambuliaji wa Misri Mohamed Salah, 26, kwenda Liverpool kwa sababu ya Sheria ya Uchezaji Haki Kifedha michezoni. (El Mundo)
Beki wa zamani wa Tottenham na timu ya taifa ya Uingereza Steven Caulker, 26, anaweza akajiunga na klabu kutoka Ukraine, Arsenal Kiev baada ya kuahidiwa dili na kocha wa klabu hiyo Fabrizio Ravanelli ambaye pia amewahi kuwa mshambuliaji wa zamani wa Middlesbrough. (Mirror)

Chanzo cha picha, Getty Images
Beki wa zamani wa Chelsea, John Terry, 37, hajaamua bado kama ataendelea kucheza baada ya kukataa kujiunga na klabu ya Urusi Spartak Moscow. Aston Villa imeonyesha nia ya kumsainisha tena beki huyo. (Birmingham Mail)
Rais wa FiFa Gianni Infantino amesema ana mashaka kuhusu kuufanya mchezo kati ya Barcelona dhidi ya Girona wa La Liga kuhamishiwa katika uwanja wa Hard Rock nchini Marekani. (ESPN)

Chanzo cha picha, Getty Images
Crystal Palace, Brighton and Watford zinamtolea macho kinda Adam Lovatt, 18, anayecheza katika klabu ya Bostik kwenye mashindano ya kanda ya kusini mashariki nchini Uingereza. (Team Talk)
Klabu ya Crystal Palace imemsajili Barry Simmonds kutoka Fulham kuungana na kocha wake wa zamani Roy Hodgson kama mapendekezo yake. Barry alikuwa mzuri sana katika kuwatafuta wachezaji nyota na ndiye aliyechangia kupatikana kwa Mousa Dembele, Chris Smalling na Zoltan Gera. (Mail)












