Tetesi za Soka Ulaya Jumatano 22.08.2018: Martial, Hazard, Mina, Ramsey, Alonso, Bolasie, Lookman

Anthony Martial

Chanzo cha picha, Getty Images

Meneja wa Manchester United Jose Mourinho amemuomba naibu mwenyekiti mtendaji wa klabu hiyo Ed Woodward kumuuza mshambuliaji wa Ufaransa anayechezea klabu hiyo Anthony Martial, 22. (Star)

Lakini Martial ameamua kwamba anataka kusalia Old Trafford na anataka kupigania nafasi yake katika kikosi cha Mourinho. (Sun)

Real Madrid wanatarajiwa kuwasilisha ofa yao ya mwisho ya kutaka kumnunua nyota wa Chelsea raia wa Ubelgiji Eden Hazard, 27, kabla ya dirisha kuu la kuhama wachezaji Ulaya kufungwa mwishoni mwa mwezi huu. (Mirror)

Barcelona wanaweza wakamnunua tena beki wa Colombia Yerry Mina kutoka Everton kwa euro 60m (£53.83m) baada ya kumuuza mchezaji huyo wa miaka 23 kwa Everton kwa euro 30.25m (£27.19m) siku ya mwisho ya kuhama wachezaji England, lakini hawawezi kutumia fursa hiyo kwenye kifungu cha mkataba wa kuhama kwake hadi mwaka 2020. (Marca)

Manchester City wataamua iwapo watamwita tena kipa wao mwenye miaka 19 Aro Muric aliye NAC Breda kwa mkopo baada ya uchunguzi zaidi wa kimatibabu kubaini kwamba kipa wao wa akiba Claudio Bravo aliumia kwenye kano za kifundo cha mguu akifanya mazoezi Alhamisi. (Telegraph)

Yerry Mina mchezaji wa kiungo cha kati upande wa nyuma wa Barcelona na Colombia

Hata hivyo klabu hiyo ya Uholanzi haitarajii mchezaji huyo anayechezea timu ya taifa ya wachezaji wa chini ya miaka 21 ya Montenegro achukuliwe tena na klabu hiyo ya Etihad. (Manchester Evening News)

West Ham wanamtafutia kiungo wa kati mwenye miaka 19 Reece Oxford klabu nyingine ya kumchukua kwa mkopo. Msimu uliopita, alikuwa an klabu ya Ujerumani ya Borussia Monchengladbach kwa mkopo. (Mail)

Aaron Ramsey

Chanzo cha picha, Getty Images

Arsenal wamekataa kukubali ombi la kiungo wa kati Aaron Ramsey la kutaka aongezewe ujira wake mara mbili lakini wana matumaini makubwa kwamba mchezaji huyo wa kimataifa wa Wales mwenye miaka 27 atatia saini mkataba mpya. (Evening Standard)

Mahasimu wa jadi Real Madrid na Atletico Madrid wote wanammezea mate beki wa kati wa Chelsea Marcos Alonso, 27, na wanataka kumchukua kabla ya soko kufungwa Ulaya mwezi huu. (AS)

Marcos Alonso

Chanzo cha picha, Julian Finney

Maelezo ya picha, Marcos Alonso

Winga wa Everton Yannick Bolasie, 29, anakaribia kwenda kwa mkopo Aston Villa baada ya kufanya mazungumzo na klabu hiyo. Mfaransa huyo pia amehusishwa na kuhamia Middlesbrough. (Birmingham Live)

Kwingineko, Everton wanataka £28m pamoja na malipo mwengine ya ziada kutoka kwa RB Leipzig ndipo wakubali kumuuza winga wa England mwenye miaka 20 Ademola Lookman. (Sky Sports)

Meneja wa Fulham Slavisa Jokanovic ameweka pembeni mazungumzo kuhusu mktaba mpya hadi baada ya Krismasi licha ya taarifa kwamba klabu hiyo imeahidi kumpa mkataba wa miaka mitatu. (Express)

Bora kutoka Jumanne

Paris St-Germain ina hamu ya kumsajili mchezaji wa Croatia Ivan Rakitic lakini Barcelona haiko tayari kumuuza mchezaji huyo mwenye miaka 30 ambaye kipengee cha kumuuza ni cha thamani ya Euro 125m (£112.2m). (Marca)

Mchezaji wa kiungo cha kati wa Real Madrid Luka Modric, mwenye umri wa miaka 32, amesema tuhuma kuwa amewasiliana na Inter Milan kuhusu uhamisho wake katika msimu wa joto kama "upuuzi mkubwa kihistoria". (Mirror)

Mchezaji wa kiungo cha kati wa Manchester City raia wa Ukraine Oleksandr Zinchenko, aliye na miaka 21, anatarajiwa kujiunga na timu ya Uhispania Real Betis kwa mkopo wa msimu mzima.(Sun)

Mchezaji wa kiungo cha kati wa Chelsea na England Ruben Loftus-Cheek, mwenye umri wa miaka 22, huenda akaelekea Uhispania kwa mkopo baada ya kutemwa katika kikosi cha Maurizio Sarri kitakachokabiliana na Arsenal mwishoni mwa juma. (Mirror)

Oleksandr Zinchenko
Maelezo ya picha, Oleksandr Zinchenko

Hatahivyo, Chelsea inamtaka Loftus-Cheek asalie na aipiganie nafasi yake licha ya mchezaji huyo kuudhika na hatua hiyo ya kutemwa katika kikosi.(Telegraph)

Middlesbrough inakaribia kufikia makubaliano ya wachezaji wawili wa Everton raia wa Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo Yannick Bolasie, aliye na miaka 29, na mchezaji wa kiungo cha kati wa Serbia Muhamed Besic, mwenye miaka 25. (Star)

Kuna uwezekano wa 50% kwa mlinzi wa Bayern Munich Jerome Boateng, aliyehusishwa na uhamisho kwenda Manchester United, huenda akaelekea Paris St-Germain katika siku chache zijazo. (Sky Sports)