Yanga yatoa mkosi Kombe la Shirikisho Afrika

kikosi cha watoto wa Jangwani, Yanga

Chanzo cha picha, yanga

Maelezo ya picha, kikosi cha watoto wa Jangwani, Yanga

Yanga yatoa mkosi Kombe la Shirikisho Afrika yashinda 2-1.

Mabingwa wa zamani wa soka nchini Tanzania Young Africans jana imefanikiwa kupata ushindi wa kwanza katika hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho Afrika baada ya kuifunga 2-1 USM Alger ya Algeria katika Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

Kwa ushindi huo young Africans imesonga hadi nafasi ya tatu katika Kundi D kwa nne baada ya ikiwa tayari imekwishafungwa michezo mitatu na kutoa sare mchezo mmoja, huku ikitaraji kucheza ugenini dhidi ya Rayon Sport nchini Rwanda wiki ijayo.

Mabao ya Young Africans yamefungwa na kiungo wake Deus Kaseke na na mchezaji raia wa Congo Eritier Makambo.

Michezo mingine Vita Club wameshinda bao 2-0 dhidi ya Raja Casablanca, CARA Barazaville imeifunga Williams ville mabao 3-1, Gor Mahia ya kenya imechapwa bao 1-0 na Rayon Sports ya Rwanda , Enyimba 1-0 na Al Hilal wamebamizwa mabao 2-0 na Berkane, Michuano hiyo itaendelea tena Agosti 29 kwa raundi ya sita.