Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Kombe la Dunia 2022: Fifa imetakiwa kufanya uchunguzi wa 'kipekee' dhidi ya Qatar
Shirikisho la soka duniani Fifa, limetakiwa kufanya 'uchunguzi wa kipekee' dhidi ya Qatar kwa madai kwamba ilipanga kampeini ya kisiri mwaka 2010 ili kuyazuia mataifa mengine kuwania nafasi ya kuwa mwenyeji wa michuano ya kimataifa mwaka 2022.
Mwenyekiti wa Mtandao, wa tamaduni , habari na michezo Damian Collins, amesema kuwa ikiwa madai hayo makali , yaliyochapishwa kwenye gazeti la Sunday Times yatakuwa ya kweli basi yatakuwa yamevunja sheria za Fifa.
''Swala hili litahitaji uchunguzi wa kipekee na Fifa inastahili kutoa hakikisho kwamba uchunguzi huo utafanyika, ''Collins alisema.
Akizungumza na BBC Radio 5, aliongeza: Iwapo nchi ya Qatar imevunja sheria , lazima wawekewe baadhi ya vikwazo.''
Katika taarifa, kamati kuu ya Qatar inayoshugulikia maswala ya kisheria imesema , inapinga madai yote yaliyowasilishwa na gazeti la Sunday Times.''
Gazeti hilo linadai kwamba liliona nyaraka zilizoonyesha kikosi cha Qatar kilichohusika kuajiri kampuni ya Marekani inaloshugulikia mahusiano ya umma na kikosi cha wakala wa zamani wa CIA ili kuwafuta mahasimu wao hasa Marekani na Australia.
Madai hayo yaliyochapishwa yalibuniwa kama propaganda ili kuonyesha kombe la dunia halitaungwa mkono na nchi za nyumbani. Waliopanga michuano ya Qatar walikana madai hayo.
Kampeini kama hiyo inayodaiwa na Sunday Times itakuwa imevunja sheria za Fifa za ushindani wa kugombea uenyeji wa mashindano ya kombe la dunia.
Qatar iliwashinda mahasimu wake kama Marekani, Australia, Korea Kusini na Japan kuwa nyenyeji halisi wa michuano ya kombe la dunia la mwaka 2022.
Sheria za FIFA zinasema wanaowania uenyeji wa Kombe la Dunia hawapaswi kutoa ombi lolote '' la maandishi, matamshi wala kauli ya aina yoyote ile , iwe ya moj kwa moja ama isiyo ya moja kwa moja kuhusu, kugombea uenyeji wa mashindano au kuwasiliana kwa namna yoyote ile na wajumbe wengine wa shirikisho hilo ".
Kamati iliyohusika kuiteuwa Qatar ilishutumiwa kwa madai ya rushwa, lakini madai hayo yalifutiliwa mbali baada ya uchunguzi wa Fifa uliofanyika kwa miaka miwili.