Kombe la Dunia Urusi: Mhubiri wa Nigeria ataka alipwe awasaidie Super Eagles kushinda Kombe la Dunia

Francis Uzoho na John Obi Mikel wakiimba wimbo wa taifa kabla ya mechi dhidi ya Iceland

Chanzo cha picha, AFP/Getty

Maelezo ya picha, Francis Uzoho na John Obi Mikel wakiimba wimbo wa taifa kabla ya mechi dhidi ya Iceland

Mhubiri mmoja nchini Argentina amewahimiza waumini wa kanisa lake kumlipa takriban $2,000 to atume kikosi cha "mashujaa wa maombi" kuwasaidia Super Eagles kupata ushindi Kombe la Dunia.

Nigeria walichapwa 2-0 na Croatia mechi yao ya kwanza Kombe la Dunia Urusi.

Waliwachapa Iceland 2-0 mechi yao ya pili Ijumaa.

Nabii wa kujitawaza Tommy Yisa Aika alisema mapema wiki hii kwamba Super eagles walishindwa mechi hiyo ya Croatia kwa sababu walikuwa wanaadhibiwa na Mungu kwa kumteua kocha mzungu, Gernot Rohr.

Shirika la habari la AFP linasema mhubiri huyo sasa anasema Nigeria wanaweza kujikomboa na kuwa taifa la kwanza la Afrika kushinda Kombe la Dunia iwapo mashabiki wa soka watampatia naira 750,000 ($2,092, euro 1,797).

"Ninachohitaji ni malipo kidogo tu, naira 750,000 ndipo nipate vifaa vya maombi vya kuwapa mashujaa wangu wa maombi kama kichochezo," alisema kwenye mahojiano ya runinga, kwa mujibu wa gazeti la Daily Post lililonukuliwa na AFP.

Aika amesema waumini wake maalum wako tayari kuanza kazi, ili "kile kilichoharibiwa kirekebishwe na Super Eagles wapate neema ya Mungu katika michuano hiyo."

Nigeria watakutana na Argentina mechi yao ya mwisho Kundi D>