Messi: Inaniuma sana kukosa penalti Kombe la Dunia

Chanzo cha picha, Getty Images
Lionel Messi amesema inamuumiza sana baada ya Penati yake dhidi ya Iceland kuokolewa wakati Argentina ilipokutana na Iceland.
Mkwaju wa penati wa Mchezaji huyu,30 na nyota wa Barcelona haukuleta madhara mbele ya mlinda mlango Hannes Halldorsson na kufanya timu hizi mbili kutoka sare ya 1-1
Messi alikuwa na matumaini makubwa ya kufanya vyema akitazama matokeo ya hasimu wake wa siku nyingi Cristiano Ronaldo hasa mabao matatu aliyoyafunga siku ya ijumaa dhidi ya Uhispania.
''Tumepata uchungu kwa kukosa alama tatu, kuanza kwa ushindi ni muhimu sana wakati wote, sasa tunapaswa kufikiria kuhusu Croatia''.
''tutajitahidi kuhakikisha hili linapita haraka''.
Messi alisema mbinu ya Iceland ilifanya mchezo ukawa mgumu ''hawakutaka kucheza'' lakini alikiri kuwa walijihami kwa ''kiasi kikubwa''

Chanzo cha picha, Getty Images
Kocha wa Argentina Jorge Sampaoli alimsifu Messi namna alivyocheza katika mchezo huu mgumu
''kutathimini kazi aliyoifanya Messi ni ngumu kwa sababu haikuwa mechi nzuri kwake''.
''Iceland walicheza kwa kujihami sana, wakifunga nafasi zote lakini tulifanya kila tuwezalo ili kushinda.Leo anajitoa kwa Argentina''.
''Mara zote huwa trunakuja kushinda, ndio maana kumekuwa na hali ya taharuki''.
Argentina itakabiliana na Croatia siku ya Alhamisi katika uwanja wa Nizhny Novgorod.

Chanzo cha picha, Getty Images
Mlinda mlango wa Iceland Hannes Halldorsson ameeleza jitihada alizofanya kuhakikisha anapangua mipira ya Messi.
Anasema alitazama penati nyingi za Messi na kutafuta mbinu ya kuzikabili.
''Ni ndoto iliyotimia kuishinda penati, hasa kwa kuwa imetusaidia kupata alama moja ambayo ni muhimu katika kufuzu hatua ya makundi''.












