Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Rais wa Ghana aamrisha kukamatwa mwenyekiti wa shirikisho la kandanda Ghana
Rais wa Ghana Akufo-Addo amemrisha kukamatwa mwenyekiti wa shirikisho la kandanda la Ghana Kwesi Nyantekyi, ambaye pia ni makamu wa rais wa kwanza wa shirikisho la kandanda barani Afrika CAF.
Hatua hiyo inafuatia makala moja ya uchunguzi ambayo inamhusisha Kwasi Nyantekyi na vitendo vya ulaghai.
Inadaiwa kuwa alitumia jina la rais wakati akipanga na kutekeleza ulaghai huo.
Uchunguzi huu uliofanywa na mwandishi wa habari maarufu Anas Aremeyaw Anas uliwasilishwa kwa rais.
Uchunguzi huu pia unadaiwa kufichua vitendo vya ufisadi miongoni mwa maafisa wengine wa shirikisho la kandanda nchini Ghana.
Video hiyo inapangiwa kuonyeswa kwa umma tarehe sita mwezi ujao.
Kwesi Nyantenkyi amekuwa rais wa shirikisho la kandanda nchini Ghana tangu mwaka 2005 na hajatamka lolote.