Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Mourinho: Lukaku amechoka lakini siwezi kumpumzisha
Mkufunzi wa manchester United Jose Mourinho amekiri kwamba mshambuliaji Romelu Lukaku amechoka lakini ng'o hawezi kumpumzisha.
Mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 24 amecheza kila dakika za mechi za Man United kufikia sasa kutokana na matatizo ya majeraha yanayomkumba mshambuliaji mwenza Zlatan Ibrahimovic.
Lukaku alianza msimu na mabao 11 katika mechi 10 lakini kufikia sasa amefunga magoli manne katika mechi 19.
''Kijana amechoka, ana nguvu nyingi sana lakini sasa zimekwisha na anahisi amechoka'', alisema Mourinho. ''Mchezaji huyu ni mzuri sana .Lakini siwezi kumpumzisha''.
Lukaku amehusishwa na makosa katika lango la timu yake katika wiki za hivi karibuni ambayo yamesababisha mabao kwa upande wa Manchester City na Burnley.
Lakini mkufunzi huyo wa United alikataa kumkosoa mchezaji huyo wa Ubelgiji akisema kuwa makosa hayo huenda yamesababishwa na uchovu.