Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Serena Williams kurudi uwanjani miezi minne baada ya kujifungua
Nyota wa tenisi Serena Williams atarejea uwanjani huko Abu Dhabi wiki ijayo miezi minne baada ya kujifungua.
Serena mwenye umri wa miaka 36, atakutana mchezaji nambari saba duniani Jelena Ostapenko tarehe 30 Disemba wakati wa mechi ya ubingwa wa dunia ya Mubadala
Alijifungua mtoto msichana Alexis Olympia Ohanian mwezi Septemba.
Bingwa huyo wa zamani duniani hajacheza tangu alisema Australian Open mwezi Januari.
Mkurugenzi wa Australian Open, Craig Tilley amesema kuwa Williama anatarajiwa kutetea taji lake katika mechi ya mwaka 2018 ambayo itaanza Januari 15.
Rafael Nadal, Milos Raonic na Stan Wawrinka wamejiondoa kutoka kwa Mubadala ambayo itachezwa kati ya 28-30 Disemba.