Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Wayne Rooney astaafu soka ya kimataifa
Mfungaji wa mabao mengi nchini Uingereza Wayne Rooney ameamua kustaafu katika soka ya kimataifa baada ya kukataa kushirikishwa katika kikosi cha timu ya taifa ya Uingereza kitakachomenyana katika mechi za kufuzu kombe la dunia.
Mshambuliaji huyo wa Everton aliombwa na meneja wa timu ya kandanda ya Uingereza kushiriki katika mechi dhidi ya Malta na Slovakia.
''Kila mara nilipochaguliwa ilikuwa fahari kubwa kwangu lakini naamini imefikia muda wa kujiondoa'' , alisema mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 31.
Mshambuliaji huyo wa zamani wa Manchester United alifunga mabao 53 katika mechi 119 za kimataifa.
Rooney ambaye hakushirikishwa na Southgate katika mechi dhidi ya Scotland na Ufaransa mnamo mwezi Juni alianza kuichezea Uingereza mwaka 2003 katika mechi ambapo Uingereza ilipoteza kwa Australia.