Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Wenger: Alexi Sanchez hajasema anataka kuondoka
Mshambuliaji wa Arsenal Alexis Sanchez hajamwambia mkufunzi wa Arsenal Arsene Wenger kwamba anataka kuondoka katika klabu hiyo , kulingana na mkufunzi huyo ambaye anatarajia mchezaji huyo wa Chile kukamilisha kandarasi yake.
Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 28 amesalia na mwaka mmoja katika kandarasi yake na Arsenal.
Hatahivyo imeripotiwa kwamba Sanchez angependa kujiunga na wapinzani wa Arsenal Manchester City .
Alipoulizwa iwapo Sanchez alimwambia kwamba angependelea kuondoka , rais huyo wa Ufaransa amesema kuwa hapana.
Wenger aliongezea: Wachezaji wana kandarasi na tunawatarajia kuheshimu kandarasi zao , hilo ndio tunalotaka.
Sanchez alijiunga na Arsenal kutoka Barcelona kwa kitita cha pauni milioni 35, 2014.