Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Emanuele Palladino:Muacheni Tiote apumzike
Wakala wa aliyekuwa mchezaji wa timu ya taifa ya soka ya Ivori Coast na klabu ya Beijing Enterprises nchini China, Cheick Tiote aliyefariki dunia wiki iliyopita Emanuele Palladino amewataka waandishi wa habari na wadau wa soka kuacha kujadili kifo cha mchezaji huyo.
Ametoa wito na kusisitiza kuwa huu ni wakati wa kuungana na familia ya mchezaji huyo katika maombolezo na kuacha kuendelea kuhoji kifo cha mchezaji huyo.
Tiote aliagwa siku ya Jumanne na mwili wake ukitarajiwa kurejeshwa nyumbani siku ya leo tayari kwa mazishi.
Cheick Tiote aliichezea nchi yake mara 52 na kuisaidia kunyakua taji la bara Afrika 2015.