Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Man Utd yasonga mbele Europa League
Manchester United wamesonga mbele na kuingia robo fainali ya michuano ya UEFA Europa League baada ya kuifunga Rostov 1-0 katika mchezo wa raundi ya pili uliochezwa Old Trafford. United wamesonga mbele kwa jumla ya magoli 2-1.
Juan mata ndio alifunga bao hilo pekee katika mchezo ambao United walionekana kupata tabu kuvunja ngome ya Rostov. Manchester United wangeweza kusonga mbele hata kwa matokeo ya 0-0 kwa kuwa tayari walikuwa na goli la ugenini.
Wasiwasi kwa mashabiki wa Manchester United pengine ni kuumia kwa kiungo wao Paul Pogba ambaye hakumaliza mchezo, kutokana na kuumia msuli wa paja. Nafasi yake ilichukuliwa na Marouane Fellaini.
United walitawala mpira lakini hawakufanikiwa kupata chochote hadi katika dakika ya 70 ambapo Mata alifunga bao hilo la ushindi.
Katika mechi nyingine mchezaji wa kimataifa wa Tanzania Mbwana Samatta aliisaidia timu yake kuingia robo fainali dhidi ya KAA Gent licha ya mchezo huo kumalizika kwa sare ya 1-1.
Samatta alipachika mabao mawili katika mchezo wa awali na hivyo KRC Genk kusonga mbele kwa jumla ya mabao 6-3.
Matokeo ya mechi nyingine, Besitkas imeingia robo fainali kwa jumla ya mabao 5-2 dhidi ya Olympiakos, Celta Vigo ilishinda 4-1 dhidi ya FK Krasnodar, Ajax imeishinda FC Copenhagen kwa 3-2, FC Schlake imesonga mbele kwa magoli ya ugenini dhidi ya Borussia Monchengladbach katika mechi mbili zilizomalizika kwa 3-3. Roma ya Italia iliweza kuingia robo fainali kwa kuichapa Lyon kwa jumla ya magoli 5-4 na Anderlecht kusonga mbele kwa 2-0 dhodo ya Apoel Nicosia.
Droo ya Klabu Bingwa Ulaya na Europa League itafanyika Ijumaa Machi 17.