Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Mesut Ozil donge nono-Arsenal
Klabu ya Arsenal imepanga kumtengea donge nono la mshahara Mesut Ozil ikiwa ni ofa nono ya mshahara unaofikia paundi 280,000 kwa wiki ili aweze kubakia katika klabu hiyo.
Kiungo huyo wa kimataifa wa Ujerumani bado hajaamua kuhusu mustakabali wake huku ikiwa imebaki miezi 15 katika mkataba wake wa sasa, na kumekuwa na wasiwasi uliobuka kuwa anaweza kuondoka msimu huu wa kiangazi.
Nyota huyo mwenye umri wa miaka 28 tayari ndio mchezaji anayelipwa zaidi Arsenal akikunja kitita cha paundi 140,000 kwa wiki ambazo zinaongezeka mpaka kufikia paundi 200,000 kwa wiki huku akiongeza na bakshishi.
Arsenal wako tayari kumuongeza zaidi lakini Ozil anaonekana kutokuwa tayari akifahamu kuwa anaweza kupata zaidi akienda kwingine.