Walinda amani waliowapiga risasi raia 2 na kuwauwa DRC ni Watanzania

Afisa wa ngazi za juu wa Umoja wa Mataifa ameiambia BBC kwamba walinda amani waliokamatwa siku ya Jumapili kwa kuwapiga risasi watu wawili hadi kufa katika mpaka kati ya Congo na Uganda walikuwa wanatoka Tanzania.

Moja kwa moja

  1. Habari za hivi punde, Walinda amani waliowapiga raia 2 risasi na kuwauwa DRC ni Watanzania

    Walinda amani wa Monusco

    Chanzo cha picha, AFP

    Maelezo ya picha, Walinda amani wa Monusco

    Afisa wa ngazi za juu wa Umoja wa Mataifa ameiambia BBC kwamba walinda amani waliokamatwa siku ya Jumapili kwa kuwapiga risasi watu wawili hadi kufa katika mpaka kati ya Congo na Uganda walikuwa wanatoka Tanzania.

    Haya ni kwa mujibu wa, Naibu Mwakilishi Maalum wa Katibu Mkuu wa MONUSCO, Khassim Diagne, aliyezungumza na BBC

    Umoja wa Mataifa umeshtumu vikali shambulio hilo ambapo watu 15 walijeruhiwa .

    Katika kipindi cha juma moja lililopita takriban watu 20 wamefariki katika maandamano ya ghasiadhidi ya walinda amani wa Umoja wa Mataifa wanaojulikana kama MONUSCO .

    Raia wengi wa DR Congo wamewashtumu walinda amani hao kwa kushindwa kuwalinda raia kutokana na mashambulizi yanayotekelezwa na waasi.

    Huku shambulizi hilo la siku ya Jumapili likitarajiwa kuliharibia sifa jeshi hilo la Umoja wa mataifa , wanahabari wanasema vurugu zimejitokeza kutokana na kile wakazi wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo wanaona kushindwa kwa kikosi cha kulinda amani cha Umoja wa Mataifa kusitisha mashambulizi ya makundi yenye silaha katika eneo hilo na kusababisha maandamano makali wiki iliyopita.

    Waandamanaji hao walishambulia kambi mbili za Umoja wa Mataifa huko Goma na Butembo, ambapo walinda amani wanne wa Umoja wa Mataifa waliuawa.

    Walinda amani wawili kati ya hao walikuwa raia wa Morocco na wengine wawili walikuwa Wahindi, wote walikuwa wamefanya kazi nchini DR Congo kwa Umoja wa Mataifa kwa muda wa chini ya miezi sita - huku mmoja wa waliouawa akiwa amekaa kwa miezi miwili na siku 22 pekee.

    Mwezi Juni vikosi vya kulinda amani vya Umoja wa Mataifa viliondoka katika jimbo tofauti la mashariki - Tanganyika - baada ya kile walichokieleza kuwa kuimarika kwa hali ya usalama.

  2. Na kufikia hapo ndio tunakamilisha matangazo yetu ya moja kwa moja kwa hii leo.

  3. Sudan yathibitisha kisa cha kwanza ugonjwa wa monkeypox

    Virusi hivi vimeenea duniani kote kwa kasi

    Chanzo cha picha, Getty Images

    Maelezo ya picha, Virusi hivi vimeenea duniani kote kwa kasi

    Sudan Jumapili ilithibitisha kisa chake cha kwanza cha ugonjwa wa monkeypox.

    Mgonjwa huyo ni mwanafunzi mwenye umri wa miaka 16 kutoka jimbo la Darfur Magharibi, wizara ya afya ya nchi hiyo ilisema.

    Shirika la Afya Duniani (WHO) wiki iliyopita lilitangaza mlipuko wa ugonjwa huo wa monkeypox kuwa ni dharura ya afya duniani.

    Kuna zaidi ya kesi 21,000 ulimwenguni kote hadi sasa, kulingana na Vituo vya Marekani vya Kudhibiti na Kuzuia Magonjwa.

    Soma zaidi:

  4. Zaidi ya watu 80 mahakamani kufuatia ubakaji wa genge Afrika Kusini

    Ramani ya Afrika Kusini
    Maelezo ya picha, Ramani ya Afrika Kusini

    Takriban watu 82 wanafikishwa katika mahakama ya Afrika Kusini Jumatatu kwa tuhuma za uchimbaji madini haramu, jaribio la mauaji, kupatikana na vilipuzi na kukiuka sheria za uhamiaji.

    Polisi wamesema washukiwa hao - ambao wengi wao ni wachimba migodi haramu - wanaweza pia kuhusishwa na ubakaji wa genge la wanawake wanane ambao walikuwa sehemu ya wafanyakazi wa kurekodi video ya muziki.

    Tukio hilo lilitokea siku ya Alhamisi huko Krugersdorp, magharibi mwa Johannesburg.

    Kundi hilo la wanawake 12 na wanaume 10 walisema walishambuliwa walipokuwa wakirekodi video ya muziki kwenye eneo la mabaki ya migodi.

    Wanawake wanane waliobakwa na genge walikuwa na umri wa kati ya miaka 19 na 37. Mmoja wa waathiriwa aliyezungumza na gazeti moja la eneo hilo alidai kuwa kundi la wachimba migodi haramu, wakiwa wamevalia blanketi na vinyago, waliwakaribia na kufyatua risasi hewani.

    Mwathiriwa alisema mmoja wa washukiwa wazee aliwaamuru wavulana wadogo kuwabaka wanawake kabla ya kuwaibia mali zao.

    Tukio hilo limeshangaza Afrika Kusini na kuibua wito mpya wa kuchukuliwa kwa madini ya wabakaji waliopatikana na hatia.

  5. UN 'sasa imedhamiria kuleta amani' baada ya vifo vya walinda amani DRC,

    Ramani

    Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa anayehusika na Operesheni za Amani amesema vifo vya hivi karibuni vya askari watano wa kulinda amani katika eneo la mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo vimeimarisha azma yao ya kuleta amani katika eneo hilo lisilo na utulivu.

    Kauli hiyo ilitolewa mapema leo katika kambi moja katika mji wa Goma wakati wa hafla ya kuwaenzi walinda amani wanne wa Umoja wa Mataifa waliouawa wakati wa maandamano ya kupinga Umoja wa Mataifa mwishoni mwa wiki iliyopita.

    Heshima pia ilitolewa kwa mlinda amani mwingine aliyefariki nchini humo akipambana na kundi la waasi la M23.

    Hafla hiyo inajiri siku moja baada ya askari wa kulinda amani wa Umoja wa Mataifa kuwafyatulia risasi wakazi wawili katika mji wa Kasindi nchini DR Congo unaopakana na Uganda.

    Vurugu zimejitokeza kutokana na kile wakazi wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo wanaona kushindwa kwa kikosi cha kulinda amani cha Umoja wa Mataifa kusitisha mashambulizi ya makundi yenye silaha katika eneo hilo na kusababisha maandamano makali wiki iliyopita.

    Waandamanaji hao walishambulia kambi mbili za Umoja wa Mataifa huko Goma na Butembo, ambapo walinda amani wanne wa Umoja wa Mataifa waliuawa.

    Walinda amani wawili kati ya hao walikuwa raia wa Morocco na wengine wawili walikuwa Wahindi, wote walikuwa wamefanya kazi nchini DR Congo kwa Umoja wa Mataifa kwa muda wa chini ya miezi sita - huku mmoja wa waliouawa akiwa amekaa kwa miezi miwili na siku 22 pekee.

    Mwezi Juni vikosi vya kulinda amani vya Umoja wa Mataifa viliondoka katika jimbo tofauti la mashariki - Tanganyika - baada ya kile walichokieleza kuwa kuimarika kwa hali ya usalama.

  6. Kenya haitafunga mtandao wa Facebook kabla ya uchaguzi – mawaziri

    Facebook

    Chanzo cha picha, Getty Images

    Maelezo ya picha, Facebook

    Serikali ya Kenya haitafunga mtandao wa kijamii wa Facebook licha ya vitisho vya shirika la uwiano wa kitaifa kuusitisha.

    Tume ya Kitaifa ya Utangamano na Uwiano (NCIC) wiki jana ilisema iliiandikia Meta, kampuni inayomiliki Facebook, ikitaka majibu kwa madai ya udhibiti dhaifu katika kudhibiti maudhui kwenye jukwaa lake kabla ya uchaguzi wa mwezi ujao.

    Ilitishia kusimamisha shughuli za kampuni hiyo iwapo haitazingatia ndani ya siku saba matakwa ya kudhibiti kuenea kwa matamshi ya chuki nchini.

    Lakini waziri wa ICT alitilia shaka mfumo wa kisheria ambao NCIC ilikuwa ikitumia kupendekeza kusimamishwa kwa Facebook.

    ‘’Wao (NCIC) walipaswa kushauriana kwa upana kwa sababu hawana uwezo wa kumfungia mtu yeyote. Hawatoi leseni kwa mtu yeyote,’’ Joe Mucheru alinukuliwa na shirika la Reuters akisema.

    Waziri wa Mambo ya Ndani Fred Matiangi, kivyake, alisema serikali ya Kenya haina mpango wa kubana mitandao ya kijamii na kujitenga na kauli ya NCIC.

    ‘’Sisi kama serikali, hatuna nia ya kukiuka haki hiyo.

    Wale ambao wametoa maoni yao juu ya kufungwa kwa mitandao ya kijamii wamefanya hivyo kama wao kibinafsi,” alisema.

    Ripoti ya mashirika ya utetezi ya Global Witness na Foxglove wiki iliyopita ilipata Facebook kuwa imeidhinisha matangazo yanayoendeleza matamshi ya chuki na uchochezi kabla ya uchaguzi.

    Facebook ilijibu kwa kusema kuwa imeongeza udhibiti kwenye majukwaa yao ili kurahisisha kutambua na kuondoa maudhui ambayo yanaweza kusababisha vurugu zinazohusiana na uchaguzi.

    Imekiri kuwa pamoja na juhudi hizo ‘’kutakuwa na mifano ya mambo tunayokosa au tunayatoa kimakosa, kwani mashine na watu hufanya makosa’’.

    ‘’Ndio maana tuna timu zinazofuatilia kwa karibu hali hiyo na kushughulikia makosa haya haraka iwezekanavyo,’’ msemaji wa Meta alisema.

    Soma zaidi:

  7. Beyoncé akosolewa kwa kutumia wimbo wa kukera kwenye albamu yake ya Renaissance

    Beyoncé akosolewa kwa kutumia wimbo wa kukera kwenye albamu yake ya Renaissance

    Chanzo cha picha, Getty Images

    Maelezo ya picha, Beyoncé akosolewa kwa kutumia wimbo wa kukera kwenye albamu yake ya Renaissance

    Beyoncé anakabiliwa na ukosoaji kwa kutumia maneno ya kukera katika baadhi ya nyimbo kwenye albamu yake mpya, Renaissance.

    Neno la dharau, ambalo mara nyingi hutumika kurejelea watu wenye ugonjwa wa kupooza kwa ubongo, limetumika mara mbili katika wimbo wa ‘Heated’, ambao umeandikwa na nyota wa Canada Drake.

    Hili linatokea wiki chache tu baada ya nyota wa pop wa Marekani Lizzo kuomba msamaha kwa kutumia neno moja katika wimbo wake GRRRLS.

    Baada ya tukio hilo, wimbo wa Beyoncé ‘’ni kama haujakubalika’’ anasema mtetezi wa ulemavu Hannah Diviney.

    ‘’Nimechoka na kufadhaika kuwa tunazungumzia hili tena mara tu baada ya kupata jibu la maana kutoka kwa Lizzo,’’ anaambia BBC.

    BBC imewasiliana na timu ya Beyoncé kutoa maoni yake.

    ‘’Inaudhi sana kwa sababu unavutia sana,’’ anasema mwandishi wa BBC wa walemavu Nikki Fox.

    ‘’Lakini ni neno la kutisha. Ni neno ambalo hatutawahi kulitumia nchini Uingereza - ingawa tunatambua wakati mwingine linatumika tofauti nchini Marekani.’’

    Fox anabainisha kuwa wimbo huo una waandishi 11, na ungeondolewa na watu kadhaa katika ngazi ya kurekodi kwenye label ya Beyoncé.

    ‘’Ukifikiria wimbo huo umepitia watu wangapi na hakuna hata mmoja wao aliyefikiria,’’ Subiri kidogo, na pia hakuna hata mtu mmoja ambaye hakufahamu wakati Lizzo alitumia neno moja. Inasikitisha sana.’’

    Albamu ya Beyoncé inatarajiwa kushika nafasi za juu licha ya utata huo.

    Soma zaidi:

  8. Mafuriko makubwa Uganda - idadi ya vifo yaongezeka

    Mvua kubwa yasababisha mafuriko Uganda (Picha kutoka maktaba)
    Maelezo ya picha, Mvua kubwa yasababisha mafuriko Uganda (Picha kutoka maktaba)

    Idadi ya vifo kutokana na mafuriko na maporomoko ya ardhi yaliyosababishwa na mvua kubwa mashariki mwa Uganda imeongezeka hadi 20, huduma za dharura zimethibitisha.

    Wenyeji, vikosi vya jeshi, na wahojiwa wengine wamekuwa wakifanya kazi tangu Jumapili kuwatafuta waliofariki na waliopotea katika hali ngumu.

    Video na picha zilizoshirikiwa kwenye mitandao ya kijamii zinaonyesha maji yanayochafuka, magari yakiwa yamezama, na maeneo mengi ya mashamba yaliyofunikwa na matope na vifusi.

    Mafuriko hayo yalitokana na mito kadhaa kuvunja kingo zake katika mikoa ya Bugisu na Sebei kufuatia mvua kubwa iliyonyesha mwishoni mwa juma.

    Kwa sababu hiyo, barabara nyingi hazipitiki.

    Mamia ya familia wamepoteza makazi na mashamba yao.

    Sehemu za mashariki mwa Uganda zinakabiliwa na majanga ya asili kama vile maporomoko ya ardhi na mafuriko karibu kila msimu wa mvua, ambayo husababisha watu kupoteza maisha na uharibifu mkubwa.

  9. Vita vya Ukraine: Meli ya kwanza ya nafaka yaondoka chini ya makubaliano ya Urusi

    Urusi imekuwa ikizuia bandari za Ukraine tangu Februari

    Chanzo cha picha, Getty Images

    Maelezo ya picha, Urusi imekuwa ikizuia bandari za Ukraine tangu Februari

    Meli ya kwanza iliyobeba nafaka imeondoka katika bandari ya Ukraine chini ya makubaliano ya kihistoria na Urusi.

    Maafisa wa Uturuki na Ukraine wanasema meli hiyo iliondoka katika bandari ya kusini ya Odesa mapema Jumatatu asubuhi saa za huko.

    Urusi imekuwa ikizuia bandari za Ukraine tangu Februari, lakini pande hizo mbili zilikubali mpango wa kurejesha usafirishaji.

    Inatarajiwa kuwa makubaliano hayo yatapunguza mzozo wa chakula duniani na kupunguza bei ya nafaka.

    Uturuki ilisema meli yenye bendera ya Sierra Leone, Razoni, itatia nanga katika bandari ya Tripoli nchini Lebanon, na kuongeza kuwa usafirishaji zaidi ulipangwa katika wiki zijazo.

    Kituo cha Uratibu wa Pamoja, kilichoanzishwa Istanbul chini ya mpango huo, kilisema meli hiyo ilikuwa imebeba tani 26,000 za mahindi na ilitarajiwa kuwasili katika maji ya Uturuki kwa ukaguzi siku ya Jumanne.

    Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres amekaribisha kuondoka kwa meli hiyo na kuipongeza Uturuki kwa jukumu lake la kutekeleza makubaliano hayo.

    ‘’Leo, Ukraine pamoja na washirika, inachukua hatua nyingine kuzuia njaa duniani,’’ Waziri wa Miundombinu wa Ukraine Alexander Kubrakov aliandika kwenye Facebook.

    Soma zaidi:

  10. Wizara ya Elimu Kenya yaagiza kufungwa kwa shule mara moja kabla ya uchaguzi

    TH

    Chanzo cha picha, Getty Images

    Wizara ya Elimu nchini Kenya imeagiza kufungwa kwa shule za msingi za umma kuanzia kesho Jumanne hadi Jumatano tarehe 10 mwezi huu na masomo yatenedlea Alhamisi tarehe 11 .

    Taarifa ya wizara hiyo iliyotiwa Saini na Waziri wa Elimu George Magoha imesema uamuzi huu umechukuliwa baada ya mashauriano ili kuruhusu maandalizi ya uchaguzi mkuu unaofanyika Jumanne tarehe 9.

    Iwapo uchaguzi wa marudio utafanyika endapo mshindi hatopatikana katika duru ya kwanza, tarehe hizo za kufunguliwa kwa shule huenda zinaweza kubadilika na hii inaweza kuathiri mitihani ya kitaifa iliyopangwa kufanyika baadaye mwaka huu.

    Shule kawaida hutumiwa kama vituo vya kupigia na kujumlisha kila mwaka wa uchaguzi.

    Taasisi nyingi ni shule za msingi, sekondari, vyuo vikuu na taasisi za mafunzo ya kiufundi.

    Kwa kawaida, uchaguzi wa mwaka huu ungefanyika wakati wanafunzi hawapo shuleni kwa likizo ndefu ya Agosti lakini ratiba hiyo ilivurugwa na janga la Corona lililosababisha shule kufungwa kwa muda mrefu.

  11. Ujasusi wa Uingereza: Huenda Urusi ikabadili mpango wa mashambulio katika Donbass

    • Kwa kipindi cha siku nne zilizopita, Urusi imeendeela kufanya mashambulio ya kimkakati katika eneo la Bakhmut kaskazini mwa Donetsk, lakini imesonga taratibu. Kama maafisa wa Ukraine walivyoripoti wiki iliyopita, Urusi ina uwezekano wa majeshi yake kusonga mbele zaidi kutoka eneo la kaskazini mwa Donbas kuelekea kusini mwa Ukraine
    • Urusi ina uwezekano wa kupunguza mpango wake wa kusonga mbele kuingia Donbass baada ya kushindwa kufanikiwa katia operesehani yake kama ilivyokuwa ikiufuata tangu Aprili. Kuna uwezekano mkubwa kwamba, Urusi imebaini kuwa mji wake wa Zaporozhye kama eneo lenye uwezekano wa kushambuliwa ambalo usalama wake unahitaji kuimarishwa
    Ruka X ujumbe
    Ruhusu maudhui? (Mitandao ya kijamii)

    Mkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue

    Onyo: BBC haihusiki na maudhui ya nje

    Mwisho wa X ujumbe

    Urusi na kraine: Mengi zaidi

    • MOJA KWA MOJA:Biden amuonya Putin: ''Madikteta watagharamika
    • YA MSINGI:Mzozo wa Ukraine: Kwanini Urusi inaivamia Ukraine na Putin anataka nini?
    • UFAFANUZI:Mzozo wa Ukraine: Swift ni nini na kwa nini kuipiga marufuku Urusi ni muhimu sana?
    • UCHAMBUZI:Mzozo wa Ukraine: Putin humsikiliza nani?
    • KWENYE RAMANI:Uvamizi wa Ukraine: Shambulio la Urusi kwenye ramani
    • ZELENSKY:Volodymyr Zelensky: Mfahamu rais wa Ukraine aliyeacha umaarufu wake wa TV na kuingia kwenye siasa
    • PUTIN:Vladimir Putin: Rais wa Urusi aliyeagiza shambulio Ukraine
  12. 'Ninasafiri duniani na paka watatu begani mwangu'

    Maelezo ya video, 'Ninasafiri duniani na paka watatu begani mwangu'

    Spongecake, Donut na Mocha ni paka wanaopenda matukio ambao wamegeuka kuwa wasafiri. Mkazi wa New York Dan Nguyen alianza kuchukua video ya uvumbuzi wao wa mijini- na kupakua video za utalii wao kwenye jukwaa la TikTok. Paka wa Dan waliweza kusafiri baada ya kipindi kirefu, umakini na mafunzo. Iwapo utataka kusafiri a mnyama wako wa nyumbani, tafadhali pata ushauri kutoka kwa daktari wa wanyama.

  13. Habari za hivi punde, Meli ya kwanza ya nafaka yaondoka Ukraine chini ya mkataba na Urusi

    Alexander Kubrakov

    Chanzo cha picha, Alexander Kubrakov

    Maafisa wa uturuki na Ukraine wamesema kuwa meli hiyo iliondoka katika bandari ya kusini ya Odesa Jumatatu majira ya asubuhi kwa saa za Ukraine.

    Urusi imekuwa ikizuia ikifunga bandari za Ukraine tangu mwezi Februari, lakini pande mbili zimefikia makubaliano ya kufufua tena usafirishaji wa nafaka kwa njia ya meli.

    Inatumainiwa kuwa mkataba huo utarahisisha mzozo wa chakula duniani na kupunguzwa kwa bei za nafaka ikiwa ni pamoja na ngano.

    Katika taarifa iliyotolewa kabla ya kuondoka kwa meli, Uturuki ilisema kuwa meli yenye bendera ya Sierra Leone- itatia nanga Lebanon, na kuongeza kuwa usafirishaji zaidi wa nafaka umepangwa kufanyika katika wiki zijazo.

    TOM BURRIDGE, BBC

    Chanzo cha picha, TOM BURRIDGE, BBC

    Maelezo ya picha, Bandari ya Odesa

    Kituo cha uratibu wa pamoja mjini Instanbul kiliwekwa chini ya mkataba na kimesema kuwa meli hiyo imebeba shehena ya tani 26,000 za mahindi ikitarajiwa kuwasili katika maji ya Uturuki kwa ajili ya ukaguzi tarehe 2 Agosti.

    "Leo Ukraine, na washirika, inachukua hatua nyingine kuzuia njaa duniani," Waziri wa miundo mbinu wa Ukrraine Alexander Kubrakov aliandika kwenye Facebook.

    Kufunguliwa kwa bandari kutaingiza walau dola bilioni moja bilioni 1 za mapato ya fedha za kigeni kwa uchumi na fursa kwa ajili ya sekta ya kilimo kwa ajili ya mpango wa mwaka ujao."

    Urusi na kraine: Mengi zaidi

    • MOJA KWA MOJA:Biden amuonya Putin: ''Madikteta watagharamika
    • YA MSINGI:Mzozo wa Ukraine: Kwanini Urusi inaivamia Ukraine na Putin anataka nini?
    • UFAFANUZI:Mzozo wa Ukraine: Swift ni nini na kwa nini kuipiga marufuku Urusi ni muhimu sana?
    • UCHAMBUZI:Mzozo wa Ukraine: Putin humsikiliza nani?
    • KWENYE RAMANI:Uvamizi wa Ukraine: Shambulio la Urusi kwenye ramani
    • ZELENSKY:Volodymyr Zelensky: Mfahamu rais wa Ukraine aliyeacha umaarufu wake wa TV na kuingia kwenye siasa
    • PUTIN:Vladimir Putin: Rais wa Urusi aliyeagiza shambulio Ukraine
  14. Mkuu wa Umoja wa Mataifa 'akasirishwa' na mauaji ya watu DR Congo

    th

    Chanzo cha picha, Reuters

    Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Antonio Guterres, anasema amekasirishwa baada ya watu wasiopungua wawili kuuawa wakati askari wa kulinda amani katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo walipofyatua risasi kwenye kivuko cha mpakani.

    Wengine kumi na watano walijeruhiwa.

    Katika taarifa, Bw Guterres alitoa wito wa kuwajibika baada ya kisa hicho, kilichotokea wakati wanajeshi hao walipokuwa wakivuka mpaka kutoka Uganda kuelekea mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.

    Mkuu wa ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa kulinda amani, Monusco, alisema watu wamekamatwa na uchunguzi umefunguliwa.

    Kanda za video zinaonekana kuonyesha mabishano yakifanyika kabla ya wanajeshi katika msafara wa Umoja wa Mataifa kuanza kufyatua risasi, huku watu wakikimbia kujificha.

    Wiki iliyopita kumekuwa na maandamano mabaya dhidi ya ujumbe wa Umoja wa Mataifa, ambao wengi wanahisi umeshindwa kuwalinda watu dhidi ya mashambulizi .

  15. Hezbollah yaapa kuchukua hatua dhidi ya Israel

    Hezbollah

    Chanzo cha picha, AFP

    Kikundi cha wapiganaji wa Hezbollah nchini Lebanon, kimetoa video ya vitisho kwa Israeli ambapo kilisema kuwa kitachukua hatua dhidi ya mitambo ya gesi na mafuta vya Israeli katika bahari ya Mediterranean.

    Video hiyo iliyotangazwa katika televisheni ya Al-Manar, ina picha nadra za silaha zinazotumiwa na Hezbullah, na kuonya kuwa maeneo ya Israeliyapo umbali mfupi tu kutoka kwenye maeeno yalipo makombora ya Hezbollah.

    Lebanon na Israeli zinalumbana juu ya mzozo wa maeneo yenye utajiri wa mafuta na gesi yaliyoko kwenye mwambao. Video hiyo ilitolewa saa kadhaa kabla ya afisa wa ngazi ya juu wa Marekani kuhudhuria mazungumzo ya upatanishi baina ya maafisa wa Lebanon mjini Beirut.

    Waziri wa mambo ya nje wa Lebanon Abdallah Bou Habib alisema Ijumaa kuwa ana matumaini makubwa kwamba mazungumzo yatakuwa ya mafanikio.

  16. Mwanamfalme Charles alikubali £1m kutoka kwa familia ya Osama Bin Laden– ripoti

    Prince Charles

    Chanzo cha picha, Reuters

    Mwanamfalme wa Wales alikubali malipo ya pauni milioni kutoka kwa familia Osama Bin Laden, limeripoti gazeti la Sunday Times.

    Mwanamfalme wa Uingereza Charles alikubali pesa kutoka kwa makaka wawili wa kambo wa Osama Bin Laden mwaka 2013, miaka miwili baada ya kiongozi wa al-Qaeda kuuawa, aliongeza.

    Wakfu wa Mwanamfalme wa Wales wa PWCF) ulipokea pesa hizo kama msaada.

    Clarence House ilisema kuwa ilikuwa imehakikishiwa na wakfu wa PWCF kwamba " ‘’ uangalifu wa kina " ulikuwa umefanyika, na uamuzi wa kukubali pesa ulichukuliwa wajumbe wa bodi ya utawala wa wakfu.

    "Jaribio lolote la kuelezea vinginevyo ni uongo," Makao makuu ya wakfu huo -Clarence House yaliieleza BBC.

    Clarence House pia ilisema kuwa inapinga na mambo kadhaa yaliyoelezwa katika Makala ya gazeti la Sunday Times.

    Bin Laden alikataliwa na familia yake mwaka 1994 na hapakuwa na ushahidi kwamba kaka zake wa kambo walikuwa na uhusiano na shughuili zake.

    Kulingana na taarifa hiyo , Mwanamfalme Charles alikubali pesa kutoka kwa Bakr Bin Laden, ambaye ni kiongozi wa familia tajiri ya Saudia, na kaka yake BakrShafiq, baada ya mkutano na Bakr katika Clarence House.

    Mrithi huyo wa Ufalme wa Uingereza alichukua pesa licha ya washauri wake katikaClarence House na PWCF kupinga hilo, ripoti ya Sunday Times, inasema kinukuu vyanzo mbali mbali.

    Hatahivyo, Sir Ian Cheshire, mwenyekiti wa PWCF, aliliambia gazeti hilo kwamba msaada huo wa mwaka 2013 ulikubaliwa "kuangaliwa kwa makini " na wajumbe watano wa bodi ya utawala wake huo.

  17. DRC yaanzisha uchunguzi baada ya wanajeshi wa Umoja wa Mataifa kukiri kuwaua raia 2

    TH

    Chanzo cha picha, Reuters

    Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo imeanzisha uchunguzi baada ya tume ya Umoja wa Mataifa ya kulinda amani nchini humo, MONUSCO, kukiri kwamba wanajeshi wake waliwaua watu wawili katika ufyatulianaji wa risasi katika mji wa Beni kwenye mpaka na Uganda, mamlaka za eneo zilisema Jumapili.

    "Watu wawili walikufa na 15 walijeruhiwa kufuatia risasi zilizopigwa na askari wa kulinda amani kutoka kwa kikosi cha MONUSCO kutoka Uganda," Patrick Muyaya Katembwe, waziri wa DRC anayehusika na mawasiliano na vyombo vya habari na msemaji wa serikali alisema .

    Alitangaza kufunguliwa kwa uchunguzi wa pamoja na MONUSCO ili kubaini kuhusika na tukio hilo na kujua sababu ya tukio hilo na kuweka vikwazo vikali dhidi ya walinda amani waliohusika.

    Katembwe alisema tayari wamekamatwa, akisisitiza kwamba hawawezi tena kuwa sehemu ya kikosi cha ujumbe wa Umoja wa Mataifa wakisubiri matokeo ya mpango wa kuiondoa MONUSCO kutoka DRC.

    Katika taarifa yake, Bintou Keita, mkuu wa misheni hiyo, alisema amepokea kwa mshtuko mkubwa habari za tukio hilo la kaburi lililotokea Jumapili asubuhi.