Uchaguzi Kenya 2022: Kwa nini vijana wanajipata nje ya uongozi wa kisiasa nchini Kenya?
Nchini Kenya Wabunge wengi wanaohitimisha hatamu zao kama wawakilishi katika bunge la taifa na lile la seneti wana umri uliozidi miaka 35, hivyo hawaonekani kuwa vijana. Licha ya kwamba vijana wengi wanajaribu kuingia katika siasa, gharama ya juu ya kufanya kampeni imefanya vyeo vya kisiasa kuwa vya wachache tu walio na pesa nyingi na wenye ushawishi.
Hata hivyo baadhi ya vijana wameamua kuwania nyadhifa mbali mbali kama wagombeaji huru katika uchaguzi wa Agosti 9. Mwanahabari wa BBC Charles Gitonga amekutana na baadhi yao.
