Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Mpina achukua rasmi fomu ya urais kwa tiketi ya chama cha ACT Wazalendo
ACT Wazalendo ilimuidhinisha rasmi Mpina kuwa mmoja wa wagombea wa Urais atakayechuana na Rais Samia Suluhu Hassan wa CCM kwenye uchaguzi Mkuu.
Muhtasari
- Mpina achukua rasmi fomu ya urais kwa tiketi ya chama cha ACT Wazalendo
- Uhalifu wa kivita huenda ulitekelezwa katika ghasia za pwani ya Syria, UN inasema
- Mali yatangaza kukamatwa kwa wanajeshi kwa madai ya kupanga kusababisha "vurugu"
- Zaidi ya watu 300 waugua Indonesia baada ya kula chakula cha mchana shuleni
- Mazungumzo ya mkataba wa Plastiki yakwama
- Malumbano ya kukosa heshima bado yanaendelea juu ya mwili wa rais wa zamani wa Zambia
- Mtu anayeshukiwa kuwa jasusi wa Ufaransa akamatwa kwa madai ya njama ya mapinduzi ya Mali
- Mzozo wa kidiplomasia waibuka kuhusu matamshi ya kamanda wa jeshi la Afrika Kusini nchini Iran
- Trump asema Putin 'hatanisumbua' huku wawili hao wakijiandaa kwa mazungumzo ya Ukraine Alaska
- Akili Mnemba (AI) yatengeneza dawa za kuua bakteria (Antibiotics) za kisonono na vimelea sugu
- Mpango wa mwisho wa mpango wa "udhibiti wa kijeshi" wa Gaza wakaribia
- Muda muhimu Alaska: Trump kukutana na Putin huku Ukraine ikitengwa
Moja kwa moja
Na Dinah gahamanyi & Asha Juma
Mpina achukua rasmi fomu ya urais kwa tiketi ya chama cha ACT Wazalendo
Mwenyekiti wa Tume ya uchaguzi Tanzania, Mheshimiwa Jaji wa Mahakama ya Rufaa Jacobs Mwambegele amemkakabidhi Mwanachama wa ACT Wazalendo, Ndugu Luhaga Mpina fomu za kuomba kuteuliwa kuwa Mgombea wa Kiti cha Rais wa Tanzania kwa tiketi ya chama cha ACT Wazalendo akiwa na mgombea mwenza, Fatma Ferej katika ofisi za tume jijini Dodoma.
ACT Wazalendo ilimuidhinisha rasmi Mpina kuwa mmoja wa wagombea wa Urais atakayechuana na Rais Samia Suluhu Hassan wa CCM kwenye uchaguzi Mkuu mwaka wa 2025.
Baada ya kuchukua fomu rasmi Mpina alihutubia wanahabari.
‘’Tunaondoka hapa, tunakwenda moja kwa moja kuanza zoezi la kutafuta wadhamini… Tunahakikishia Watanzania kwamba sisi kama wagombea wa chama hiki cha ACT Wazalendo, tutazingatia masharti ya Tume, tunaenda kusoma sheria zote za Tume, lipi tunaruhusiwa kufanya, lipi haturusiwi kufanya…,’’ Mpina alisema.
Mpina alitoa hakikisho kuwa wamekagua nyaraka zote kama inavyohitajika na tume pamoja na barua na kuwa ziko sawa.
‘’Tunaomba Watanzania wajitokeze kwa wingi ili tupate sifa zote za kisheria kwa ajili ya kupata uteuzi wakuwa wagombea wa wanafasi ya urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,’’ Mpina aliwarai Watanzania.
Katika Mkutano Mkuu Taifa wa chama hicho, Mpina alichaguliwa kwa kishindo kwa kupata kura 559 sawa na asilimia 92.3 ya kura zote 610 zilizopigwa.
Soma zaidi:
Uhalifu wa kivita huenda ulitekelezwa katika ghasia za pwani ya Syria, UN inasema
Wanachama wa vikosi vya serikali ya mpito ya Syria pamoja na wapiganaji wanaohusishwa na utawala wa zamani huenda walifanya uhalifu wa kivita wakati wa ghasia za kidini mnamo mwezi Machi ambazo ziliua takriban watu 1,400, hasa raia, ripoti ya Umoja wa Mataifa inasema.
Tume ya Uchunguzi ya Umoja wa Mataifa ya Syria ilisema haikupata ushahidi wowote kwamba mamlaka huko Damascus ziliamuru mashambulizi hayo.
Vurugu za ufukweni, kitovu cha madhehebu ya Kiislamu ya Alawite, zilifichua mgawanyiko uliokuwepo baada ya waasi wanaoongozwa na Waislamu kumwondoa madarakani aliyekuwa Rais Bashar al-Assad mnamo mwezi Desemba.
Ghasia zilizuka huku vikosi vya usalama vikivamiwa na makundi yanayotii utawala wa zamani, na kusababisha mapigano kati ya vikosi vya serikali, wengi wao wakiwa Waislamu wa madhehebu ya Sunni na wafuasi wa Assad, wengi wao wakiwa Alawite.
Soma zaidi:
Trump kukutana na Putin huko Alaska – Msemaji wa Kremlin
Msemaji wa Kremlin Dmitry Peskov amemwambia mwandishi wa Televisheni ya serikali Pavel Zarubin kwamba Trump atakutana na Putin kwenye ngazi za ndege ya rais wa Urusi atakapowasili Alaska.
Peskov alikuwa akizungumza na Zarubin akiwa ndani ya ndege, mjini Magadan.
Alisema ndege ya Putin itaondoka Magadan kama ilivyopangwa na itawasili Alaska saa 11:00 saa za eneo (20:00 BST).
Kando na vita vya Ukraine, Putin na Trump watajadili masuala mengine mengi yakiwemo "yanayokera" katika uhusiano wa Marekani na Urusi na miradi inayoweza kutekelezwa ya kiuchumi, msemaji huyo aliongeza.
Soma zaidi:
Mali yatangaza kukamatwa kwa wanajeshi kwa madai ya kupanga kusababisha "vurugu"
Mamlaka nchini Mali inasema wamekamata kikundi cha maafisa wa jeshi na raia wanaoshukiwa kupanga njama ya kusababisha "vurugu" nchini humo.
Kati ya wale waliowekwa kizuizini ni majenerali wawili wakuu wa Jeshi na raia wa Ufaransa anayeshukiwa kufanya kazi na ujasusi wa Ufaransa.
Tangazo hilo linafuata uvumi wa hivi karibuni juu ya jaribio la mapinduzi lililoshindwa katika nchi hiyo ya Sahel.
Waziri wa Utawala wa Mali alithibitisha kukamatwa kwa watu hao siku ya Alhamisi jioni.
Mmoja wa waliokamatwa ni Jenerali Abass Dembele, ambaye aliondolewa hivi karibuni kama gavana wa mkoa wa Mopti baada ya kutaka uchunguzi juu ya mauaji ya raia na wanajeshi wa Mali.
Pia aliyekamatwa ni Jenerali Nema Sagara - afisa mashuhuri wa kike, anayejulikana kwa jukumu lake katika kupigana na vikundi vya waasi mnamo 2012.
Raia wa Ufaransa aliyekamatwa anadaiwa alikuwa akifanya kazi kwa niaba ya huduma za ujasusi za Ufaransa - madai yanayoweza kuongeza mvutano kati ya Bamako na Paris.
Kukamatwa kwa watu hao kunaonekana kuonyesha kuongezeka kwa hali ya wasiwasi ndani ya jeshi la Mali.
Na hatua hii inashuhudiwa baada ya Rais wa Mpito Assimi Goïta kuongeza utawala wake kwa miaka mitano licha ya ahadi za mapema za kurudisha nchi hiyo kwa utawala wa raia ifikapo Machi 2024.
Soma zaidi:
Zaidi ya watu 300 waugua Indonesia baada ya kula chakula cha mchana shuleni
Takriban watu 365 wamakuwa wagonjwa katika mji mmoja nchini Indonesia baada ya kula chakula cha mchana shuleni, idadi kubwa zaidi ya watu waliokula chakula chenye sumu kuwahi kuathiri mpango wa chakula cha bure wa Rais Prabowo Subianto kufikia sasa.
Chakula hicho kimesitishwa kwa muda huko Sragen, katikati mwa Java, huku chakula hicho kikichukuliwa kwa ajili ya vipimo, viongozi wa eneo hilo walisema.
Mpango huo - ambao unagharimu wastani wa $28bn (£21bn) – ni ahadi ya kampeni ya rais ya kukabiliana na ukuaji na maendeleo ya watoto kutokana na lishe duni nchini humo.
Lakini mpango huo umekuwa ukikabiliana na msururu wa matukio ya chakula kutiwa sumu , pamoja na ukosoaji kwamba gharama yake ya juu imekuwa kikwazo kwa fedha za serikali - na wizara kadhaa zimelazimika kupunguza bajeti zao.
Soma zaidi:
Mazungumzo ya mkataba wa Plastiki yakwama
Mazungumzo ya kimataifa ya kutafuta mkataba wa kihistoria wa kukomesha uchafuzi unaosababishwa na plastiki yamekwama.
Mazungumzo hayo ya Umoja wa Mataifa ya duru ya sita katika kipindi cha chini ya miaka mitatu, yalipaswa kukamilika siku ya Alhamisi lakini nchi ziliendelea kujadiliana hadi usiku wa manane kwa matumaini ya kupata suluhu.
Bado kuna mgawanyiko kati ya kundi la zaidi ya mataifa 100 linalotaka kuzuiliwa kwa uzalishaji wa plastiki huku mataifa yenye mafuta yakishinikiza kuzingatia uchakataji upya.
Wakizungumza mapema, wajumbe wa Cuba walisema kuwa nchi "zimekosa fursa ya kihistoria lakini inabidi tuendelee".
Mazungumzo hayo yalianzishwa mnamo mwaka 2022 kama hatua iliyochukuliwa kutokana na ushahidi unaoongezeka wa kisayansi wa hatari za uchafuzi wa plastiki kwa afya ya binadamu na mazingira.
Licha ya manufaa ya plastiki kwa karibu kila sekta, wanasayansi wanawasiwasi sana juu ya kemikali zinazoweza kuwa na sumu, ambazo zinaweza kujitokeza kutokana na plastiki inapovunjika na kuwa vipande vidogo vidogo.
Plastiki ndogo ndogo zimegunduliwa katika udongo, mito, hewa na hata kwenye viungo katika mwili wa binadamu.
Nchi zilikuwa na makataa ya awali ya kupata mkataba juu ya suala hili kufikia mwishoni mwa Desemba mwaka jana, lakini zilishindwa kufikia makubaliano.
Graham Forbes, mkuu wa wajumbe wa shirika la Greenpeace kwenye mazungumzo ya Mkataba wa Kimataifa wa Plastiki, alisema: "Kutoweza kufikia makubaliano huko Geneva lazima iwe mwamko mpya ulimwenguni: kukomesha uchafuzi wa plastiki kunamaanisha kukabili masilahi ya mafuta ya kisukuku moja kwa moja.
Mwenyekiti alitangaza kuwa mazungumzo hayo yataanza tena siku nyingine.
Pia unaweza kusoma:
Malumbano ya kukosa heshima bado yanaendelea juu ya mwili wa rais wa zamani wa Zambia
"Unarudi nyumbani!" - msemo unaohusishwa na mashabiki wa soka wa Uingereza - sasa umepata umaarufu miongoni mwa baadhi ya Wazambia katika vita ya nini cha kufanya na mwili wa Rais wa zamani Edgar Lungu.
Lungu mwenye umri wa miaka 68 alifariki miezi miwili iliyopita nchini Afrika Kusini ambako alikuwa akitibiwa.
Katika tukio la hivi karibuni, mahakama ya Pretoria ilitoa uamuzi unaopendelea serikali ya Zambia, ikisema kwamba kwa maslahi ya umma, mwili wa Lungu unaweza kurejeshwa na kufanyiwa mazishi ya serikali, jambo ambalo ni kinyume na matakwa ya familia.
Uamuzi huo uliibua shangwe miongoni mwa baadhi ya wafuasi wa chama tawala, ambao walichapisha ujumbe wao kwenye mtandao wa Facebook kwa maneno: "Unarudi nyumbani," kana kwamba Zambia ilikuwa imeshinda kombe.
Jibu lisilo na heshima, pengine, lakini limejitokeza kuashiria jinsi suala hili limeleta mgawanyiko.
Kwa wengine ambao wamechoshwa na mzozo huo huzuni iliyosababishwa na kifo cha Lungu imefifia na kuwa hisia ya uchovu.
Na licha ya matatizo mengi zaidi ya kiuchumi, mijadala ya umma inaendelea kutawaliwa juu ya kifo cha rais huyo wa zamani, ambaye aliongoza nchi hiyo kwa miaka sita kuanzia 2015.
Kiini cha mzozo wa ni wapi atakapozikwa umesababishwa na tofauti iliyokuwepo kati ya Lungu na mrithi wake - ambaye alimshinda katika uchaguzi wa 2021 - Hakainde Hichilema.
Jaji wa Afrika Kusini alipotoa uamuzi wake wiki iliyopita, hasira ya dada mkubwa wa Lungu ilijitokeza wazi.
Bertha Lungu alipandwa na hasira, akilia bila kujizuia huku akimrushia maneno yasiyopendeza Mwanasheria Mkuu wa Zambia, Mulilo Kabesha, ambaye pia alikuwepo mahakamani.
"Kabesha, Lungu si mtoto wa baba yako... si mtoto wa Hakainde... Hii ni uchungu sana. Sitaki kwenda Zambia," alilia huku watu akiwemo mpwa wake, Tasila Lungu wakihangaika kumliwaza na kumziba mdomo.
Mwili bado haujarejeshwa Zambia kwa sababu familia ya Lungu inakata rufaa dhidi ya uamuzi wa jaji wa Afrika Kusini - kesi ambayo inatazamiwa kusikilizwa Jumatatu.
Soma zaidi:
Mtu anayeshukiwa kuwa jasusi wa Ufaransa akamatwa kwa madai ya njama ya mapinduzi ya Mali
Watawala wa kijeshi wa Mali wanasema wamemkamata raia mmoja wa Ufaransa kwa tuhuma za kufanya ujasusi wa nchi yake katika jaribio la kuliyumbisha taifa hilo la Afrika.
Katika taarifa iliyosomwa kwenye televisheni ya taifa siku ya Alhamisi, utawala wa kijeshi wa Mali wa junta ulidai kwamba Yann Vezilier alikuwa akifanya kazi "kwa niaba ya idara ya ujasusi ya Ufaransa". Bw Vezilier bado hajatoa maoni yake kuhusu tuhuma hiyo.
Picha yake pia ilitangazwa, pamoja na ya majenerali kadhaa wa jeshi waliokamatwa hivi karibuni kwa madai ya kupanga kuipindua serikali ya kijeshi .
"Njama hiyo imezimwa na kukamatwa kwa wale waliohusika," Waziri wa Usalama wa Mali Jenerali Daoud Aly Mohammedine alisema katika hotuba ya televisheni.
Ufaransa, ambayo ni mtawala wa zamani wa kikoloni wa Mali, pia bado haijazungumzia kukamatwa kwa mtu huyo na madai ya kuvuruga utulivu.
Taifa hilo la Afrika Magharibi limekumbwa na mzozo wa kiusalama uliochochewa na waasi wa Kiislamu tangu mwaka 2012 - moja ya sababu zilizotolewa za kunyakua jeshi lakini mashambulizi ya makundi ya kijihadi yameendelea na hata kuongezeka.
Kufuatia siku za uvumi kuhusu madai ya njama ya mapinduzi, Jenerali Mohammedine alithibitisha kwamba "wahusika wengine wa vikosi vya usalama vya Mali" wamezuiliwa kwa kutaka "kuvuruga taasisi za jamhuri".
"Askari hawa na raia" walisemekana kupata "msaada wa mataifa ya kigeni", waziri alisema.
Pia unaweza kusoma:
Mzozo wa kidiplomasia waibuka kuhusu matamshi ya kamanda wa jeshi la Afrika Kusini nchini Iran
Jenerali Rozani Mavuanya, kamanda wa jeshi la Afrika Kusini, anakabiliwa na ukosoaji mkubwa nchini mwake kutokana na kauli zake wakati wa mkutano na maafisa kadhaa wa ngazi za juu wa jeshi la Iran mjini Tehran, kwa kushindwa kutoegemea upande wowote na ukiukaji wa sheria za kijeshi.
Kwa mujibu wa mashirika ya habari ya Iran, katika moja ya mikutano hiyo, aligusia uzoefu wa uchungu wa wakati wa utawala wa ubaguzi nchini Afrika Kusini, akichukulia "uchokozi na uhali wa utawala wa Kizayuni kuwa ni utawala mpya wa kibaguzi," na akasema, "Tunasimama pamoja nanyi katika kuwatetea wanyonge wa dunia."
Aidha , kwa mujibu wa ripoti za vyombo vya habari vya Iran, kamanda wa jeshi la Afrika Kusini, katika kikao na maafisa wakuu wa Iran, alitoa wito wa "ushirikiano wa kina" na Iran, hasa katika masuala ya ulinzi.
Kumekuwa na mazungumzo ya "majaribio kumshitaki katika mahakama ya kijeshi" Jenerali Rozani Mavuanya mara moja kutokana na kauli zake.
Msemaji wa Wizara ya Ulinzi ya Afrika Kusini, Chris Hattingh, alisema chama cha Democratic Alliance Party kiliyataja matamshi ya mkuu wa jeshi la nchi hiyo kuwa "kuonyesha uzembe" na kusema kuwa "amevuka mijadala ya kijeshi na kuingia katika ulingo wa sera za kigeni."
Bw. Hattingh pia alitoa wito wa "mashitaka ya kijeshi" mara moja dhidi ya Jenerali Mafuanya kwa uvunjaji wa sera ya kutoegemea upande wowote na ukiukaji wa sheria za kijeshi.
Trump asema Putin 'hatanisumbua' huku wawili hao wakijiandaa kwa mazungumzo ya Ukraine Alaska
Jana mchana Donald Trump alizungumza na vyombo vya habari katika Ikulu ya White House kuhusu mkutano wake na Putin na hiki ndicho alichokisema:
- Trump alisema kwamba, kama asingekuwa rais, Putin "afadhali zaidi... angeichukua Ukraine yote", na kuongeza kuwa: "Lakini mimi ni rais, na hatanisumbua."
- Trump alisema atajua katika dakika chache za kwanza kama yeye na Putin "watakuwa na mkutano mzuri", akisema kwamba vinginevyo "utaisha haraka sana"
- Lengo lake la mazungumzo hayo, alisema, ni "kuweka meza" kwa mkutano mwingine na kiongozi wa Urusi na Rais wa Ukraine Zelensky.
- Akiongea na Fox News Radio mapema jana, Trump alisema ikiwa ni "mkutano mzuri" atampigia simu Zelensky kupanga mwingine, lakini akaongeza kuna uwezekano wa "25% mkutano huu hautakuwa na mafanikio"
- Na rais huyo wa Marekani alisema itabidi kuwe na kile alichokitaja kama "kutoa na kuchukua " kwenye mipaka kati ya Urusi na Ukraine
Soma zaidi:
Akili Mnemba (AI) yatengeneza dawa za kuua bakteria (Antibiotics) za kisonono na vimelea sugu
Akili Mne imevumbua dawa za aina mbili za maambukizi (Antibiotics) mpya zinavyoweza kuwaua vimelea vya kisonono sugu na MRSA, watafiti wamefichua.
Dawa hizo ziliundwa Akili Mnemba kwa chembembe chembe ndogo sana na kuua vimelea hao wa maambukizi sugu katika majaribio ya maabara yaliyohusisha Wanyama.
Michanganyiko miwili bado inahitaji miaka ya uboreshaji na majaribio ya kimatibabu kabla ya kutolewa na madaktari kwa wagonjwa
Lakini timu ya Taasisi ya Teknolojia ya Massachusetts (MIT) uvumbuzi huu inasema Akili Mnemba inaweza kuanza "enzi mpya ya dhahabu" katika ugunduzi wa dawa za kuua bakteria.
Dawa hizo huua bakteria, lakini maambukizi sugu sasa yanasababisha vifo vya zaidi ya milioni moja kwa mwaka.
Kutumia dawa za bakteria kupita kiasi kumewasaidia bakteria kubadilika ili kuepuka athari za dawa, na kumekuwa na uhaba wa dawa zinazoua bakteria mpya kwa miongo kadhaa.
Unaweza pia kusoma:
Uidhinishaji wa mwisho wa mpango wa "udhibiti wa kijeshi" wa Gaza unakaribia
Wanajeshi wa Israel wakiendesha shughuli zao karibu na vifaru kwenye eneo la mkutano karibu na mpaka na Ukanda wa Gaza, Agosti 13, 2025
Waziri wa Ulinzi wa Israel Yisrael Katz alikutana Alhamisi na Mkuu wa Majeshi wa IDF Eyal Zamir na baadhi ya maafisa wakuu wa Utumishi ili kukagua "mpango wa jeshi wa kuudhibiti kijeshi" mji wa Gaza.
Ni vyema kutambua kwamba mpango wa mwisho utawasilishwa Jumapili ijayo kwa idhini ya mwisho.
Televisheni ya Channel 12 ilimnukuu Zamir akisema, "Haja ya mshikamano kati ya ngazi ni muhimu ili kuhakikisha uamuzi na nguvu ya serikali."
Pia alisema, "Uhusiano kati ya ngazi ya kisiasa na kijeshi ni mhimili na msingi wa usalama wa taifa, hasa wakati wa vita."
Mkutano kati ya Zamir na Katz ni sehemu ya mkutano wao wa kawaida wa kila wiki. Zamir anatarajiwa kuidhinisha mipango ya kuchukua udhibiti wa mji wa Gaza Jumapili ijayo, wakati jeshi baadaye litawasilisha mipango ya kina na ratiba ya operesheni hiyo katika ngazi ya kisiasa, kulingana na Mamlaka ya Utangazaji.
Jeshi la Israel lilisema katika taarifa yake kwamba wakati wa mkutano wa Mkuu wa Majeshi na viongozi wa usalama na kijeshi, "wazo kuu la mpango wa hatua zinazofuata katika Ukanda wa Gaza lilipitishwa, kwa mujibu wa maagizo ya kisiasa."
Baraza la Mawaziri la Usalama liliidhinisha mpango siku ya Ijumaa wa kudhibiti mji wa Gaza na awamu inayofuata ya vita katika eneo la Palestina.
Unaweza pia kusoma:
Muda muhimu Alaska: Trump kukutana na Putin huku Ukraine ikitengwa
Maafisa wa Marekani na Urusi watakutana katika jimbo la Alaska kabla ya mkutano wa Ijumaa unaotarajiwa kati ya Rais Donald Trump na Vladimir Putin.
Wawili hao watakutana kwa mara ya kwanza baada ya miaka sita, huku Trump akijaribu kutunga ahadi muhimu ya kampeni ya kumaliza vita vya Urusi nchini Ukraine.
Rais wa Marekani, ambaye amejionyesha kama mtu wa kuleta amani duniani, anatumaini kuimarisha uhusiano wake wa kibinafsi na Putin ili kufikia muafaka wa kusitisha mapigano ambapo wengine wameshindwa.
Siku ya Alhamisi alikadiria kuwa kwa "fursa ya 25%" mkutano huo hautafanikiwa.
Kiongozi wa Ukraine Volodymyr Zelensky ameondolewa kwenye mazungumzo hayo, na kuonya kuwa maazimio yoyote yatakayotolewa bila kuwepo kwake hayatakuwa na maana yoyote.
Huko Anchorage kuna dalili chache za mkutano wa hali ya juu unaokuja, isipokuwa vyombo vya habari vya kimataifa ambavyo vimefika kwenye eneo hilo.
Mkutano wa Ijumaa kati ya viongozi hao wawili utafanyika katika kambi ya kijeshi ya Marekani iliyo karibu - ikiwa ni taswira ya wasiwasi wa kiusalama na mpango wa kuketi kwa ajili ya mazungumzo hayo umefupishwa, ikipagwa kuwa mkutano huoutadumu kwa saa chache tu.
Mkutano huo unakuja wiki moja baada ya makataa ya Trump yakikaribia kwa Urusi kufikia usitishaji vita au kukabiliwa na vikwazo vipya vikali.
Soma zaidi:
Hujambo na karibu kwa matangazo haya ya mubashara, kwa habari za kikanda na kimataifa.