Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Dead Hand: Usichokijua kuhusu silaha hii ya urusi inayoweza kuangamiza dunia
"Trump anapaswa kukumbuka jinsi 'mkono uliokufa' ulivyo hatari," ni maneno ambayo rais wa zamani wa Urusi Dmitry Medvedev alitumia akihutubia Marekani, suala ambalo liliikasirisha Ikulu ya Whitehouse na kurudisha kumbukumbu za Vita Baridi.
Kauli ya Medvedev, ambaye kwa sasa ni naibu mwenyekiti wa Baraza la Usalama la Taifa la Urusi, inajiri baada ya Rais wa Marekani Donald Trump kuweka makataa kwa Urusi kusitisha vita vyake nchini Ukraine.
Kauli kali za uchochezi
Trump alitangaza siku ya Ijumaa kwamba aliamuru kutumwa kwa nyambizi mbili za nyuklia , kujibu matamshi ya "uchochezi" ya afisa wa Urusi.
Elena Suponina, mshauri katika Kituo cha Urusi cha Mafunzo ya Kimataifa, aliiambia BBC kwamba matamshi ya Medvedev yalikuwa "ya ukweli mtupu," akibainisha kuwa alirejelea uwezo wa Urusi na umiliki wa silaha za nyuklia.
Ingawa matamshi ya Medvedev "yalikosa mwelekeo," Waziri wa Mambo ya Nje wa Urusi Sergei Lavrov alituliza mvutano na kuashiria kwamba Moscow iko tayari kwa mazungumzo na Washington na kuendelea na mazungumzo na Ukraine, kulingana na Suponina.
Je, mfumo wa 'mkono uliokufa' ni nini?
Shirika la habari la Urusi TASS lilielezea 'Dead Hand 'kama mfumo wa kuzuia nyuklia ambao hutoa mashambulio makubwa ya kulipiza kisasi cha shambulio la nyuklia ..
Katika Umoja wa Kisovyeti, mfumo huo uliitwa "Mashambulizi ya kupindukia ," wakati katika nchi za Magharibi, wakati wa Vita Baridi karne nyingi zilizopita, uliitwa "mkono wa kifo."
Baadhi ya vyombo vya habari vimeelezea "Dead Hand" kama mfumo wa kiotomatiki wa kudhibiti silaha za nyuklia uliotengenezwa na Muungano wa Sovieti wakati wa Vita Baridi ili kudhibiti silaha zake za nyuklia.
Pia ni mfumo wa siri wa amri ya nyuklia wa Urusi uliyoundwa kurusha makombora ya nyuklia iwapo mji mkuu wa Moscow utashambuliwa.
Mtaalamu wa kijeshi wa Marekani ameielezea kama "Mashine ya Siku ya Mwisho."
Ripoti ya New York Times inasemaje?
Mwaka wa 1993, gazeti la New York Times lilichapisha mahojiano na mtaalamu wa Marekani wa masuala ya kijeshi ya Urusi, Ross Blair, ambapo alisema kuwa Urusi ilikuwa na mfumo wa kompyuta wenye uwezo wa kurusha moja kwa moja makombora yake ya nyuklia wakati wa vita, ikiwa makamanda wa kijeshi walikuwa wamekufa au hawawezi kuongoza vita.
Brown, ambaye amefanya mahojiano ya kina na maafisa wanaohusika na silaha za Urusi na vifaa vinavyohusiana, alielezea mfumo huo kama "mashine ya siku ya mwisho." Mahojiano hayo yamezua utata juu ya usahihi wa mfumo huu.
Shirika la Ujasusi la Ulinzi la Marekani lilisema katika ripoti ya 2017 kwamba mifumo ya amri na udhibiti ya Urusi iliundwa kwa hali mbaya zaidi.
Alifafanua kuwa mifumo hii imeundwa ili kuwezesha usambazaji wa maagizo ya mashambulizi wakati wa shambulio la nyuklia kupitia mifumo kadhaa, ukiwemo mfumo wa "Perimeter".
"Moscow inadumisha mfumo wa Circular, ambao umeundwa ili kuhakikisha kuwa amri ya kulipiza kisasi inaweza kutolewa katika tukio la shambulio la nyuklia dhidi ya Urusi," ripoti hiyo ilisema.
Mnamo mwaka wa 2011, kamanda wa Kikosi cha makombora ya Kimkakati cha Urusi, Sergei Karakayev, alitoa mahojiano na gazeti la Komsomolskaya Pravda.
Afisa huyo alisema kuwa mfumo wa "Perimeter" ulikuwepo katika Umoja wa Kisovyeti, akibainisha kuwa "mfumo huo bado unafanya kazi na upo."
Maelezo ya kuvutia
Mchambuzi wa kijeshi wa Urusi Sergei Shashkov aliiambia BBC kwamba mfumo huo utaruhusu makombora ya nyuklia ya Urusi kurushwa moja kwa moja katika malengo yao hata kama nguzo zote za amri zitaharibiwa. Lakini Shashkov alitilia shaka hesabu za utawala, akisema, "Hakuna kitu cha kuaminika."
Kwa upande wake, Suponina aliiambia BBC kuwa jina na maelezo ya mfumo huo "ni ya kuvutia sana" na yametajwa katika filamu, fasihi na baadhi ya wataalamu.
Suponina alisema kuwa mfumo wa "Hand of Death" ni mfumo unaofuatilia silaha za nyuklia ili kuzidhibiti na kuhakikisha hazilipuki kwa bahati mbaya au kimakosa.
Je, "Dead Hand" inafanya kazi vipi?
Ripoti iliyochapishwa katika gazeti la serikali ya Urusi Rossiyskaya Gazeta ilisema kuwa mashirika ya kijasusi ya kigeni yameweza, kwa miongo kadhaa, kutambua kanuni za jumla tu za mfumo wa uendeshaji.
Mnamo 1993, mtaalam wa Marekani Blair alisema kuwa mfumo wa Urusi uliundwa kutumiwa na makamanda wa kijeshi katika hali mbaya, na kwamba kwa nadharia mfumo huo utachukua hatua ikiwa tu sensa zake zitagundua shambulio la nyuklia huko Moscow.
"Mfumo huu unafanya kazi kwa uangalizi mdogo au hakuna kabisa wa kibinadamu, unaweza kutuma ujumbe wa siri maelfu ya maili kwa vikosi vya kijeshi, na unaweza kurusha makombora ya nyuklia bila usaidizi wa kibinadamu," Blair alisema, akiongeza kuwa mfumo huo "una uwezekano wa kufanya makosa."
Gazeti la Military.com, ambalo linaangazia habari za kijeshi za Marekani, lilisema kuwa mfumo huo unaweza kurusha kombora linaloongozwa na kichwa cha nyuklia, ambacho hutuma amri za kurusha vituo vya nyuklia vya Urusi, hata ikiwa kuna kuingiliwa na redio.
Shirika la habari la serikali ya Urusi, Sputnik, liliripoti kwamba mfumo huo umeboreshwa ili kugundua kurushwa kwa makombora ya balestiki yanayolenga Urusi kupitia satelaiti, na kusambaza haraka maagizo kwa mashirika mengine yanayohusika na kukabiliana na mashambulio ya makombora.
Imetafsiriwa na Seif Abdalla