Trump kuipatia Ukraine makombora ya masafa marefu, Vance asema

Chanzo cha picha, Getty Images
Marekani inazingatia ombi la Ukraine la kutaka makombora ya masafa marefu ya Tomahawk, Makamu wa Rais wa Marekani JD Vance amesema.
Hatahivyo, Vance aliongeza kuwa Rais Donald Trump atakuwa akifanya "uamuzi wa mwisho" kuhusu suala hilo.
Kwa muda mrefu Kyiv imekuwa ikitoa wito kwa washirika wake wa Magharibi kuipatia silaha zinazoweza kugonga miji mikubwa ya Urusi iliyo mbali na mstari wa mbele, ikisema kwamba zingeisaidia Ukraine kudhoofisha kijeshi Urusi na kumaliza vita.
"Ikiwa gharama ya kuendeleza vita vya Moscow ni kubwa mno, italazimika kuanzisha mazungumzo ya amani," naibu waziri wa ulinzi Ivan Havryliuk aliambia BBC.
Msemaji wa Kremlin Dmitry Peskov alipuuza kauli ya Vance, akisema "hakuna dawa ambayo inaweza kubadilisha hali ya serikali ya Kyiv." "Iwe ni Tomahawks au makombora mengine, hayataweza kubadilisha nguvu," aliongeza.
Makombora ya Tomahawk yana masafa ya kilomita 2,500 (maili 1,550), ambayo yataifanya Moscow kufikia Ukraine. Wakati Vance alisalia kuwa na utata kuhusu ombi la Ukraine kwa Tomahawks katika hotuba yake siku ya Jumapili, mjumbe maalum wa Marekani nchini Ukraine, Keith Kellogg, alieleza Trump alikuwa tayari ameidhinisha mashambulizi ndani ya ardhi ya Urusi.
Alipoulizwa kwenye Fox News kama Washington iliruhusu Kyiv kufanya shambulizi la masafa marefu ndani ya Urusi katika matukio maalum, Kellogg alisema: "Jibu ni ndiyo, tumia uwezo wa kupiga kwa kina, hakuna vitu kama mahali patakatifu."
Maoni ya Vance na Kellogg yanalingana na mabadiliko ya hivi karibuni ya utawala wa Marekani kuhusiana na vita.
Siku ya Jumapili, shambulizi kubwa la saa 12 lililohusisha mamia ya ndege zisizo na rubani na karibu makombora 50 lilisababisha vifo vya watu wanne mjini Kyiv na takribani 70 kujeruhiwa.
Mwanahabari wa Ukraine Havryliuk aliiambia BBC kwamba Urusi itaongeza tu ukubwa na ukali wa mashambulizi yake ya angani.
Unaweza kusoma;













