Serikali ya Marekani imemfungulia mashtaka
raia mmoja wa Afghanistan kuhusiana na njama ya Iran ya kutaka kumuua Donald
Trump kabla ya kuchaguliwa kuwa rais ajaye.
Siku ya Ijumaa wizara ya sheria ya nchi hiyo ilifichua mashtaka dhidi ya Farhad Shakeri, 51, ikidai
kuwa madai alipewa jukumu la "kuandaa mpango" wa kumuua Trump.
Serikali ya Marekani inasema Bw Shakeri
hajakamatwa na inaaminika kuwa yuko Iran.
Iran ambayo ilieleza madai hayo kuwa "hayana
msingi kabisa".
Katika malalamishi ya jinai
yaliyowasilishwa katika mahakama ya Manhattan, waendesha mashtaka wanadai kuwa
afisa mmoja katika jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Iran alimwelekeza Bw
Shakeri mnamo Septemba kubuni mpango wa kumuua Trump.
"Wizara ya sheria imeshtaki mtu wa utawala wa Irani ambaye alipewa
jukumu na serikali la kupanga mtandao wa washirika wa uhalifu ili kuendeleza
njama za mauaji ya Iran dhidi ya watu inaowalenga , akiwemo Rais mteule Donald
Trump," Mwanasheria Mkuu wa Marekani Merrick Garland alisema katika
taarifa yake.
Watu wengine wawili pia walishtakiwa kwa
kupewa kazi ya kumuua mwandishi wa habari wa Marekani ambaye alikuwa mkosoaji
mkubwa wa Iran.
Walitambuliwa kama Carlisle Rivera, anayejulikana pia kama
"Pop", 49, kutoka Brooklyn, na Jonathon Loadholt, 36, kutoka Staten
Island.
Wawili hao walifikishwa mahakamani katika
Wilaya ya Kusini mwa New York siku ya Alhamisi na wanazuiliwa huku wakisubiri
kusikilizwa kwa kesi.
Msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya Iran
Esmaeil Baghaei amesema shutuma sawa na hizo za majaribio ya kuwaua marais wa
Marekani zilitolewa siku za nyuma jambo ambalo Iran ililikanusha na kuendelea kusema
kuwa ni uongo.