Mwanamke mkongwe zaidi duniani afariki New York

Chanzo cha picha, Reuters
Mwanamke aliyetambuliwa kuwa mkongwe zaidi duniani ameaga dunia akitibiwa jijini New York, Marekani, madaktari wamesema.
Susannah Mushatt Jones, amefariki akiwa na umri wa miaka 116.

Chanzo cha picha, Reuters
Alizaliwa eneo la mashambani jimbo la Alabama mwaka 1899, na amekuwa akiugua kwa siku kadha.
- <link type="page"><caption> Mwanamume mzee zaidi duniani afariki Japan</caption><url href="http://www.bbc.com/swahili/habari/2016/01/160119_japan_oldest_man_dead" platform="highweb"/></link>
Mwanamke Mwitaliano, Emma Morano, ambaye ni mdogo wa umri wa Bi Jones kwa miezi kadha, sasa ndiye anayetambuliwa kuwa mwanamke mkongwe zaidi duniani.

Chanzo cha picha, AP
Anaaminika kuwa mtu pekee duniani aliyezaliwa karne ya 19 ambaye bado yuko hai.








