Zuma kulipa fedha za ukarabati wa nyumba yake

Nyumba ya Zuma huko Nkandla

Chanzo cha picha, Reuters

Maelezo ya picha, Nyumba ya Zuma huko Nkandla

Rais wa Afrika Kusini Jacob Zuma amekubali kulipa kiasi cha dola milioni 23 ambazo serikali ilitumia kurekebisha nyumba yake iliopo mashambani.

Katika ripoti ya 2014,ripoti yake mlinzi wa umma imesema bw.Zuma alifaidi kinyume na sheria.

Bw.Zuma amesema kuwa mkaguzi mkuu na waziri wa fedha wanafaa kubaini ni kiasi gani anapaswa kulipa ili kumaliza mgogoro huo.

Tangazo hilo linajiri wiki moja kabla ya kusikilizwa kwa swala hilo.

Rais Jacob Zuma wa Afrika Kusini

Chanzo cha picha, Getty

Maelezo ya picha, Rais Jacob Zuma wa Afrika Kusini

Urekebishaji wa makao hayo katika kijiji cha Nklanda nyumbani kwa zuma katika mkoa wa kwa Zulu Natal umezua mgogoro mkubwa wa kisiasa nchini Afrika Kusini.

Baadhi ya fedha zilitumiwa kujenga ukumbi wa maonyesho,kidimbwi cha maji na zizi la ng'ombe.