Coleen Rooney kula kondo la nyuma

Coleen

Chanzo cha picha, AFP

Maelezo ya picha, Coleen alijifungua mtoto mvulana Jumapili

Mke wa nahodha wa Manchester United Wayne Rooney, Coleen Rooney, ametangaza kwamba atakula kondo lake la nyuma baada ya kuzaliwa kwa mwana wao wa tatu aliyepewa jina Kit.

Kondo hilo la nyuma, limetengenezwa na kuwa vidonge na anasema amekabidhiwa vikiwa vimewekwa kwenye jagi.

Vidonge hivyo vimeandaliwa na “mtaalamu wa kugeuza kondo la nyuma kuwa vidonge”, anayesema kumeza vidonge hivyo humsaidia mwanamke aliyejifungua kurejelea hali yake ya kawaida haraka.

Mwingine aliyewahi kufanya hivyo awali ni Kim Kardashian, aliyekula kondo lake la nyuma baada ya kujifungua mtoto wake wa kwanza North West.

  • <link type="page"><caption> Rooney na mkewe wajaliwa mtoto mvulana</caption><url href="http://www.bbc.com/swahili/michezo/2016/01/160125_rooney_baby_boy" platform="highweb"/></link>

Mwigizaji wa Mad Men January Jones pia alikula kondo lake la nyuma baada ya kujifungua mwanawe wa kiume Xander mwaka 2011.

Chanzo cha picha, Coleen Rooney Twitter

Hata hivyo, Coleen ameandika kwenye Twitter kwamba haigi Kim na kwamba hakuwa amesikia kuhusu mwigizaji huyo.

Coleen alijifungua mtoto wake wa tatu wa kiume Jumapili.

Ana watoto wengine wawili wa kiume: Kai naKlay.

Wengine waliowahi kula kondo la nyuma ni mwigizaji wa Clueless Alicia Silverstone made na Kourtney Kardashian aliyemfuata dada baada ya kujifungua mwanawe wa tatu 2014.