Trevor Noah afanyiwa upasuaji wa dharura

Chanzo cha picha,
Mashabiki wa kipindi mashuhuri cha The Daily Show hawakupata fursa ya kutazama kipindi kipya Jumatano baada ya Trevor Noah kutofika kazini.
Badala yake walitazama marudio ya mojawapo ya vipindi alivyowahi kutangaza awali.
Mcheshi huyo kutoka Afrika Kusini alikuwa na sababu muhimu ya kutoonekana runingani, kwani alikuwa amefanyiwa upasuaji wa dharura wa kuondoa kidole tumbo Jumatano asubuhi.
“Tuna furaha kutangaza kwamba upasuaji ulifaniyka vyema na anapata nafuu,” kituo cha habari cha Comedy Central kimesema.

Chanzo cha picha, Trevor Noah
Noah, aliyechukua usukani kipindi cha The Daily Show kutoka kwa Jon Stewart mwezi Septemba, anatarajiwa kurejea kazini anatarajiwa kurejea kazini Alhamisi mgeni wake akiwa mwigizaji Regina King.








