Picha bora za kutawazwa kwa Mfalme Charlse

Mfalme Charles na Malkia Camilla wametawazwa katika sherehe iliyosheheni muziki na ishara ndani ya ukumbi wa Westminster Abbey.

Akiwa amevalia vazi la babu yake, Mfalme Charles alikula kiapo na kupakwa mafuta matakatifu, kabla ya Taji la kihistoria la St Edward kuwekwa kichwani mwake.

Mbunge wa Conservative Penny Mordaunt aliwasilisha upanga wenye vito vya sadaka kwa Mfalme.

Malkia Camilla alitawazwa katika hafla fupi na kuvishwa Taji ya Malkia Mary. Hakula kiapo.

Baada ya sherehe hiyo, Mfalme na Malkia walifanya msafara katika mitaa ya katikati mwa London katika gari maalum la Dhahabu.

Mwana Mfalme Harry aliwasili bila mke wake, Meghan, Duchess wa Sussex.

Mwanamfalme Louis akifuatilia yanayojiri huku akipiga miayo mara kwa mara

Wageni waalikwa, ikiwa ni pamoja na Familia ya Kifalme, watu mashuhuri, viongozi wa kidini na wakuu wa nchi, waliketi kabla ya kuwasili kwa Mfalme.

Picha zote zina haki miliki.