Tetemeko la Ardhi Uturuki: Ulimwengu waungana baada kukumbwa na janga

Wakati Uturuki na Syria zikianza kutathmini uharibifu uliosababishwa na tetemeko la ardhi lenye kipimo cha 7.8 ambalo hadi sasa limesababisha vifo vya watu wasiopungua 4,800, nchi mbalimbali duniani zimejipanga kusaidia juhudi za uokoaji.

Mvua na theluji inaathiri waokoaji, lakini timu maalum kutoka mataifa mengi, ikiwa ni pamoja na Italia, Marekani, Israel na Taiwan - ziko njiani.

1px transparent line
Msaada wa shirika la Red crescent katika masanduku karibu na mlango wa ndege

Chanzo cha picha, Reuters

Maelezo ya picha, Iraq inatoa msaada kwa Syria. Vikosi vya usalama vilichakata vifaa kutoka kwa shirika la misaada la Red Crescent ili kutuma katika nchi jirani
Wanaume watatu wakipakia vifaa vya misaada kweye lori kwa ajili ya Syria

Chanzo cha picha, Reuters

Maelezo ya picha, Wanajeshi wa Iraq na wafanyakazi wa shirika la Red Crescent wakipakia vifaa hivyo kwenye lori.
Afisa wa Taiwan akisimama mbele ya kundi la waokoaji official stands in front of a group of rescuers

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Waokoaji kutoka Taiwan wanajipanga kusaidia katika oparesheni ya kutafuta na kuokoa manusura nchini Uturuki.
Kundi la wazima moto likipakia vifaa kwenye ndege

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Kundi maalumu la wazima moto kutoka Jamhuri ya Czech itasaidia kutafuta manusura kwenye vifusi nchini Uturuki.
Mbwa wakiwa karibu na wafanyakazi wa USAR staff katika uwanja wa ndege

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Kundi la Czech USAR lina mafunzo maalum ya kutafuta watu ambao huenda wamezikwe kwenye vifusi.
Maafisa wa kundi la utafutaji na uokoaji ya Uholanzi

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Maafisa wa kundi la utafutaji na uokoaji ya Uholanzi walipaswa kusafiri kutoka Eindhoven kutoa usaidizi nchini Uturuki.
Mwanamke akimkumbatia mbwa

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Takriban wazima moto 50 na wafanyikazi wa matibabu waliondoka Pisa, Italia, kusaidia katika mpaka wa Syria na Uturuki katika juhudi za uokoaji.
Wazima moto wakisimama karibu na mizigo yao

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Rome inasema safari zaidi za ndege zitafuata baada ya wazima moto kuwasili, wakileta wafanyikazi wa matibabu na vifaa vya Uturuki.
A Greek soldier stands near a plane being loaded with supplies

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Waziri Mkuu wa Ugiriki siku ya Jumatatu aliahidi kufanya "kila juhudi" kusaidia jirani yake Uturuki. Walituma vifaa na waokoaji kuelekea Uturuki siku hiyo hiyo yamkasa.
Kindi la waokoaji wakisimama karibu na ndege

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Ugiriki na Uturuki kihistoria zimekumbwa na migogoro mbalimbali ya mipaka na kitamaduni.
Two men in a fire truck pass a border check

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Vikosi vya uokoaji vya Bulgaria vilisambazwa katika Lango la Mpaka wa Kapikule kusaidia katika juhudi za kutoa misaada kote Uturuki.
A man stands near aid and checks a list in Israel

Chanzo cha picha, Reuters

Maelezo ya picha, Kitengo cha kutoa msaada cha jeshi la ulinzi la Israeli lilielekea Uturuki kusaidia juhudi za uokozi baada ya tetemeko la ardhi. Waziri Mkuu wa Israel pia alisema ameidhinisha kutumwa msaada kwa Syria - ambayo serikali yake haitambui Israel.
Men in army uniforms walk on tarmac towards a plane

Chanzo cha picha, Reuters

Maelezo ya picha, Israel ilipokea ombi la kuisaidia Syria kupitia njia za kidiplomasia. Lakini Damascus ilikataa kuomba msaada.
Four US firefighters pack supplies to go to Turkey

Chanzo cha picha, Reuters

Maelezo ya picha, Rais wa Marekani Joe Biden alisema maafisa wanajitahidi kuondoka haraka iwezekanavyo ili kuanza kusaidia juhudi za utafutaji na uokoaji za Uturuki.
A US firefighter secures supplies for Turkey

Chanzo cha picha, Reuters

Maelezo ya picha, Marekani ilisema itatuma timu mbili za utafutaji na uokoaji zenye takriban watu 80 kila moja.
At the Turkish embassy in Moscow, flowers are laid

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Katika ubalozi wa Uturuki mjini Moscow, kumewekwa shada la maua. Pia kuna mshumaa umewashwa na kando yake kumebandikwa karatasi iliyoandikwa ujumbe "Pole kwa Uturuki". Urusi imetoa msaada kwa Uturuki na Syria.

Picha zote zina haki miliki.