Malkia Elizabeth II: Maisha yake kabla ya kuwa Malkia

Chanzo cha picha, Getty Images
Wakati Princess Elizabeth alizaliwa haikutarajiwa kamwe kuwa angekuwa malkia.
Baba yake alikuwa mtoto wa pili wa Mfalme George V, kwa hivyo ilifikiriwa kuwa angeishi maisha ya kifalme kidogo tu.
Lakini mjomba wake alipoacha kiti hicho cha enzi bila kutarajia, alimtengenezea njia ya kuwa Malkia aliyehudumu kwa muda mrefu zaidi katika historia ya Uingereza.
Huku kukiwa hakuna ndugu wa kiume, ikawa jukwaa limeandaliwa kwa Elizabeth siku moja kutwaa taji la kifalme.
1926

Chanzo cha picha, PA
Tofauti na watoto wengi wa kifalme wa wakati huo Elizabeth hakuzaliwa katika jumba la kifalme au ngome.
Alizaliwa katika nyumba huko Mayfair, ambapo sasa kuna mkahawa wa Cantonese, na alipewa jina la utani Lilibet.
Alipozaliwa wazazi wake walikuwa Duke na Duchess wa York lakini miaka 10 baadaye wakawa mfalme na malkia.
1935

Chanzo cha picha, Getty Images
Babu Uingereza ndio yule Elizabeth na dada yake mdogo Margaret walimwita babu yao, Mfalme George V.
Walionekana kwa mara ya kwanza kwenye roshani ya Jumba la Buckingham pamoja na babu na bibi zao.
Hata katika umri mdogo, angesalimia umma kwa mtindo uliomaarufu wa kifalme.
1937

Chanzo cha picha, Getty Images
Baba yake Elizabeth alikua mfalme bila kutarajia kaka yake alipoacha kiti cha enzi ma kwenda kumuoa mtaliki wa Kimarekani.
Ilimaanisha kwamba alipaswa kusomeshwa nyumbani na kufundishwa masomo kama vile historia ya kikatiba.
Ingawa alikuwa binti wa kifalme, hakuwa na marafiki wengi wa rika lake kwa hivyo kampuni ya Girl Guides iliundwa katika ikulu.
1940

Chanzo cha picha, Getty Images
Wakati wa Vita vya Pili vya Dunia, Elizabeth alitoa hotuba yake ya kwanza kwa watoto wa Jumuiya ya Madola.
Elizabeth na dada yake mdogo Margaret walitumaini kuwafikia watoto wengi waliokuwa wakiishi mbali na nyumbani kwa sababu ya vita.
''Amani ikija, kumbuka itakuwa kwa ajili yetu, watoto wa leo, kufanya ulimwengu wa kesho kuwa mahali bora na penye furaha''.
1945

Chanzo cha picha, PA
Elizabeth alijiunga na tawi la wanajeshi wa Uingereza wakati wa Vita vya Pili vya Dunia na ilijulikana kama 'Second Subaltern Elizabeth Windsor'.
Alipata mafunzo ya udereva na aliendesha lori la kijeshi.
Binti wa kifalme wakati mwingine alijulikana kama No 230873 alipokuwa akihudumu.
1947

Chanzo cha picha, PA
Elizabeth aliolewa na Luteni Philip Mountbatten miaka miwili baada ya vita.
Binti wa kifalme ilimbidi akusanye kuponi za mgao wa mavazi kwa ajili ya mavazi yake, kama bibi arusi mwingine yeyote nchini Uingereza wakati huo.
Tofauti na wengine, harusi yake ilitangazwa kwa watu milioni 200 kote ulimwenguni.
1949

Chanzo cha picha, PA
Prince Charles alizaliwa mwaka wa 1948. Elizabeth na Philip waliendelea kupata watoto wengine watatu, Princess Anne, Prince Andrew na Prince Edward.
Familia yao ingeendelea kukua, ikiwa na wajukuu wanane na vitukuu 12.
1953

Chanzo cha picha, Getty Images
Baada ya kifo cha baba yake mnamo 1952, Elizabeth alikua Malkia Elizabeth II.
Alitawazwa mwaka mmoja baadaye huko Westminster Abbey na akatangaza hotuba kwa Jumuiya ya Madola.
''Katika maisha yangu yote na kwa moyo wangu wote nitajitahidi kustahili kutumainiwa,'' alisema.










