Siwezi kumsahau'- Wanajeshi wa Myanmar wakiri ukatili

A man tries to put out a fire

Wanajeshi katika jeshi la Myanmar wamekiri kuwauwa, kuwatesa na kuwabaka raia katika maohiano ya kipekee na BBC . Kwa mara ya kwanza wametoa maelezo ya ushahidi wa kuendea kwa ukiukaji wa haki za binadamu ambavyo wanasema waliamrishwa kuvifanya.

Onyo; Taarifa hii ina maelezo ya unyanyasaji wa kingono na mukatili

"Waliniamrisha kutesa, kuwaibia na kuwauwa watu wasio na hatia."Maung Oo anasema alifikiri alikuwa amepatiwa kazi katika jeshi kama mlinzi.

Lakini aliwa sehemu ya kikosi cha batalioni ambacho kiliwauwa raia waliokuwa wamejificha katika katika makazi ya mapadre mwezi Mei 2022.

"Tuliamrishwa kuwazingira wanaume na kuwauwa kwa kuwapiga risasi," anasema. "Kitu cha kusikitisha ni kwamba tulilazimika kuwauwa wazee wanaume na mwanamke."

Ushuhuda wa wanajeshi sita, akiwemo mwenye cheo cha Kopro, pamja na baadhi ya waathiriwa unatoa mwanagaza nadra wa shauku ya jeshi ya kunyakuwa mamlaka. Majina yote ya Myanmar katika taarifa hiiyamebadilishwa ili kuulinda utambulisho wao.

Wanajeshi, ambao hivi karibuni walitoroka jeshi , wako chini ya ulinzi wa kikosi cha ulinzi wa raia cha People's Defence Force (PDF), mtandao wa makundi ya ya raia yanayopigania kurejesha demokrasia.

Jeshi lilinyakua mamlaka kutoka kwa serikali iliyochaguliw akidemokrasia iliyoongozwa na Aung San Suu Kyi katika mapinduzi ya mwaka jana. Inajaribu kukabiliana na raia wenye silaha wanaoipinga.

2px presentational grey line

Tarehe 20 Disemaba mwaka jana, helikopta mbili zilizingira kijiji cha Yae Myet kilichopo katikati mwa Myanmar, na kuwashusha wanajeshi pale waliopewa amri ya kufyatua risasi.

Takriban watu watano tofauti , waliozungumza bila kufahamiana waliiambia BBC kile kilichotokea.

Wanasema jeshi liliingia katika makundi matatu tofauti, na kuwapiga risasi wanaume na watoto bila kuchagua.

"amri ilikuwa ni kumpiga risasi yeyote unayemuona," anasema Kopro Aung kutoka eneo ambalo halikufichuliwa katika eneo la msitu la Mynmar.

Anasema kuwa baadhi ya watu walikuwa wamejificha katika kile walichodhani kwua ni mahala salama, lakini kadri wanajeshi walipokuwa wakiwasogelea "walianza kukimbia na tukawapiga risasi".

Kopro Aung anakiri kuwa kikosi chake kiliwauwa kwa risasi wanaume watano na kuwazika.

"Pia tulikuwa tumemrishwa kuchoma nyumba yoyote kubwa na nzuri katika kijiji," anasema.

Wanajeshi walifanya gwaride katika maeneo ya kijiji hicho wakichoma nyumba na kupaza sautu wakisema, "Choma, Choma!"

Kopro Aung alichoma moto majengo manne . Wale waliohojiwa walisema nyumba zipatazo 60 zilichomwa, na kuiacha sehemu kubwa ya kijiji ikiwa majivu.

Your device may not support this visualisation

Wengi wa wanavijiji walikuwa wametoroka, lakini sio kila mtu. Nyumba moja katikati ya kijiji ilikuwa inakaliwa.

Thiha anasema walikuwa wamejiunga na jeshi kwa miezi mitano tu kabla ya uvamizi. Sawa na wengine wengi, aliajiriwa kutoka katika jamii na anasema hakuwa amepatiw amafunzo. Kazi hizi hufahamika nchini humo kama Anghar-Sit-Thar au " wanajeshi wa kukodiwa".

Wakati huo alikuwa akilipwa mshahara mzuri wa pesa za Mynmar 200,000 Myanmar- Khat (takriban dola 100 za kikmarekani) kwa mwezi. Anakumbuka kile kilichotokea katika nyumba ile vizuri.

The girl's house
Maelezo ya picha, Mjomba wa msichana alisema kuwa walivunjika moyo.

Alimuona msichana huyo akiwa amekwama katika chumba cha mabati katika nyumba ambayo walikuwa wanataka kuichoma kwa moto."Siwezi kusahau akipiga vmayowe, bado naweza kuisikiliza sauti yake katika masikio yangu na naikumbuka katika moto wangu ," anasema.

Wakati alipomwambia mkuu wake, alijibu, "Nilikuwambia kuua yeyote unayemuona ". Kwahiyo Thiha akawasha moto ndani ya chumba.

Kopro Aung alikuwa pia pale na kusikia kilio chake alipokuwa akichomwa angali hai. "Ilivunja moyo sana kumsikia. Tulisikia sauti yake mara kwa mara kwa dakika zipatazo 15 wakati nyumba ilipokuwa inaungua," anakumbuka.

BBC iliifuatilia familia ya msichana, ambao walizungumza mbele ya vifusi vya nyumba yao.

Ndugu yake U Myint alisema kuwa msichana huyo alikuw ana matatizo ya afya ya akili na alikuwa ameachwa nyumbani wakati wazazi wake walipokuwa wameenda kufanya kazi. "Alijaribu kutoroka lakini walimzuia na kumuacha aungue ," anasema.

2px presentational grey line

Si msichana mdogo pekee aliyeumia mikononi mwa wanajeshi hawa.

Thiha anasema alijiunga na jeshi kwa ajili ya pesa lakini alishitushwa na kile alicholazimishwa kukifanya na mateso aliyoyashuhudia yakifanyika.

Anazungumzia kuhusu kikundi cha vija wa kike ambao waliwakamata katika Yae Myet.

Afisa aliwakabidhi kwa wakuu wake na alisema , "Fanya kama mnavyotaka," anakumbuka. ''Anasema waliwabaka wasichana lakini yeye hakuhusika. Tuliwafuatilia wawili kati ya wasichana hawa.

Pa Pa na Khin Htwe wanasema walikutana na wanajeshi barabarani walipokuwa wakijaribu kutoroka kwenda mbali. Hawakuwa wakazi wa kijiji cha Yae Myet, twalikuwa wamekwenda kumuona fundi wao wa nguo pale.

Lica ya kusisitiza kuwa hawakuwa wapiganaji wa PDF au hata hawakuwa wakazi wa kijiji hicho, walifungwa katika shule yae neo hilo kwa siku tatu. Kila usiku walikuwa wakibakwa mara kwa mara na watekaji wao, wanasema. "Wa;liufunika uso wang una kunisukuma chini kwa nguvu, wakavua nguo zangu na kunibaka ," Pa Pa anasema "Nilipiga mayowe huku wakiendelea kunibaka ."

Aliwaomba wanajeshi wamuhurumie waache kumbaka , lakini walimpiga kichwani na kumtishia kwa mtutu wa bunduki. "Ilibidi tukubali bila kupinga kwasababu tulikuwa tunaogopa kwamba wangetuua ," anasema dada yake Khin Htwe, ambaye alikuwa anatetemeka wakati akizungumza.

Wasichana walikuwa na uoga sana wa kuwatazama wabakaji wao, lakini wanasema wanakumbuka wakiwaona baadhi wakiwa wamevalia nguo za kawaida na wengine walikuwa wamevaa sare ya jeshi.

"Wakati tulipomkamata msichana mdogo," anakumbuka mwanajeshi Thiha, " walikuwa anasema, 'hii ni kwasbabu unaunga mkono PDF huku waki (wabaka ) wasichana."

Rakriban watu 10 waliuawa katika ghasia za Yae Myet na wasichana wanane waliripotiwa kubakwa kwa kipindi cha siku tatu.

2px presentational grey line

Mauaji ya kikatili ambayo wanajeshi wa kukodiwa ambayo Maung Oo alishiriki yalitokea tarehe 2 Mei, 2022 katika kijiji cha Ohake pho , katika jimbo la Sagaing pia. Ushahidi wake wa wajumbe wa kikundi chake cha Kitengo cha 33 kuhusu jinsi walivyozingira na kuwapiga risasi watu katika makazi ya makasisi unafanana na ushahidi wa mashuhuda na video ya kushitua ambayo BBC iliipata baada ya shambulio. Video hiyo inaonyesha miili tisa ya wafu iliyopangwa akiwemo mwanamke na mwanaume mwenye nywele za mvi wakiwa wamelala karibu.

Ishara za picha ziliashiria kuwa walipigwa rshasi kutokea nyuma na kwa karibu.

Bullet holes in a building
Maelezo ya picha, Askari aliyehusika katika mauaji anasema anajutia matendo yake

Pia tulizungumza na wanajiji ambao walishuhudia maasi. Walimtambua msichana huyo katika video ambaye alikuwa amelala kando ya mwanaume mzee. Alikuwa anaitwa Ma Moe Moe, na alikuwa amembeba mtoto na vipande vya dhahabu. Aliwaomba wanajeshi wasichukue vitu vyake.

"Licha ya mtoto aliyekuwa amembeba, walimpora vitu vyake na kumpiga risasi na kumuua. Pia waliwapanga wanaume a kuwapiga risasi mmoja baada ya mwingine anasema Hla Hla, ambaye alikuwa katika eneo la tukio lakini alinusurika.

Mtoto alinusika na sasa anatunzwa na ndugu.

Hla Hla anasema aliwsikia wanajeshi wakisema kwenye simu kwamba wamewauwa watu wanane au tisa, kwamba ilikuwa ni "tamu" kuwauwa watu na kuielezea kama ''siku yao ya mafanikio zaidi''.

Anasema waliondoka kijijini hapo wakishangilia "Ushindi! ushindi!"

Mwanamke mwingine alimuona mume wake akiuawa. "Walimpiga risasi kwenye paja, halafu wakamwambia ainamishe uso wake na wakampiga risasi kwenye takokalio lake . Mwisho wakampiga risasi ," anasema.

Wanajeshi wote sita waliozungumza na BBC walikiri kuchoma moto nyumba na vijiji katika maeneo yote ya kati kati mwa Myanmar. Hii inabaisha kuwa huu ulikuw amkakati uliopangwa wa kuangamiza yeyote anayeunga mkono upinzani.

2px presentational grey line

Inakuja huku baadhi wakisema jishi linahangaika kudhibiti vita vingi vya raia.

Alisisitiza kuwa alikuwa mjumbe wa PDF. "Alikuwa mfanyakazi wa kiwanda cha tende akijipatia riziki kwa njia ya kawaida. Nina mtoto wa kiume na wa kike na sijui jinsi ya kuendelea kuishi."

Maung Oo anasema anajutia matendo yake. "Kwahiyo, nitawambia yote ," anasema. "Ninataka kila mtu kujua ili waweze kuepuka kujipata katika hatima sawa na hii ."

Your device may not support this visualisation

Ushahidi wa Myanmar - kikundi cha watafiti wanaofuatilia visa vya ukiukaji wa haki za binadamu - kimehakikisha zaidi ya ripoti ripoti 200 za vijiji vilivyochomwa kwa njia hii kwa kipindi cha miezi 10 iliyopita.

Wanasema kiwango cha mashambulio haya mauaji kinaendelea kuongezeka kwa haraka, huku mashambulio walau 40 yakiripotiwa kufanyika katika miezi ya Januari na Februari, na kufuatiwa na mashambulio 60 katika miezi ya Machi na Aprili.

Your device may not support this visualisation

Hii si mara ya kwanza kwa jeshi la Myanmar kutumia sera ya kuunguza . Sera hii iliripotiwa sana dhidi ya watu wa jamii ya Rohingya katika mwaka 2017 katika jimbo la Rakhine.

Majimbo yenye milima yanayokaliwa na makabila yamekabiliwa na aina hizi za maasi kwa miongo mingi. Baadhi ya wapiganaji wa jamii hizi sasa wanasaidi kuwapatia mafunzo na kuwahami wapiganaji wa PDF katiavita vya hivi karibuni dhidi ya jeshi.

Utamaduni wa kutoadhibu wenye makosa ambapo wanajeshi wanaruhusiwa kupora na kuua, umekuwepo kwa miongo nchini Myanmar, Human Rights Watch inasema.

Ni nadra kwa watu kuwajibishwa kwa ukatili unaodaiwa kufanywa na jeshi.

2px presentational grey line

Lakini jeshi la Myanmar linaendelea kulazimika kuwakodi wanamgambo na wanajeshi kutokana na utoro na mauaji yanayofanywa na PDF.

Watu wapatao 10,000 wametoroka kutoka jeshini na polisi tangu yafanyike mapinduzi mwaka 2021, kwa mujibu wa kikundi kinachoitwa People's Embrace, kilichoundwa na wanajeshi na polisi wa zamani.

A house on fire
Maelezo ya picha, Jeshi limekuwa likiangamiza vijiji kwa makusudi.

"Jeshi linahangaika kudhibiti vita vingi vinavyopiganwa na raia dhidi yake," anasema Michael Martin kutoka kituo na stratejia na wasomi wa Stadi za kimataifa.

Majimbo ya Magway Sagaing (ambako matukio yaliyoelezewa juu yalitokea) kihistoria yalikuwa ni maeneo walikotoka watu walioajiriwa kufanya kazi katika jeshi la Myanmar.

Lakini vijana hapa badala yake wanachagua kujiunga na makundi ya PDF.

Kopro Aung alikuwa wazi kuhusu ni kwanini alitoroka katika jeshi: "Kama ningefikiria jeshi lingeshinda kwa muda mrefu, nisingehamia upande wa watu."

Anasema wanajeshi hawadiriki kuondoka kwenye ngome yao peke yao wana wasi wasi wanaweza kuuawa na PDF.

2px presentational grey line

"Kokote tunakoenda, tunaweza kwenda katika kikosi. Hakuna yeyote anayeweza kuwa tunatawala," anasema.

Tuliwasilisha madai katika uchunguzi kwa Jenerali Zaw Min Tun, msemaji wa jeshi la Myanmar. Katika taarifa, alikanusha kwamba jeshi limekuwa likiwalenga raia. Alisema kwua uvamizi wote walioufanya katika eneo lililotajwa katika taarifa hii lilikuwa la ni shambulio la kisheria na wale waliouliwa walikuwa "magaidi".

Alikanusha kwamba jeshi limekuwa likichoma vijiji na akasema kwamba PDP wanafanya mashambulio ya moto.

Ni vigumu kusema nilini vita vya wenyewe kwa wenyewe vinaweza kuisha lakini inaonekana kuna uwezekano kwamba mamilioni ya raia wa Myanmar wataachwa na kiwewe.

Na kadri itakapovyochukua muda kupata amani, wanawake wengi wanakabiliwa na uwezekano zaidi wa kuwa wahanga wa ubakaji Khin Htwe atakuwa na uwezekano mkubwa wa kukabiliwa na ghasia.

Anasema hataki tena kuishi baada ya kile kilichomtokea na anafikiria kujiua. Hajaweza kumwambia mchumba wake kwamba alibakwa.