Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Mzozo wa Ukraine: Je makombora ya masafa marefu yanayopelekwa na nchi za magharibi Ukraine yatabadilisha hali ya mambo kwa haraka?
Licha ya vitisho vya kuharibu uhusiano na Urusi, Uingereza inaipa Ukraine silaha za masafa marefu, ikifuatiwa na Marekani. Wachambuzi wanasema silaha hizi zenye ufanisi mkubwa zinaweza kugeuza hali ya mambo, lakini sio haraka.
Waziri wa Ulinzi wa Uingereza Ben Wallace anasema makombora hayo ya M270 yataisaidia Ukraine kujilinda dhidi ya uvamizi wa Urusi.
Hata hivyo Serikali haikubainisha ni silaha ngapi zilikuwa zikisafirishwa kwenda Ukraine. Kwa mujibu wa BBC, kwa sasa kuna mifumo mitatu ya makombora.
Wachambuzi wa masuala ya kijeshi wa Magharibi wanahusisha ushindi wa jeshi la Urusi dhidi ya Donbass, ikiwa ni pamoja na sehemu ya jiji la Severodonetsk, na ubora wake katika vifaa vizito na mizinga.
Jeshi la Ukraine linatumai kupelekwa kwa maroketi Ukraine kutoka nchi za Magharibi utasaidia kuwashinda vilivyo wanajeshi wa Urusi. Wiki iliyopita, Marekani ilitangaza kuwasilisha mfumo wa makombora wa masafa marefu wa M142 (HIMARS). Hii ilisababisha mashambulizi makali ya kujibu mapigo kutoka Moscow.
Siku ya Jumapili, Putin alitishia kuongeza wigo wa mashambulizi ambayo Moscow ingeyafanya ikiwa nchi za Magharibi zitaanza kupeleka silaha za masafa marefu kwa Ukraine.
Serikali ya Uingereza imetangaza kuwa katika wiki zijazo jeshi la Ukraine litashiriki katika mafunzo ya matumizi ya silaha mpya nchini Uingereza. Silaha hizo za roketi ya M270 inaweza kurusha makombora 12 na kulenga shabaha ndani ya eneo la kilomita 80 kwa dakika moja. Ni silaha ya masafa marefu inayopatikana kwa sasa katika jeshi la Ukraine.
"Kadiri mbinu za Urusi zinavyobadilika, ndivyo pia tunavyowaunga mkono Ukraine kwenye kukabiliana. Mfumo huu wa makombora wa masafa marefu wenye ufanisi mkubwa unawaambia marafiki zetu wa Ukraine kwamba Urusi inajilinda dhidi ya silaha za masafa marefu ambazo Urusi hiyo hiyo inatumia kuharibu miji ya Ukraine."
Mwandishi wa BBC Jonathan Billy anasema Uingereza na Marekani zinasambaza silaha nyingi kwa Ukraine, lakini uwasilishaji wa mfumo wa kisasa wa makombora ya masafa marefu ni mabadiliko makubwa.
Pia inakubali kwamba Ukraine haiwezi kushindana na silaha kubwa zaidi ya Urusi.
Uchambuzi: Makombora ya Magharibi hayawezi kubadilisha hali mara moja
Jack Watling, mchambuzi wa Uingereza kuhusu oparesheni za kijeshi za ardhini, alisema ahadi za Marekani na Uingereza za kuipatia Ukraine mfumo wa kisasa wa makombora ya masafa marefu itabadilisha hali ya mambo huko mbele, lakini si mara moja.
Alisema mfumo wa makombora wa M270 unaopelekwa Ukraine ni moja ya silaha za thamani zaidi za Jeshi la Uingereza.
Ni silaha nzito lakini raiawa Ukraine wana haja ya kufundishwa matumizi yake.
"Ikiwa Putin atatishia kushambulia zaidi nchini Ukraine ikiwa nchi za Magharibi zitatoa silaha za masafa marefu, itakuwa vigumu kufanya hivyo, kwa sababu Moscow tayari inahujumu maeneo muhimu na nafasi za kijeshi kwa uchumi wa Ukraine," alisema.
Kulingana na mwandishi wa BBC Joe Inwood huko Kyiv, mizinga inaweza kuchukua jukumu muhimu katika kupigania kuitetea Donbass. Silaha nzito zinazopelekwa Ukraine zinaweza kuviweka vikosi vya Urusi katika wakati mgumu ikiwa vitalengwa.
"Siku chache zilizopita, ilikuwa karibu hakika kwamba mji wa Severodonetsk utateketea. Lakini sasa waukraine wanashambulia, na hili linamaanisha kuwa itakuwa vigumu kwa Warusi kujisalimisha," alisema.