Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Jinsi sarafu ya Urusi ‘ruble’ inavyofanya vizuri zaidi Ulimwenguni licha ya vikwazo
Licha ya vikwazo, sarafu ya Urusi imekuwa sarafu inayofanya vizuri zaidi duniani dhidi ya dola mwaka huu, hata kuizidi sarafu ya Brazil real.
Sio hata kwa vikwazo vya haraka na vikali vya kiuchumi katika historia ya kisasa vilivyowekwa na nchi za Magharibi katika kukabiliana na uvamizi wa Ukraine havijaweza kuzuia ukuaji wake.
Miezi miwili tu baada ya thamani ya ruble kushuka kwa kasi hadi chini ya senti moja ya Marekani, sarafu ilichukua hatua za kushangaza.
Machi 7 ruble ilishuka sana chini kwa dola 0.007, mpaka sasa kwa mwaka huu sarafu ya Urusi imepanda thamani kwa takriban 15% dhidi ya sarafu ya Marekani na inafanya biashara kwa karibu 0.016.
Marufuku ya raia wake kuuza ruble ili kununua fedha za kigeni ilielezewa na Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Antony Blinken kama udanganyifu wa kifedha ambapo ni sera ambayo nchi hudhoofisha sarafu zao ili kuongeza ziada ya biashara zao,
Udhibiti huu ulitumika kufungia akiba nyingi za fedha za kigeni za Urusi wakati ambapo ilihitaji sana rasilimali hizi, ili kufidia uwekezaji na mtaji na kufadhili uvamizi wa kijeshi wa Ukraine, ambao umechukua muda mrefu kuliko ilivyotarajiwa.
Kesi ya Uturuki au Argentina
Kinachotarajiwa kuhusu ahueni hii ni kwamba nchi nyingine, kama vile Uturuki au Argentina, ambazo zililazimishwa kuweka hatua kama hizo, sio tu kwamba hazikupata matokeo sawa na Urusi, lakini sarafu za lira na peso zilipata matokeo mabaya.
Sarafu zote zimeshuka kwenye rekodi na bado zinapambana kurudi katika viwango vilivyokuwa.
Katika hatua yake ya dharura mara baada ya kujifunza juu ya adhabu ya kimataifa, Kremlin ilianza kuchukua hatua zisizojulikana kwa vizazi ambavyo havikuishi wakati wa Umoja wa Kisovyeti.
"Benki kuu ya Urusi ililazimika kuongeza viwango vya riba kwa kiasi kikubwa na kuongeza udhibiti wa mtaji kwa kukabiliana na vikwazo vya Magharibi," Ben Laidler, mtaalamu wa mikakati wa masoko ya kimataifa katika jukwaa la uwekezaji la eToro, aliiambia BBC Mundo.
"Viwango vya riba zaidi ya mara mbili hadi 20%. Wauzaji wa bidhaa nje ya nchi wa Urusi walilazimishwa kubadilisha 80% ya mapato yao ya kigeni kuwa rubles, na watu walikuwa na kikomo cha kiasi fulani wanachoweza kuhamisha nje ya nchi," anaongeza.
Na ni kwamba moja ya vikwazo vikubwa na vilivyoathiri zaidi Urusi ni kufungiwa kwa akaunti zake nje ya nchi.
Hatua nyingine ya kutetea sarafu yake ilikuwa kutaka nchi za Umoja wa Ulaya zinazonunua gesi asilia kutoka nchini humo zilipe bili zao kwa ruble, badala ya dola au euro.
Kulipiza kisasi kimkakati dhidi ya Ulaya
Nchi za Ulaya zinategemea sana gesi ya Urusi na licha ya mipango ya kutafuta vyanzo mbadala vya nishati, mradi wa Umoja wa Ulaya wa kusitisha usambazaji kutoka Urusi utachukua miaka mingi kukamilika.
Ujerumani, mmoja wa wateja wakubwa wa kampuni ya gesi ya serikali ya Urusi Gazprom, tayari imekubali kulipa kwa ruble pamoja na wanunuzi wengine wakubwa wa Ulaya.
"Uamuzi wa Urusi ni kulipa kisasi kimkakati dhidi ya EU, ikichukua fursa ya uwezo wake kama muuzaji mkuu wa gesi asilia kwa Ulaya. Bara la ulaya lilikuwa likipata karibu 40% ya gesi yake kutoka Urusi kabla ya vita vya Ukraine," anaelezea Levon Kameryan, mwandamizi. mchambuzi Scope Ratings.
Mwisho, bei ya juu ya bidhaa pia imesaidia sana.
Gharama kubwa zaidi za mafuta inamaanisha kuwa wateja wa Urusi sasa watalazimika kulipa dola zaidi kwa pipa na kwa hivyo wanahitaji ruble zaidi
Ufumbuzi wa muda mfupi
Hata hivyo, wataalam wanasema kwamba kuna mambo matatu - udhibiti mkali wa mtaji, viwango vya juu vya riba na bei ya juu ya bidhaa ambayo yameweza kupunguza tu kile ambacho kingkuwa mwaka "mbaya" kwa uchumi wa Urusi.
"Kupanda kwa kasi kwa ruble ni tatizo kwa wauzaji bidhaa nje na baadhi ya wazalishaji wa ndani, na kuongeza shinikizo la vikwazo. Pia inamaanisha mapato kidogo kwa bajeti," anasema Scott Johnson, mwanauchumi anayeshughulikia Uchumi wa Bloomberg nchini Urusi.
Lakini je, kurudi tena kwa ruble kunaweza kuonekana kama kipimo cha kupima iwapo vikwazo vya Magharibi vinafanya kazi?
Kwa Johnson "Kwa nje, Urusi inajaribu kuona kurudi kwa ruble kama ishara kwamba vikwazo havina athari inayotarajiwa. Lakini hiyo si sahihi kabisa."
"Kukubalika kumechangiwa kwa kiasi kikubwa na ubadilishaji wa lazima wa mapato ya mauzo ya nje na udhibiti mwingine wa mtaji, ambao unapunguza mzunguko wa pesa kutoka nje," anafafanua.
"Ruble inatoa picha sahihi ya usawa wa malipo, lakini sio ya uchumi wa chini, ambapo mtazamo ni mdogo," anasema.
Laidler anafikiria kwa njia sawa.
"Upinzani wa ruble sasa unaweza kuwa uemalizika. Nguvu ya sarafu ilifanya mauzo ya nje ya Urusi kuwa ya ushindani na vikwazo vikali vya Marekani vimeongeza uwezekano wa kushindwa kulipa deni."