"Nikiwa na miaka 18 nilifungwa, walikuwa wananilipa US$0.75 kwa saa kuwafulia nguo zao"

Chanzo cha picha, ANALÍA LLORENTE
Elizabeth "Rami" Gunn ni msichana mwenye umri wa miaka 21 ambaye, baada ya kifo cha George Floyd mnamo Mei 25, 2020 mikononi mwa polisi huko Minneapolis, Minnesota, aliandamana kwa miezi sita, maelfu ya maili kwenye mitaa ya jiji. Portland, Oregon.
Rami anasema tangu akiwa mdogo amekuwa akikabiliwa na ubaguzi wa rangi. Alichukuliwa na familia ya kizungu, aliishi mitaani kwa muda na alifungwa kwa ugomvi wa familia.
Anasema kwamba kwa miaka mingi alikuwa na hasira na jamii, na polisi na fikra zao, lakini anasema kwamba bado ana matumaini kwamba watu watabadilika.
Sasa anafanya kazi kama mlezi wa wazee walio na ugonjwa wa akili na anasema kwamba muhimu zaidi kwake ni kusaidia wengine.
Hii ni simulizi yake.
Nimeteseka kwa ubaguzi wa rangi tangu nikiwa mdogo.
Uzoefu wangu wa kwanza ulitokea kwa binamu yangu, wakati aliniponiambia uso kwa uso kwamba hatukuwa na uhusiano, kwamba hatukuwa rangi moja.

Chanzo cha picha, GENTILEZA ELIZABETH GUNN
Wakati huo sikuelewa. Baadaye niliumia. Tulipokua, binamu yangu alielewa athari alizonisababishia na akaomba msamaha.
Ni jambo linaloendelea kutokea. Ninaliona kila siku kila mahali.

Chanzo cha picha, ELIZABETH GUNN FACEBOOK
Niliamua kuandamana kupinga hili kwa sababu nimekuwa nikifanya kazi kwa bidii ili nisiandikwe "mwanamke mweusi mwenye hasira" na nimefanya kazi kwa bidii ili watu wanielewe na sio kunifananisha.
Kuwanyima fedha polisi
Hakuna kitu ambacho kinaweza kutatua ubaguzi wa rangi kwa urahisi.
Hivi sasa ninafanya kazi na wagonjwa wenye matatizo ya akili.
Lakini napenda kazi yangu. Ninafanya hivyo kwa sababu watu hawa ni wa ajabu na wana haiba nzuri. Na ninawasaidia, hilo ndilo jambo pekee ambalo ni muhimu kwangu.

Chanzo cha picha, GENTILEZA ELIZABETH GUNN
Tunataka kuwanyima pesa polisi ili kuwaondoa wale watu ambao hawataki kubadilika ili wawe bora kwa jamii zingine, haswa na jamii ya watu weusi.
Ikiwa hutabadilika, hatutaki uwe na uwezo wa kutuumiza sana. Hujafunzwa wala kuelimika kwa kazi hiyo (kuumiza), kwa hivyo hupaswi kuifanya.
Nilipokuwa na umri wa miaka 18, nilifungwa kwa miezi michache, kwa sababu ya ugomvi wa familia, na ilinibidi kufanya kazi mfululizo. Nililipwa Dola za Marekani 0.75 kwa saa ili kufua nguo. Kama huo sio utumwa, ni nini?
Mwisho wa siku kupambana na ubaguzi wa rangi itabidi iwe kazi ya kila mtu.

Chanzo cha picha, GENTILEZA ELIZABETH GUNN
Imani kwa watu
Baada ya kuandamana tulipiga hatua kidogo kwa juhudi tuliyoiweka.
Nina imani kwamba watu wanataka kweli kubadilika. Ninaona mabadiliko. Ninaona watu kila siku wakijaribu kuelewa zaidi kiasi. Sasa kuna ufahamu na unasikia mwenyewe ukisema, "Wewe ni mbaya sana." Ikiwa ni ubaguzi kulingana na rangi ya ngozi, rangi, jinsia, kazi, nk.

Chanzo cha picha, ANALÍA LLORENTE
Nadhani tusingeanza kuandamana jinsi tulivyofanya, hakuna ambaye angesimama na kusema, "Sikubaliani na hili."
Ni hatua kidogo, lakini inatosha kuwa na dumisha tumaini hai.
Usifikiri hakuna mabadiliko. Na usifikirie kuwa tutaacha kupambana.












