Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Mwaka mmoja baada ya kifo cha Abubakar Shekau: Mashambulizi 12 mabaya zaidi ya Boko Haram nchini Nigeria ambayo hayatasahaulika.
Mwaka mmoja baada ya kifo cha kiongozi wa Boko Haram Abubakar Shekau, kumekuwa na ongezeko la wanachama wa kundi hilo wanaojisalimisha kwa jeshi la Nigeria.
Tangu kifo cha kiongozi wa kundi hilo, sifa za kundi hilo zimevunjwa, na hali ya sintofahamu imetawala, huku baadhi ya wanachama wake na watu muhimu wakijisalimisha kwa jeshi la Nigeria.
Kifo cha Abubakar Shekau, kiongozi wa miaka 12 wa kundi la waasi la Boko Haram, ambalo limefanya mashambulizi mabaya zaidi nchini Nigeria, Niger, Cameroon na Chad kilianza Mei 19, 2021.
Kabla ya kifo cha Shekau mnamo Mei 2021, angalau mara nne kifo chake kiliripotiwa, lakini alijitokeza kukanusha.
Tangu kuchukua uongozi wa Boko Haram mwaka 2009, Shekau amekuwa akikosolewa vikali kwa ukatili wake kaskazini mashariki mwa Nigeria, pamoja na kaskazini magharibi na kaskazini-kati mwa Nigeria, na kwingineko ambako kulimfanya kuwa maarufu.
Katika kuadhimisha mwaka mmoja wa kuondoka kwake, BBC Hausa inaangalia nyuma mashambulizi 12 kati ya hayo mabaya yaliyoongozwa na Shekau wakati wa miaka 12 madarakani, ambayo yameibua sintofahamu duniani kote.
Shambulizi la 1
Shambulio la kwanza ambalo lilitikisa watu wa Nigeria na kuvuta hisia za kimataifa na kundi chini ya Shekau lilikuwa shambulio la makao makuu ya polisi huko Abuja mnamo Juni 16, 2011.
Ingawa watu wawili waliuawa, alikasirishwa kuona mji mkuu wa Nigeria kwa mara ya kwanza.
Shambulizi la 2
Miezi miwili baadaye, kundi hilo lilifanya shambulizi jingine la bomu kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa katika mji mkuu wa Nigeria, Abuja, na kuua takriban watu 21.
Hili lilikuwa tukio la pili baya zaidi chini ya utawala wa Shekau mnamo Agosti 27, 2011.
Shambulizi la 3
Msururu wa mashambulizi ya mabomu ukatokea kwenye makanisa huko Jos na Madalla huko Suleja Siku ya Krismasi 2011.
Siku hiyo hiyo, kulikuwa na mashambulizi zaidi huko Damaturu na Gadaka katika Jimbo la Yobe. Aidha, kulikuwa na majeruhi katika matukio hayo.
Shambulizi la 4
Bila shaka, Wanigeria hawatawahi kusahau Januari 20, 2012.
Ilikuwa ni siku ambayo Boko Haram walifanya mfululizo wa mashambulizi kwa wakati mmoja katika mji mkuu wa kibiashara wa kaskazini mwa Nigeria, Kano, na kuripotiwa kuua zaidi ya watu 180.
Mara nyingi, Shekau alipoamuru mfululizo wa mashambulizi mabaya, alionekana kwenye video kutangaza matendo yake.
Wakati wa mashambulizi ya Kano pia alionekana kwenye video akisema alifurahia kuua watu - kama vile alivyofurahia kuua kuku na kondoo.
Shambulizi la 5
Mnamo Aprili 16, 2013, Boko Haram walifanya shambulio la tano kubwa, mauaji ya Baga katika Jimbo la Borno, ambapo takriban watu 187 waliuawa.
Baada ya hapo, Baga ilishuhudia mauaji mengine ya kutisha Januari 2015 ambapo watu 150 waliuawa.
Shambulizi la 6
Uhalifu wa sita wa kutisha ulioamriwa na Shekau ulikuwa mauaji ya Februari 30, 2014 ya wanafunzi 59 wa kiume wa Shule ya Sekondari ya Serikali ya Shirikisho huko Buni Yadi, Jimbo la Yobe.
Walifanya hivyo kwa kuwapiga risasi baadhi na kuwachinja wengine, kulingana na ripoti hiyo.
Shambulizi la saba
Mnamo Aprili 14, 2014, mabomu mawili yalilipuka katika kituo cha mabasi cha Nyanya katika Jimbo la Nasarawa, karibu na Abuja, na kuua watu 88 na kujeruhi wengine karibu 200.
Shambulizi la nane
2014 unaonekana kuwa mwaka mbaya zaidi kwa Shekaru, kwani siku moja tu baada ya shambulio la Nyanya, habari za kutekwa nyara kwa wasichana wa Shule ya Upili ya Chibok katika Jimbo la Borno ziliibuka.
Wizi huu ni mtindo wa Shekau wa kuvutia watu wengi zaidi na kuwa gumzo tena machoni pa ulimwengu.
Video iliyosambaa sana ikimuonyesha akicheka akimwambia jinsi ya kuwauza wasichana hao au kuwaoa, inaonyesha yeye ni mtu wa aina gani.
Wengi wa wasichana hao walinusurika, na kwa watoto na wazazi wao na watu wengine katika eneo hilo wataendelea kuhisi athari za kutekwa nyara hata sasa baada ya kifo chake.
Shambulizi la tisa
Mnamo Septemba 2, 2014, kikundi hicho kilifanya shambulio lingine baya huko Bama, Jimbo la Borno, na kuua watu kadhaa.
Ahmed Zanna, mbunge wa jimbo hilo wakati huo, aliambia BBC kwamba siku mbili baada ya shambulio hilo, wapiganaji wa kundi hilo walizuia maziko hayo.
Baadaye serikali ilitangaza kwamba Boko Haram wamechukua udhibiti wa Bama, na kwamba karibu watu 26,000 wamekuwa wakimbizi.
Shambulizi la kumi
Mnamo tarehe 28 Novemba 2014, kikundi hicho kilifanya shambulio lingine baya kwenye Msikiti Mkuu siku ya Ijumaa huko Kano karibu na kasri ya kifalme.
Takriban waumini 120 waliuawa katika kile kilichojulikana kama "Mauaji ya Ijumaa."
Shambulizi la 11
Mnamo Desemba 9, 2016, mabomu mawili yalilipuka Madagali, Jimbo la Adamawa na kuua watu 57 na kujeruhi 177.
Shambulizi la 12
Shambulio la 12 ni baya zaidi na Umoja wa Mataifa unasema takriban watu 110 waliuawa katika shambulio la Boko Haram dhidi ya wakulima karibu na Maiduguri mnamo Novemba 2020.
Gavana wa Jimbo la Borno Babagana Umara Zulum aliongoza mazishi ya wahanga wa mauaji ya Boko Haram huko Zabarmari, eneo la Serikali ya Mtaa ya Mafa katika Jimbo la Borno.
Wachambuzi sasa wanaona kifo cha Shekau kuwa pigo kwa nguvu ya kikundi, lakini hakitasahaulika.
Licha ya ukatili wa Shekau, vikosi vya Nigeria, Niger, Chad na Cameroon pia vimefanikiwa dhidi yake na wapiganaji wake.
Na mwishowe inaweza kusemwa kuwa jamii za nchi hizi nne zimeshinda, baada ya mtoto huyu kushindwa, ambaye hatimaye inaripotiwa kwamba alijiua.