Roe v Wade: Wanawake nchini Marekani wanaweza kupoteza haki ya utoaji mimba

Chanzo cha picha, Getty Images
Mamilioni ya wanawake kote nchini Marekani wanaweza kupoteza haki yao ya kisheria ya kutoa mimba hivi karibuni, kulingana na hati ya Mahakama ya Juu iliyovuja.
Waraka huo, uliochapishwa katika gazeti la Politico, unaonyesha kuwa mahakama ya juu zaidi nchini humo inatarajiwa kutengua uamuzi wa mwaka 1973 ambao ulihalalisha kisheria utoaji mimba kote nchini humo.
Kama mahakama itapinga hukumu ya Roe dhidi ya Wade maarufu Roe v Wade, majimbo yataruhusiwa kila moja kupiga marufuku utoaji mimba, iwapo yatataka kufanya hivyo.
Inatarajiwa kuwa iwapo hilo litatokea karibu nusu ya majimbo yote ya Marekani yataweka marufuku ya kutoa mimba.
Majaji wa mahakama ya juu ya Marekani wanatarajiwa kutoa uamuazi mwishoni mwa mwezi Juni au mapema mwezi Julai
Sharia ya Roe v Wade ipo inaangaliwa vikali na mahakama kwa sababu jimbo la Mississippi nchini humo inaomba ibatilishwe.
Majaji walisikiliza kesi hiyo mwezi Desemba mwaka jana.
Majimbo kumi na moja tayari yamepitisha kile kinachojulikana kama sheria za kuchochea ambazo zitapiga marufuku utoaji mimba moja kwa moja ikiwa Roe atabatilishwa msimu huu wa joto.
Baadhi ya wanawake milioni 36 wanaweza kupoteza uwezo wa kutoa mimba, kulingana na utafiti kutoka Planned Parenthood, shirika la afya ambalo hutoa huduma ya utoaji mimba.
Vikundi vinavyopinga hatua ya kutoa mimba kama vile Orodha ya Susan B. Anthony vilikaribisha habari hiyo. "Iwapo Roe atapinduliwa, kazi yetu itakuwa ni kujenga maelewano kwa ajili ya ulinzi mkali unaowezekana kwa watoto ambao hawajazaliwa," ilisema.

Chanzo cha picha, Reuters
Lakini Hati iliyovuja iliyoandikwa rasimu ya kwanza inaonekana kuakisi maoni ya wengi wa mahakama, na Politico inaripoti kwamba iliandikwa na Jaji Samuel Alito na kusambazwa ndani ya mahakama tarehe 10 Februari mwaka huu.
Lakini bado haijulikani ikiwa inawakilisha maoni ya mwisho, kwani majaji wamebadilisha maoni yao hapo awali wakati wa mchakato wa kuandaa rasimu.
Mahakama ya Juu na Ikulu ya Marekani bado hazijatoa maoni yoyote kuhusiana na suala hilo.
Kuchapishwa kwake siku ya Jumatatu usiku kulizua malalamiko ya mara moja kutoka kwa wanachama wa Democrats pamoja na maandamano ya wanaharakati wanaounga mkono uchaguzi na kupinga uavyaji mimba nje ya mahakama huko Washington DC.
Wanasiasa wakuu wa Kidemokrasia Nancy Pelosi na Chuck Schumer wamesema kwa pamoja kwamba ikiwa ripoti hiyo ilikuwa sahihi, Mahakama ya Juu "iko tayari kuweka kizuizi kikubwa zaidi cha haki katika miaka 50 iliyopita".
Magavana wa demokrats wa majimbo kadhaa yakiwemo California, New Mexico na Michigan walitangaza mipango ya kuweka haki za uavyaji mimba ndani ya katiba zao hata kama mahakama itabatilisha sheria Roe v Wade.
"Hatuwezi kuamini [Mahakama Kuu] kulinda haki ya kutoa mimba, kwa hivyo tutafanya sisi wenyewe," Gavana wa California Gavin Newsom alituma katika mtandao wake wa Twitter.
Chombo cha habari cha Politico kilichapisha waraka huo uliovuja kwa ukamilifu, na kumnukuu Jaji Alito akisema: "Roe alikosea sana tangu mwanzo. Mawazo yake yalikuwa dhaifu sana, na uamuzi huo umekuwa na matokeo mabaya.
"Na mbali na kuleta suluhu ya kitaifa ya suala la utoaji mimba, imezua mjadala na kuzidisha mgawanyiko."
Makundi hasimu ya waandamanaji yaliendelea na maandamano nje ya Mahakama ya Juu Jumanne, huku wanaharakati wa kupinga uavyaji mimba wakiimba "Roe v Wade inabidi iondoke" na wafuasi wa haki za uavyaji mimba wakipaza sauti "kutoa mimba ni huduma ya afya".
"Hawataepuka jambo hili," mwanaharakati Mchungaji Wendy Hamilton aliambia shirika la habari la Reuters. "Kuna wengi wetu kuliko walio nao, na tutapigana."
"Hii inasambaratisha kila kitu ambacho tumefanyia kazi," mwandamanaji mwingine alisema.

Mahakama ya Juu imeundwa upya na teuzi tatu chini ya Rais wa zamani Donald Trump, na imeitwa yenye mwelekeo wa kihafidhina zaidi katika historia ya kisasa ya Marekani.
Majaji sita kati ya tisa wa sasa waliteuliwa na marais wa Republican. Wengine watatu walichaguliwa na marais wa demokratiki. Mahakama inahitaji wingi wa kura ili kutoa uamuzi.
Politico inaripoti kuwa Jaji Alito na majaji wengine wanne walioteuliwa na Republican - Clarence Thomas, Neil Gorsuch, Brett Kavanaugh na Amy Coney Barrett - wanaunga mkono hatua hiyo dhidi ya Roe v Wade lakini haijabainika wazi jinsi Jaji Mkuu John Roberts atapiga kura.
Wanawake katika miaka yao ya 20 ndio idadi kubwa ya watoaji mimba, katika mwaka 2019 karibu 57% walikuwa katika kundi hili la umri.
Wamarekani weusi huavya mimba kwa kiwango cha juu zaidi ,27 kwa kila wanawake 1,000 wenye umri wa miaka 15-44.














