Mzozo wa Ukraine: Vidonge vya uzazi wa mpango vyasambazwa Ukraine kulinda wanawake wanaobakwa vitani

Lviv

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Mmoja wa watu wa kujitolea akitoa msaada kwa akina mama huko Lviv, Ukraine mwezi March

Mashirika ya misaada yanafanya kazi ya kupeleka vidonge vya dharura vya uzazi wa mpango katika hospitali za Ukraine wakati ripoti za ubakaji zikiongezeka. Karibu pakiti 3,000 za vidonge hivyo zimepelekwa katika maeneo ya nchi hiyo yaliyoathiriwa zaidi na uvamizi wa Urusi.

Shirikisho la Kimataifa la Uzazi wa Mpango (IPPF) limetoa tembe hizo, ambazo watu wa kujitolea wanazitoa. Caroline Hickson, kutoka kundi hilo, anasema muhimu kwenda na na muda sahihi wakati zinaposambazwa.

"kuna siku tano ambapo [kidonge] kina ufanisi katika kuzuia mimba," aliiambia BBC.

"Kwa hiyo kama umekuwa mwathirika wa unyanyasaji wa kijinsia ni muhimu kumeza haraka iwezekanavyo, kwa sababu kupata ujauzito kutokana na ubakaji ni jambo la kuhuzunisha sana." Shirika hilo pia limekuwa likituma tembe za kutoa mimba kwa sababu za kimatibabu, ambazo zinaweza kutumika hadi wiki 24 za ujauzito.

Bi Hickson alisema dawa hizo zipo kwa ajili ya kuwasaidia wanawake katika hali mbalimbali, ikiwa ni pamoja na wale wanaofanya mapenzi ya makubaliano lakini wanahisi kuwa ni wakati usio sahihi wa kupata mtoto.

"Kabla ya vita iliwezekana kupata dawa za dharura za uzazi wa mpango nchini Ukraine, lakini minyororo ya usambazaji imevurugwa na kwa wanawake kwa ujumla ni muhimu sana kufikiwa na huduma hii," alisema.

UN

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Umoja wa Mataifa umekuwa ukitoa misaada pia ya nepi kwa ajili ya watoto

Watu wengi wamekuwa wakihamahama na kukimbia kote Ukraine, kwa hivyo ni vigumu kwa wafanyikazi wa misaada kujua kwa kiwango gani dawa hizo zinahitajika na katika maeneo gani hasa. Wiki iliyopita, wanajeshi wa Ukraine walitoa ombi la chakula na dawa kwa ajili ya mji wa Mariupole, ambao umekuwa vigumu kufikisha misaada kutokana na zuio la uwepo wa wanajeshi wa Urusi.

IPPF imekuwa ikifanya kazi na Mfuko wa Umoja wa Mataifa wa Idadi ya Watu na Shirika la Kimataifa la Matibabu kwa Brig Supplement ya Tablet Intu Ukraine. HickSon Saeed: "Mashirika ya Umoja wa mataifa, mashirika ya kiraia na Wizara ya Afya yanashirikiana kwa pamoja, katika kutambua mahitaji na kutufahamisha sote tunaofaanya kazi yakusaidia.

"tukafahamishwa baadae kwamba ni hospitali gani inahitaji msaada wa vifaa na dawa kwa ajili ya wanawake waliobakwa."Umoja wa Mataifa umekuwa ukijumuisha vidonge vya uzazi wa mpango vya dharura na kupelekwa kwa wanawake na wasichana waliokumbwa na migogoro duniani kote.

Wamefanya hivyo pia nchini Ukraine, ambapo pamoja na kutuma vidonge vya uzazi wa mpango nwamekuwa wakitoa pia nepi kwa ajili ya watoto. BBC imekuwa na taaarifa zenye Ushahidi za wanawake wa Ukraine kubakwa na askari wanaovamia vijiji wakati huu wa vita, maili chache kutoka mji wa Kiev. Vyombo vingine vya habari vimeripoti habari kama hizo kutoka mji wa Bucha, Kaskazini-Magharibi mwa Kiev.

Zingatia: Kwa muktadha wa taarifa hii, 'mimba zisizokuwa na baba', inamaanisha ni ujauzito uliotokana na vitendo vya ubakaji vinavyofanywa na wanajeshi wanaoivamia vijiji na kuwabaka wanawake huko Ukraine.